Ijumaa, 15 Agosti 2014

PARETO YAIWAKIRISHA TANZANIA KWA KUINGIZA MABILIONI.


 Zao la Pareto likiwa  Shambani.
 Ramani ya Tanzania ikionyesha mikoa ambayo inalima zao la Pareto
 Kushoto ni Ephraem Mhekwa Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Pareto akiwa na  Gerlad Chuwa (Kulia) ambaye ni mdhibiti wa zao la Pareto nyanda za juu kusini.
 Ephraem Mhekwa Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Pareto akiwa na  Gerlad Chuwa (mwenye miwaniKulia) ambaye ni mdhibiti wa zao la Pareto nyanda za juu kusini.
 Semu Kalekezi mtaalamu wa maabara ya Pareto akiwa na Tumaini Ngajilo (Mwenye kofia) Mtakwimu bodi ya Pareto akitoa maelezo juu ya bidhaa zitokanazo na zao la Pareto.

 Semu Kalekezi mtaalamu wa maabara ya Pareto.
 Shamba la Pareto.
 Kutoka kulia ni Semu Kalekezi, mtaalamu wa maabara (katikati) ni Innocent Mogha na wakwanza kushoto ni Tumaini Ngajilo mtakwimu wa bodi ya pareto, wakiwa katika shamba la Pareto.
 Kutoka kulia ni Semu Kalekezi, mtaalamu wa maabara (katikati) ni Innocent Mogha mkaguzi wa zao la Pareto, na wakwanza kushoto ni Tumaini Ngajilo mtakwimu wa bodi ya pareto, wakiwa katika shamba la Pareto.
 Semu Kalekezi, mtaalamu wa maabara.
 Innocent Mogha mkaguzi wa zao la Pareto.
 Tumaini Ngajilo mtakwimu wa bodi ya pareto.
 Pareto ikiwa shambani


Bango likionyesha hatua za shughuli za kilimo cha zao la Pareto, kuanzia shambani hadi kusafirisha kwenda nyumbani na namna ya kuanika.

HABARI.


TANZANIA imeng’ara katika soko la dunia kupitia zao la Pareto, zao ambalo baadhi ya wakulima wameligeuzia kisogo, licha ya zao hilo kuwa na mauzo mazuri kwa kilo, ukilinganisha na mazao mengine ambayo yamezoeleka.

Hayo yamezungumzwa na Ephraem Reuben Mhekwa, ambaye amesema kwa sasa Tanzania ipo juu kwa kuuza zao hilo la Pareto kwa kiwango kikubwa katika soko la dunia, huku bei ya kilo moja ya Pareto ikipaa kulingana na kiwango cha sumu kilichopo katika maua ya zao hilo.

 Mhekwa amesema Tanzania imefanikiwa kukusanya tani elfu 6700 za zao la Pareto, na kuwa miongoni mwa nchi chache zinazofanya vizuri kwa kulima zao hilo, huku ikiipita nchi ya Kenya ambayo awali ilikuwa ni bora zaidi, huku kilo moja ikifikia zaidi ya shilingi 1500 hadi 2500.

Amesema Kenya awali ilikuwa inaongoza kulima zao hilo na sasa wamefikia tani 2000  pekee huku Tanzania ikifikia tani elfu 6700 na mahitaji ya dunia yakiwa ni tani elfu 20 za Pareto kwa mwaka, huku Pareto iliyopatikana ni tani elfu 13200.

Amesema zao la Pareto kwa takwimu za kuanzia june 30 liliingiza zaidi ya dola milioni 10 hadi 15, na kuwa asilimia 90 ya soko la Pareto lipo nchini Marekani na sasa Mmarekani huyo amenunua kiwanda cha Mafinga.

Amewasihi wakulima kuchangamkia fulsa hiyo, kwa kulima zao hilo kwa wingi, licha ya kukabiliwa na changamoto katika uendeshaji wa kilimo cha zao hilo la Pareto, hasa katika  upatikanaji wa Pembejeo na vikaushio.

Mhekwa ameitaja Mikoa inayolima zao la Pareto kwa Wingi Tanzania  kuwa ni Mbeya, Njombe, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, na mkoa wa Iringa, huku mkoa wa Rukwa, Moro, Ruvuma, Kagera na  mkoa wa Tanga kwa sehemu ya Rushoto, ikiwa imefanyiwa utafiti amb ao umeonyesha uwezo wa kulima zao hilo.

Mhekwa amesema Changamoto kubwa kwa upande wa wakulima ambo ndiyo wazazilishaji wa zao hilo  ni upatikanaji wa pembejeo hasa mbegu, vitendea kazi vya kukaushia Pareto, kwani zao hili hulimwa katika maeneo yenye baridi,  na hivyo hatua ya ukaushaji ukitakiwa kuwa niwa umakini zaidi.

Aidha amesema Sekta ya Pareto imeanzisha mfuko wa kuendeleza zao la Pareto, mfuko unaochangiwa na wakulima, wafanyabiashara, Halmashauri na serikali kuu na lengo kuu la mpango wa mfuko huo ni kugharamia utafiti, nyenzo za kufanyia kazi kama vikausha nk ili kuwawezesha kupata Pareto bora zaidi.

Aidha  katika mkutano huo mkuu, mfuko wa kuendeleza kilimo cha zao la Pareto, umeadhimia  kupandisha kiwango cha bei ambacho kitajikita katika ubora, huku azimio likiwa ni  wakulima watakaozalisha  Pareto nzuri watalipwa bei nzuri na watakaozalisha  Pareto mbaya, wataadhibiwa kwa ubaya wa Pareto yao.

Amesema hatua hiyo imelenga pia kuongeza hamasa ya kuitunza vizuri Pareto tangu ikiwa shambani mpaka inapofikia hatua ya kuuzwa, ambapo makubaliano yaliafikiwa kuwa kilo moja ya Pareto yenye ubora wa 0.9 italipwa   kiasi cha shilingi 1500 na Pareto yenye ubora wa 1.8 na kuendelea italipwa kiasi cha shilingi 2500 kwa kilo moja.

Amesema matumizi ya kuzalisha zao la Pareto ni kupata Sumu inayopatikana katika maua ya Pareto,  sumu ambayo hutumika kuulia wadudu waharibifu wa shambani na nyumbani na katika mazingira yanayozunguka nyumba, huku sumu hiyo ikidaiwa kutokuwa na madhara yoyote kwa afya ya binadamu yeyote.

Amesema changamoto inayowakabiri wanunuzi ni uwezo mdogo wa kumiliki vifaa vya kukamulia/ kuzindulia Pareto, kwani sheria inawataka wanunuzi kuwa na mitambo ya kuengua sumu kwa kuwa mitambo hiyo inapatikana kwa gharama ya zaidi ya dola milioni 1 na hali hiyo imesababisha kuwepo kwa mnunuzi mmoja pekee aliyekidhi vigezo hivyo, mnunuzi ambaye anapatikana Mafinga – Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Pia amesema changamoto nyingine inayowakabiri wanunuzi ni ufinyu wa soko  la Pareto kwa kuwa soko kubwa linalotegemewa ni nchi ya Marekani, Ulaya, huku wafanyabiashara wadogo soko lao kubwa likipatikana katika nchi ya Ruanda, Kenya na China.

Kwa upande wa bodi amesema changamoto kubwa inayowakabiri ni uhaba wa fedha na vitendea kazi kutotoshereza shughuli za utafiti, kwakuwa Fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kufanyia utafiti hazitosherezi, na hiyo ni kutokana na zao hilo kuhitaji utafiri wa mara kwa mara.

“Sisi kama bodi tunashirikiana na mfuko wa kuendeleza zao la Pareto, ambapo fedha asilimia 30 zilizopatikana kutokana na michango huwasaidia  wakulima kupatikana kwa mbegu na kugharamia utafiti.

Amesema tangu zao hilo liingie hapa nchini mwaka 1930 mpaka sasa kuna aina chache tu za Pareto kwa ajili ya kufanya utafiti ili kupata ubora wa sumu inayokubarika katika zao hilo.

Amesema matumizi ya Sumu ya Pareto ni kuulia wadudu kama Nzi, Mbu na  mazalia yake, na  mabaki yake au machicha hutumika kwa ajili  ya chakula cha mifugo, huku sumu  chache iliyopo katika mabaki au mashudu hayo husaidia  kuua minyoo na wadudu waliopo katika tumbo la  mnyama/mfugo.

Na kuwa mafuta yanayofahamika kama “Pay Gris” hutumika kupambana na wadudu  wanawashambulia mifugo, kama Ng’ombe, Mbuzi, Nguruwe, paka, wadudu kama Kupe, Viroboto nk.


“Kwa bahati mbaya sana Kiwanda kimejengwa katika eneo ambalo uzalishaji wa Pareto ni hasi, sio mkubwa sana, na kiwanda hicho kimejengwa tangu mwaka 1980 Mafinga katika Wilaya ya Mufindi, wakitarajia wakulima watachangamkia kulima Pareto, lakini kwa bahati mbaya wananchi wa Wilaya ya Mufindi hawana mwamko wa kulima zao hili la Pareto, na hii ni kutokana na wakulima kuwa na mazao mengine mbadala, kama zao la Chai na zao la Miti,” Amesema Mhekwa.

Hata hivyo Mhekwa ametoa wito kwa wakulima kuendesha kilimo kwa kuendana na ubora ili kulifanya zao kuwa na tija kwao kwa kuwaletea maendeleo na kulitangaza Taifa la Tanzania.
MWISHO


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni