Jumapili, 1 Desemba 2013

WILAYA YA KILOLO YAWAPATIA MSAADA WA MBUZI WAATHIRIKA

Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo- Mkoni Iringa
 Wataalamu wa masauala ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Kilolo, wa kwanza kulia ni Bi. Faraja Chaula, mratibu wa Ukimwi Wilaya ya Kilolo, akiwa na kaimu mganga mkuu wa Wilaya ya Kilolo Bw. Nimroad Chengula.
 Bi. Faraja Chaula akisikiliza kwa makini jambo, katika moja ya vikao vya baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, akiwa na kaimu mganga mkuu wa Wilaya ya Kilolo Bw. Nimroad Chengula.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya kilolo Mh. Joseph Muumba (mwenye joho jekundu) akiwa na makamu mwenyekiti wake, katika moja ya vikao vya baraza la madiwani.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya kilolo Bi. Rukia Muwango akiwa ndani ya ukumbi wa mikutano katika Halmashauri yake, wakati wa kikao cha baraza la madiwani. 
 Bw. Benson Kilangi mmoja wa maafisa wilayani Kilolo akisikiliza jambo na mkurugenzi Bi. Rukia Kiwango katika ukumbi wa mikutano wa Wilaya hiyo.
 Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo wakiwa katika majukumu yao ndani ya kikao  cha baraza la madiwani.
 Jengo la halmashauri ya Wilaya ya kilolo.

 <<<<<HABARI>>>>>
 HALMASHAURI ya Wilaya ya Kilolo imetoa msaada wa Mbuzi 18 kwa waathirika wa ugonjwa wa ukimwi wa kikundi cha Matumaini kilichopo kijiji cha Kitumbuka, msaada wenye lengo la kuwaongezea mtaji katika kukuza uchumi wao na kuwaepusha na hali duni.

Akikabidhi Mbuzi hao wenye thamani zaidi ya shilingi Milioni 1 na nusu, katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani, iliyofanyika katika Kijiji cha Kitumbuka, mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Mh.Joseph Muhumba amesema msaada huo utawawezesha waathirika hao kuendelea kuzihudumia familia zao.

Aidha Muumba amesema jamii inatapaswa kufahamu kuwa waathirika wa ugonjwa wa ukimwi wanauwezo wa kuchangia shughuli za maendeleo kwa kufanya kazi, huku akiwataka wananchi kutambua kuwa kupata maambukizi sio mwisho wa maisha.

Amesema mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi ni jukumu la kila mmojawapo na hivyo jamii iache kuona kuwa wajibu huo niwa Taasisi, Mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na serikali, kwani fikra hizo ni potofu.

Amewataka wananchi kuona ugonjwa huo ni sawa na magonjwa mengine kwa kuupa kipaumbele katika kupima, na kuacha tabia ya unyanyapaa kwa wathirika, kwa kuwa nao wanao mchango mkubwa wa maendeleo na uchumi katika Taifa.

“Ndugu zangu, ugonjwa huu mnapaswa kuuona kama yalivyo magonjwa mengine, muwe na utayari wa kupima ili mjue afya zenu kama mnavyofanya kwa maradhi mengine, lakini hata ukigundulika unamaambukizi siyo mwisho wa maisha yako, unatakiwa kuzingatia tu ushauri wa wataalamu na kasha kuendeleza majukumu ya maendeleo kama kawaida, siyo mtu unatambulika umeathirika sasa hata kazi hufanyi, au wananchi wanaona kuwa wewe ndiyo huna mchango, hapana, tunatakiwa kubadili sana fikra hizo potofu kwa ukimwi ni ugonjwa kama maradhi mengine kama Malaria, na yatupasa sote tuwajali na kuwapa faraja wenzetu walioathirika ili waweze kuishi,” Alisema Muumba.

Pia Muumba amewasihi wale wote wanaoishi na VVU na kutumia dawa za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV’s) kuacha tabia ya kutofuata masharti ya matibabu yao, kwa madai kuwa kupuuzia dawa hizo kunawasababishia wao wapoteze maisha.

Semeni Monge mmoja kati ya wanufaika wa msaada huo wa Mbuzi amesema, msaada huo utawaboresha maisha yao, kwani  madai kuwa mifugo hiyo wataitumia kama mtaji wa kukuza uchumi katika kuzihudumia familia zao. 

Mwenyekiti wa kikundi cha Mshikamano, cha wanaoishi na Virusi vya ukimwi Bw. Leonard Chusi amesema msaada huo unaongeza imani kwao ya kuwa jamii inawajali, tofauti na awali jamii ilivyokuwa na tabia ya kunyanyapaa, jambo lililochangia baadhi yao kupoteza maisha kwa hofu.

Hata hivyo  mratibu wa Ukimwi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Bi. Faraja Chaula amesema Wilaya hiyo ina asilimia 9.1 cha watu wanaoishi na Virus vya Ukimwi, na kuwa sababu kubwa ya tatizo hilo ni pamoja na jamii kuendekeza mila na destuli potofu zilizopitwa na wakati.

Bi. Chaula amesema pia tatizo la ulevi wa kupindukia na jamii kutotumia Kondomu kwa usahihi wakati wa kujamiiana ni sababu zinazochangia maambukizi mpya ya VVU na hivyo kuwepo na idadi kubwa ya waathirika wa ugonjwa huo wa Ukimwi.

“Zipo sababu nyingi zinazochangia ongezeko la watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi katika Wilaya yetu ya Kilolo, sababu hizo ni Ulevu uliokithiri, jamii kuendeleza mila na destuli zilizopitwa na wakati kama vile imani za kulogwa, kurithi wajane/ wagane bila kupima afya zao, kuhudumia wagonjwa pasipo kuchukua tahadhari ya kujikinga, lakini pia kuna tatizo la jamii kutotumia Kondomu kwa usahihi na muda wote wakati wa kujamiiana, huku mwingiliano mkubwa wa watu unaosabishwa na uwepo wa barabara kuu itokayo Dar es salaam kuelekea Mbeya, ni suala linalochangia Wilaya yetu kuwa na  idadi kubwa ya wafanyabiashara wa mali mbichi na mali kavu,” Alisema Chaula.

MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni