Jumapili, 18 Mei 2014

CHUO KIKUU IRINGA CHAZINDUA CHAMA CHA KISWAHILI


Baadhi ya majengo ya chuo kikuu cha Iringa zamani kilifahamika kama Tumaini.
 Tula Tweve, Muhadhiri wa Kiswahili chuo kikuu cha Iringa (Tumaini) akizungumza na wanafunzi wa chuo siku ya uzinduzi wa chama cha wanafunzi wa Kiswahili wa vyuo vikuu Afrika Mashariki.
  Albert Chalamila mkuu wa idara ya Lugha na Stadi za mawasiliano, akizungumza na wanachuo siku ya uzinduzi wa chama cha wanafunzi wa Kiswahili wa vyuo vikuu Afrika Mashariki.
 Enock Ugulumo - naibu makamu mkuu wa chuo utawala na fedha chuo kikuu cha Iringa, akitoa wosia kwa wanafunzi wa Kiswahili Afrika mashairiki, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu cha Iringa.
Dr. Newton Kyando mkuu wa kitivo cha Sayansi na taaluma za ualimu, akizungumza na wanafunzi wa chuo siku ya uzinduizi wa chama cha wanafunzi wa Kiswahili wa vyuo vikuu Afrika Mashariki.
 Gervas Amos- Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa,  akizungumza na wanafunzi wa chuo siku ya uzinduizi wa chama cha wanafunzi wa Kiswahili wa vyuo vikuu Afrika Mashariki.
 Keki ikikatwa kuashiria uzinduzi wa CHAWAKAMA.
 Keki ya uzinduzi wa CHAWAKAMA.
 Tula Tweve, Muhadhiri wa Kiswahili chuo kikuu cha Iringa (Tumaini) akiandika kumbukumbu za changamoto zinazotolewa na wanafunzi katika hafla ya uzinduzi wa chama cha wanafunzi wa Kiswahili wa vyuo vikuu Afrika Mashariki.
 Aggnes Ernest Kowi mmoja wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa, akiwa na wenzake katika hafla ya uzinduzi wa CHAWAKAMA.
Baadhi ya wanafunzi washiriki wa hafla hiyo wakisikiliza jambo katika siku hiyo ya Uzinduzi wa CHAWAKAMA.
 Philicanus Lukinga. Mwenyekiti mstaafu wa chama cha Kiswahili chuo kikuu cha Iringa (Tumaini), akiwa katika hafla hiyo, kulia ni Tula tweve muhadhiri wa Kiswahili chuo kikuu cha Iringa.
 Baadhi ya wanafunzi washiriki wa hafla hiyo wakisikiliza jambo katika siku hiyo ya Uzinduzi wa CHAWAKAMA.
 Baadhi ya wanafunzi washiriki wa hafla hiyo wakisikiliza jambo katika siku hiyo ya Uzinduzi wa CHAWAKAMA.


<<<HABARI>>>.

CHAMA cha wanafunzi wa Kiswahili, wa vyuo vikuu Afrika mashariki (CHAWAKAMA), kimeitaka jamii kutumia lugha ya Kiswahili, katika mawasiliano, ili kuitangaza zaidi Tanzania katika mataifa mengine.

Hayo yamezungumza na wanachuo, katika uzinduzi wa chama hicho cha CHAWAKAMA, uliofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu cha Iringa (Tumaini) kilichopo manispaa ya Iringa., uzinduzi uliohudhuriwa na wasomi mbalimbali.

Dr. Newton Kyando mkuu wa kitivo cha sayansi na taaluma za ualimu amesema Kiswahili ni hazina ya maendeleo, na kuwa Lugha hiyo ni zaidi ya utamaduni ambao unaweza kukuza soko na hivyo kuinua  uchumi wanchi.

Dr. Kyando amesema katika kioo cha utandawazi Lugha hiyo ya Kiswahili inaonekana kuwa ni nyenzo ya kiuchumi, na hivyo cham hicho kionekane kama ni chama cha watumiaji wa Lugha ya Kiswahili, pasipo kuwaachia wanafunzi wa Kiswahili pekee.

Aidha amesema lugha hiyo si tunu pekee ya watanzania bali niya sfrika mashariki, na inapaswa kulindwa na kutoiona kama ni lugha au somo pekee, hatua ambayo jamii inaiona lugha hiyo niya wasomi pekee, huku akiwataka wataalamu wa lugha kuondoa dhana ya kuwa Kiswahili ni finyu na hakijitosherezi.

Albet Chalamila mkuu wa idara ya Lugha na stadi za mawasiliano amesema Kiswahili kinapaswa kutumika kama lugha ya maarifa, na si kama inavyoonekana sasa kuwa ni lugha ya mawasiliano pekee.

Chalamila amesema wasomo wanatakiwa wasipindishe lugha hiyo kwa makusudi , huku akiiasa jamii kuacha kasumba ya kusahau utaifa wao kwa kuthamini lugha za kigeni ambazo baadhi yake hazina uwanja mkubwa kama ilivyo kwa lugha hiyo ya Kiswahili.

“Hoja yangu ya msingi hapa ni kuwa tunapaswa kuifahamu vyema lugha ya Kiswahili lakini pia tunapaswa kuifahamu vyema lugha ya kiingereza, kwa sababu moja tu ya kozi ya sarufi linganishi,” Amesema Chalamila.

Naye muhadhiri wa Kiswahili wa chuo kikuu cha Iringa Tula tweve, amesema watanzania ifike wakati waepukane na dhana ya kuwa Kiswahili ni somo dhaifu tofauti na masomo mengine, na kuwa somo la Kiswahili ni somo bora.

Tweve ametoa wito kwa wajumbe wa bunge la katiba, viongozi pamoja na wananchi kuzingatia matumizi bora na sahihi ya lugha ya Kiswahili nchini, kwa madai kuwa lugha hiyo ni Lulu ya Taifa, na kutoegemea lugha nyingine za kigeni.

“Nitoe wito hasa katika mchakato huu wa katiba mpya, wajumbe wa bunge la katiba, viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wote kwa ujumla, natamani sana kipengele moja wapo katika katiba kikazingatia matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili, nina maana katika Nyanja zote hasa Nyanja ya kielimu,” amesema Tweve.

………..Wanazuoni mbalimbali na wanachuo mbalimbali siyo kwamba wanashindwa kufaulu katika masomo yao siyo kwamba hawana uwezi, hapana!!Kwa sababu lugha ya Kiswahili ni lugha yao ya Taifa ambayo wanaitumia kila siku katika shughuli mbalimbali, lakini lugha hii endapo ingekuwa inatumika katika mtaala kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu naamini tungekuwa tunawanazuoni bora zaidi kuliko  lugha nyingine,” Alisema.

Enock Ugulumo - naibu makamu mkuu wa chuo utawala na fedha chuo kikuu cha Iringa,amesema wanafunzi wanapaswa kujifunza lugha kwa ufasaha zaidi ili wawe wa kimataifa wakubalike kwa kuwafunza na wageni kutoka nje ya nchi wanaokuja nchini.

Ugulumo amesema Kiswahili kikichukuliwa kwa hali halisi na kuthaminiwa kitaongeza nafasi kubwa za ajira kwa watanzania, kwani ni lugha niya utandawazi inayokuza biashara kimataifa.

Kenneth Komba afisa michezo mkoa wa Iringa ambaye alikuwa mgeni rasmi wa uzinduzi huo wa CHAWAKAMA amesema hata mikataba mibovu inayoingiwa na baadhi ya viongozi nchini inatokana  na changamoto ya lugha.

“Unakuta kitabu kina kurasa zaidi ya miamoja, kiingereza chenyewe cha kuokotaokota, kwa sababu  lugha siyo yakwetu, unasaini mambo mengine kumbe ni bomu, lakini kama ingekuwa inatumika lugha ya Kiswahili ambayo tunaielewa vyema hizo changamoto ambazo zipo kwenye mikataba ingekuwa rahisi kuzibaini,” Alisema Komba.

Hata hivyo amesema katika suala la kudidimiza Kiswahili, hakuna mtu wa kurushiwa lawama, kwani wao wasomi ndiyo wanaongoza katika kuidharau lugha hiyo, kwa kutokizungumza mara kwa mara, na badala yake wamekuwa wakitumia zaidi lugha za kigeni ili kujikweza na kujitofautisha na watu wengine.
MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni