Ijumaa, 15 Agosti 2014

PARETO YAIWAKIRISHA TANZANIA KWA KUINGIZA MABILIONI.


 Zao la Pareto likiwa  Shambani.
 Ramani ya Tanzania ikionyesha mikoa ambayo inalima zao la Pareto
 Kushoto ni Ephraem Mhekwa Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Pareto akiwa na  Gerlad Chuwa (Kulia) ambaye ni mdhibiti wa zao la Pareto nyanda za juu kusini.
 Ephraem Mhekwa Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Pareto akiwa na  Gerlad Chuwa (mwenye miwaniKulia) ambaye ni mdhibiti wa zao la Pareto nyanda za juu kusini.
 Semu Kalekezi mtaalamu wa maabara ya Pareto akiwa na Tumaini Ngajilo (Mwenye kofia) Mtakwimu bodi ya Pareto akitoa maelezo juu ya bidhaa zitokanazo na zao la Pareto.

 Semu Kalekezi mtaalamu wa maabara ya Pareto.
 Shamba la Pareto.
 Kutoka kulia ni Semu Kalekezi, mtaalamu wa maabara (katikati) ni Innocent Mogha na wakwanza kushoto ni Tumaini Ngajilo mtakwimu wa bodi ya pareto, wakiwa katika shamba la Pareto.
 Kutoka kulia ni Semu Kalekezi, mtaalamu wa maabara (katikati) ni Innocent Mogha mkaguzi wa zao la Pareto, na wakwanza kushoto ni Tumaini Ngajilo mtakwimu wa bodi ya pareto, wakiwa katika shamba la Pareto.
 Semu Kalekezi, mtaalamu wa maabara.
 Innocent Mogha mkaguzi wa zao la Pareto.
 Tumaini Ngajilo mtakwimu wa bodi ya pareto.
 Pareto ikiwa shambani


Bango likionyesha hatua za shughuli za kilimo cha zao la Pareto, kuanzia shambani hadi kusafirisha kwenda nyumbani na namna ya kuanika.

HABARI.


TANZANIA imeng’ara katika soko la dunia kupitia zao la Pareto, zao ambalo baadhi ya wakulima wameligeuzia kisogo, licha ya zao hilo kuwa na mauzo mazuri kwa kilo, ukilinganisha na mazao mengine ambayo yamezoeleka.

Hayo yamezungumzwa na Ephraem Reuben Mhekwa, ambaye amesema kwa sasa Tanzania ipo juu kwa kuuza zao hilo la Pareto kwa kiwango kikubwa katika soko la dunia, huku bei ya kilo moja ya Pareto ikipaa kulingana na kiwango cha sumu kilichopo katika maua ya zao hilo.

 Mhekwa amesema Tanzania imefanikiwa kukusanya tani elfu 6700 za zao la Pareto, na kuwa miongoni mwa nchi chache zinazofanya vizuri kwa kulima zao hilo, huku ikiipita nchi ya Kenya ambayo awali ilikuwa ni bora zaidi, huku kilo moja ikifikia zaidi ya shilingi 1500 hadi 2500.

Amesema Kenya awali ilikuwa inaongoza kulima zao hilo na sasa wamefikia tani 2000  pekee huku Tanzania ikifikia tani elfu 6700 na mahitaji ya dunia yakiwa ni tani elfu 20 za Pareto kwa mwaka, huku Pareto iliyopatikana ni tani elfu 13200.

Amesema zao la Pareto kwa takwimu za kuanzia june 30 liliingiza zaidi ya dola milioni 10 hadi 15, na kuwa asilimia 90 ya soko la Pareto lipo nchini Marekani na sasa Mmarekani huyo amenunua kiwanda cha Mafinga.

Amewasihi wakulima kuchangamkia fulsa hiyo, kwa kulima zao hilo kwa wingi, licha ya kukabiliwa na changamoto katika uendeshaji wa kilimo cha zao hilo la Pareto, hasa katika  upatikanaji wa Pembejeo na vikaushio.

Mhekwa ameitaja Mikoa inayolima zao la Pareto kwa Wingi Tanzania  kuwa ni Mbeya, Njombe, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, na mkoa wa Iringa, huku mkoa wa Rukwa, Moro, Ruvuma, Kagera na  mkoa wa Tanga kwa sehemu ya Rushoto, ikiwa imefanyiwa utafiti amb ao umeonyesha uwezo wa kulima zao hilo.

Mhekwa amesema Changamoto kubwa kwa upande wa wakulima ambo ndiyo wazazilishaji wa zao hilo  ni upatikanaji wa pembejeo hasa mbegu, vitendea kazi vya kukaushia Pareto, kwani zao hili hulimwa katika maeneo yenye baridi,  na hivyo hatua ya ukaushaji ukitakiwa kuwa niwa umakini zaidi.

Aidha amesema Sekta ya Pareto imeanzisha mfuko wa kuendeleza zao la Pareto, mfuko unaochangiwa na wakulima, wafanyabiashara, Halmashauri na serikali kuu na lengo kuu la mpango wa mfuko huo ni kugharamia utafiti, nyenzo za kufanyia kazi kama vikausha nk ili kuwawezesha kupata Pareto bora zaidi.

Aidha  katika mkutano huo mkuu, mfuko wa kuendeleza kilimo cha zao la Pareto, umeadhimia  kupandisha kiwango cha bei ambacho kitajikita katika ubora, huku azimio likiwa ni  wakulima watakaozalisha  Pareto nzuri watalipwa bei nzuri na watakaozalisha  Pareto mbaya, wataadhibiwa kwa ubaya wa Pareto yao.

Amesema hatua hiyo imelenga pia kuongeza hamasa ya kuitunza vizuri Pareto tangu ikiwa shambani mpaka inapofikia hatua ya kuuzwa, ambapo makubaliano yaliafikiwa kuwa kilo moja ya Pareto yenye ubora wa 0.9 italipwa   kiasi cha shilingi 1500 na Pareto yenye ubora wa 1.8 na kuendelea italipwa kiasi cha shilingi 2500 kwa kilo moja.

Amesema matumizi ya kuzalisha zao la Pareto ni kupata Sumu inayopatikana katika maua ya Pareto,  sumu ambayo hutumika kuulia wadudu waharibifu wa shambani na nyumbani na katika mazingira yanayozunguka nyumba, huku sumu hiyo ikidaiwa kutokuwa na madhara yoyote kwa afya ya binadamu yeyote.

Amesema changamoto inayowakabiri wanunuzi ni uwezo mdogo wa kumiliki vifaa vya kukamulia/ kuzindulia Pareto, kwani sheria inawataka wanunuzi kuwa na mitambo ya kuengua sumu kwa kuwa mitambo hiyo inapatikana kwa gharama ya zaidi ya dola milioni 1 na hali hiyo imesababisha kuwepo kwa mnunuzi mmoja pekee aliyekidhi vigezo hivyo, mnunuzi ambaye anapatikana Mafinga – Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Pia amesema changamoto nyingine inayowakabiri wanunuzi ni ufinyu wa soko  la Pareto kwa kuwa soko kubwa linalotegemewa ni nchi ya Marekani, Ulaya, huku wafanyabiashara wadogo soko lao kubwa likipatikana katika nchi ya Ruanda, Kenya na China.

Kwa upande wa bodi amesema changamoto kubwa inayowakabiri ni uhaba wa fedha na vitendea kazi kutotoshereza shughuli za utafiti, kwakuwa Fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kufanyia utafiti hazitosherezi, na hiyo ni kutokana na zao hilo kuhitaji utafiri wa mara kwa mara.

“Sisi kama bodi tunashirikiana na mfuko wa kuendeleza zao la Pareto, ambapo fedha asilimia 30 zilizopatikana kutokana na michango huwasaidia  wakulima kupatikana kwa mbegu na kugharamia utafiti.

Amesema tangu zao hilo liingie hapa nchini mwaka 1930 mpaka sasa kuna aina chache tu za Pareto kwa ajili ya kufanya utafiti ili kupata ubora wa sumu inayokubarika katika zao hilo.

Amesema matumizi ya Sumu ya Pareto ni kuulia wadudu kama Nzi, Mbu na  mazalia yake, na  mabaki yake au machicha hutumika kwa ajili  ya chakula cha mifugo, huku sumu  chache iliyopo katika mabaki au mashudu hayo husaidia  kuua minyoo na wadudu waliopo katika tumbo la  mnyama/mfugo.

Na kuwa mafuta yanayofahamika kama “Pay Gris” hutumika kupambana na wadudu  wanawashambulia mifugo, kama Ng’ombe, Mbuzi, Nguruwe, paka, wadudu kama Kupe, Viroboto nk.


“Kwa bahati mbaya sana Kiwanda kimejengwa katika eneo ambalo uzalishaji wa Pareto ni hasi, sio mkubwa sana, na kiwanda hicho kimejengwa tangu mwaka 1980 Mafinga katika Wilaya ya Mufindi, wakitarajia wakulima watachangamkia kulima Pareto, lakini kwa bahati mbaya wananchi wa Wilaya ya Mufindi hawana mwamko wa kulima zao hili la Pareto, na hii ni kutokana na wakulima kuwa na mazao mengine mbadala, kama zao la Chai na zao la Miti,” Amesema Mhekwa.

Hata hivyo Mhekwa ametoa wito kwa wakulima kuendesha kilimo kwa kuendana na ubora ili kulifanya zao kuwa na tija kwao kwa kuwaletea maendeleo na kulitangaza Taifa la Tanzania.
MWISHO


Ijumaa, 8 Agosti 2014

WILAYA YA IRINGA YAIBUKA KUWA BORA NYANDA ZA KUSINI.



 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Steven Mhapa akizungumza jambo mara baada hya kupokea Kombe la ushindi wa kuwa Wilaya bora nyanda za kusini.
 Diwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Ritha Mlagala akizungumza jambo mara baada hya kupokea Kombe la ushindi wa kuwa Wilaya bora nyanda za kusini.
 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Steven Mhapa.
 
 Diwani wa Kata ya Izazi Wilaya ya Iringa akifurahia kupata ushindi huo wa Halmashauri yake kuwa bora kwa mkpoa wa Iringa na Halmashauri zlote za mikoa ya Kanda ya kusini.
 Madiwani wakifurahia ushindi huo.
 Diwani Shakira Kiwanga wa Kata ya Kalenga akifurahia kupata ushindi huo.








<<<HABARI>>>

HALMASHAURI ya Wilaya ya Iringa imefanikiwa kuwa Wilaya bora, kati ya Wilaya za mikoa ya kusini kwa shughuli mbalimbali za kilimo, ujasiliamali na ufugaji.

Sifa ya Wilaya hiyo imetolewa katika maonyesho ya 22 ya sherehe za wakulima nanenane, ambazo kanda ya kusini hufanyika katika uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya.

Mbele ya viongozi, watumishi na wananchi mbalimbali wakiwemo wakulima, Wilaya ya Iringa imepewa kombe la ushindi wa kwanza Kimkoa na kikanda kwa kuwa na sifa bora na zinazokidhi vigezo katika mpangilio wa kazi zake za kilimo.

Akitanabaisha namna Halmashauri yake ilivyofanikiwa kushika nafasi hiyo ya kwanza, mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Steven Mhapa amesema siri kuu ni ushirikiano baina ya wao madiwani, watumishi wa halkmashauri yake pamoja na wananchi kwa ujumla.

Aidha Mhapa amesema pia walijipanga vyema katika kuonyesha shughuli halisi ziunazofanywa katika Halmashauri yake, kikiwemo kilimo, ufugaji na masuala ya utalii ambayo ni kielelezo cha mkoa wa UIringa ambo ni kitovu cha utalii mikoa ya nyanda za juu kusini.

Akitoa wito- Mhapa ameutaka uongozi wa uwanja huo kuhakikisha unaboresha miundombinu ya barabara, kwa kuweka Lami katika barabara zake zote zilizopo katika uwanja huo.

Mhapa amesema changamoto kubwa zilizopo katika uwanja huo, hazivumiliki,  hasa uhaba mkubwa wa vyoo ambavyo haviendana na takwimu ya wananchi wanaoingia katika uwanja huo.

“Uwanja huu unakabiliwa na changamoto mbalimbali, mfano hali hii ya vumbi ni hatari sana, tunataka barabara zote za ndani ya uwanja huu ziwekwe lami, lakini suala la vyoo nalo ni tatizo kubwa sana, mfano hapa tulipo kwenye eneo la hii la jukwaa kuna choo kimoja tu, hii ni hatari sana,” alisema Mhapa.

Naye Ritha Mlagala mmoja wa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, amesema kukosekana kwa huduma ya vyoo vya kutosha katika uwanja huo, ni ni adha kwa wananchi wanaoingia katika uwanja huo wa nanenane.

Maonyesho ya nanenane yamefungwa rasmi na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabiti  Mwambungu, akiwemo Abbas Kandolo mkuu wa mkoa wa Mbeya, na maonyesho hayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya viwanja vya Ngongo  mkoani Lindi, na kufungwa rasmi na makamu wa rais Mohamed Bilal.

MWISHO.

Jumatano, 6 Agosti 2014

VETA KUVIFUNGIA VYUO


Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha utalii Ruaha cha Iringa wakiwa nje ya jengo la chuo chao, mara baada ya chuo hicho kuzindiliwa rasmi na mamlaka ya vyuo vya ufundi stadi Tanzania - VETA.
Mwenyekiti wa bodi ya VETA Kabaka Ndenda-  wa pili kushoto mara baada ya kuzindua chuo cha Utalii cha Ruaha- Iringa, akiwa na baadhi ya viongozi wa VETA mkoa wa Iringa, wa kwanza kulia ni mkurugenzi wa Chuo cha utalii Ruaha  Yohanes Nicorous Sanga.
 Mkurugenzi wa Chuo cha utalii Ruaha  Yohanes Nicorous  Sanga, akizungumza jambo mara baada ya chuo chake kuzinduliwa rasmi.
 Kabaka Ndenda-  mara baada ya kuzindua chuo cha Utalii cha Ruaha- Iringa, akisikiliza jambo kwa umakini, kutoka kwa  mkurugenzi wa Chuo cha utalii Ruaha  Yohanes Sanga (pichani hayupo).
 Mmoja wa viongozi wakuu wa VETA nyanda za kusini, akiwa katika siku ya uzinduzi wa chuo cha Utalii Ruaha- kilichopo Iringa.
 Suzan Magani kaimu mkurugenzi wa VETA kanda ya nyanda za kusini, akiwa katika siku ya uzinduzi wa chuo cha utalii Ruaha.

 Mkurugenzi wa Chuo cha utalii Ruaha  Yohanes Nicorous Sanga, akishukuru baada ya chuo chake kuzinduliwa.
                               Bango la uzinduzi
 Bango la uzinduzi wa jengo la kulala wanafunzi- wa chuo cha utalii Ruaha.
       Jengo la chuo cha Utalii cha Ruaha- Iringa.
 Chuo cha utalii cha Ruaha, kikiwa tayari kimezinduliwa rasmi.
                   Chuo cha utalii Ruaha- Iringa.
 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha utalii Ruaha wakiwa nje ya jengo lao.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha utalii Ruaha wakifurahia jambo baada ya chuo chao kuzinduliwa rasmi.
 Baadhi ya Wanafunzi wa chuo cha utalii Ruaha Iringa wakiwa nje ya kati ya jengo la chuo chao.



<<<HABARI>>> 

MAMLAKA ya vyuo vya ufundi Stadi VETA imesema itahakikisha inavifungia vyuo vyote vinavyokiuka sheria na taratibu, kwa kutokuwa na sifa ya utoaji wa elimu hiyo, kwa madai kuwa vinachangia wahitimu wake kukosa fulsa ya ajira.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa bodi ya vyuo vya Ufundi stadi VETA Kabaka Ndenda wakati akizindua chuo cha Utalii cha Ruaha kilichopo Kalenga Wilaya ya Iringa, chuo ambacho kitasaidia katika utoaji wa elimu ya sekta ya utalii na kuutangaza mkoa wa Iringa.

Ndenda amesema mpango huo umelenga kuokoa muda wanaopoteza wanafunzi kusoma katika vyuo hivyo visivyo na sifa, kwa madai kuwa vinapoteza fedha za wazazi / walezi wa wanafunzi, jambo ambalo linachangia ongezeko la vijana wasio na ajira.

Aidha ndenda amesema katika kukabiliana na hali hiyo pia watawadhibiti wamiliki wa Hotel, Motel na “Lodge” nyumba za kulala wageni ambao wanatoa ajira kwa wafanyakazi wasio na elimu ya huduma ya hotel.

Ndenda amesema waajiri wengi wamekuwa wakikimbilia kuajiri wafanyakazi wasio na sifa, ili kulipa mishahara duni isiyoendana na viwango vinavyotakiwa na serikali, na kuwa hata hivyo waajiri hao wanajimaliza wenyewe kwa kuwakabidhi kazi watu wasio na taaluma.

Naye mkurugenzi wa chuo cha utalii cha Ruaha -Yohanes Sanga amesema mpango huo utasaidia jamii kuwa na elimu bora, kwa kuwa sasa kuna ushindani usio na tija, ambapo baadhi ya walezi na wazzi wasio na uelewa juu ya usajili wa vyuo hujikuta wakiwapeleka watoto wao katika vyo hivyo na hivyo kupata hasara ya fedha na muda.

Sanga amesema kuna umuhimu jamii ikazingatia masuala ya elimu bora ya utalii, na kuachana na kasumba ya kukimbilia unafuu wa ada, kwa kuwa jambo hilo ndilo linalowafanya wahitimu kukosa ajira, baada ya vyuo vyao kutotambulika kisheria.

Sanga amesema kumekuwa na ushindani mkubwa wa uendeshaji wa vyuo, hasa hivyo visivyo na sifa, na kuitaka jamii kuwa makini kwa kufanya uchunguzi ili kutambua mapema- mapungufu ya vyuo kabla ya kujiunga navyo.

“Ningeiomba jamii isikimbilie unafuu wa ada, kuna vitu vya msingi vya kuzingatia hasa usajili, utoaji wa elimu bora, lakini pia hata mazingira nayo yanatakiwa kuwa mazuri na yenye muonekano unaovutia kwa wanafunzi -yawe rafiki kwa utoaji na upokeaji wa elimu,” Alisema Sanga.

Sanga amesema kuanzishwa kwa chuo hicho cha Utalii Ruaha ni mwarobaini wa kuinua hali ya utalii mikoa ya nyanda za juu kusini, na hasa mkoa wa Iringa ambao umepewa dhamana ya kuwa kitovu cha utalii mikoa ya kusini.

Aisha Sharif mwanafunzi wa chuo cha utalii Ruaha amesema changamoto kubwa inayowakabili pindi wanapojiunga na vyuo visivyo na sifa ni kupoteza muda wao walioutumia kusoma, na pia kupoteza fedha za wazazi wao.

Naye Radhia Abdullah ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo hicho cha utalii Ruaha amitaka serikali kuvifungia haraka iwezekanavyo vyuo vyote visivyokidhi sifa na vigezo vya kutoa elimu, kwa kuwa vinaifanya taaluma hiyo ya Hoteli na utawala kutothaminiwa katika jamii.

Mwanafunzi Furahini Msigwa, ameiomba serikali kuvisajiri haraka vyuo vyote vinavyokuwa na sifa, ili kutoa fulsa ya wanafunzi wengi kipata elimu hiyo, kwa kuwa baadhi ya vijana wamekuwa wakipoteza dira ya maisha yao kwa kukosa nafasi ya kujiunga na vyuo hivyo vya ufundi.

Wanafunzi hao wamesema kukamilika kwa chuo hicho, ikiwa pamoja na kuwa na vigezo ni majibu tosha kwa kundi lao vijana ambao kilio chao kikubwa ni juu ya upatikanaji wa ajira, kwa madai kuwa sasa watapata elimu ya utalii na hivyo kuwawezesha kupata ajira na kuondokana na utegemezi.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo wa bodi ya VETA -mikoa ya kusini ina jumla ya vyuo vya ufundi stadi 69 pekee, huku vinavyomilikiwa na mamlaka ya ufundi  stadi yaani VETA vikiwa ni vyuo vitatu tu, 66 vikiwa nivya watu binafsi na taasisi mbalimbali.

Hata hivyo hali hiyo ya ndiyo inayotoa mwanya wa uvunjaji wa sheria na kusababisha baadhi ya wanafunzi kuangukia katika vyuo visivyosajiliwa na hivyo kujikuta wakikosa ajira- kwa kuwa vyuo vyao havitambuliki.
 MWISHO.