Ijumaa, 8 Agosti 2014

WILAYA YA IRINGA YAIBUKA KUWA BORA NYANDA ZA KUSINI.



 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Steven Mhapa akizungumza jambo mara baada hya kupokea Kombe la ushindi wa kuwa Wilaya bora nyanda za kusini.
 Diwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Ritha Mlagala akizungumza jambo mara baada hya kupokea Kombe la ushindi wa kuwa Wilaya bora nyanda za kusini.
 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Steven Mhapa.
 
 Diwani wa Kata ya Izazi Wilaya ya Iringa akifurahia kupata ushindi huo wa Halmashauri yake kuwa bora kwa mkpoa wa Iringa na Halmashauri zlote za mikoa ya Kanda ya kusini.
 Madiwani wakifurahia ushindi huo.
 Diwani Shakira Kiwanga wa Kata ya Kalenga akifurahia kupata ushindi huo.








<<<HABARI>>>

HALMASHAURI ya Wilaya ya Iringa imefanikiwa kuwa Wilaya bora, kati ya Wilaya za mikoa ya kusini kwa shughuli mbalimbali za kilimo, ujasiliamali na ufugaji.

Sifa ya Wilaya hiyo imetolewa katika maonyesho ya 22 ya sherehe za wakulima nanenane, ambazo kanda ya kusini hufanyika katika uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya.

Mbele ya viongozi, watumishi na wananchi mbalimbali wakiwemo wakulima, Wilaya ya Iringa imepewa kombe la ushindi wa kwanza Kimkoa na kikanda kwa kuwa na sifa bora na zinazokidhi vigezo katika mpangilio wa kazi zake za kilimo.

Akitanabaisha namna Halmashauri yake ilivyofanikiwa kushika nafasi hiyo ya kwanza, mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Steven Mhapa amesema siri kuu ni ushirikiano baina ya wao madiwani, watumishi wa halkmashauri yake pamoja na wananchi kwa ujumla.

Aidha Mhapa amesema pia walijipanga vyema katika kuonyesha shughuli halisi ziunazofanywa katika Halmashauri yake, kikiwemo kilimo, ufugaji na masuala ya utalii ambayo ni kielelezo cha mkoa wa UIringa ambo ni kitovu cha utalii mikoa ya nyanda za juu kusini.

Akitoa wito- Mhapa ameutaka uongozi wa uwanja huo kuhakikisha unaboresha miundombinu ya barabara, kwa kuweka Lami katika barabara zake zote zilizopo katika uwanja huo.

Mhapa amesema changamoto kubwa zilizopo katika uwanja huo, hazivumiliki,  hasa uhaba mkubwa wa vyoo ambavyo haviendana na takwimu ya wananchi wanaoingia katika uwanja huo.

“Uwanja huu unakabiliwa na changamoto mbalimbali, mfano hali hii ya vumbi ni hatari sana, tunataka barabara zote za ndani ya uwanja huu ziwekwe lami, lakini suala la vyoo nalo ni tatizo kubwa sana, mfano hapa tulipo kwenye eneo la hii la jukwaa kuna choo kimoja tu, hii ni hatari sana,” alisema Mhapa.

Naye Ritha Mlagala mmoja wa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, amesema kukosekana kwa huduma ya vyoo vya kutosha katika uwanja huo, ni ni adha kwa wananchi wanaoingia katika uwanja huo wa nanenane.

Maonyesho ya nanenane yamefungwa rasmi na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabiti  Mwambungu, akiwemo Abbas Kandolo mkuu wa mkoa wa Mbeya, na maonyesho hayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya viwanja vya Ngongo  mkoani Lindi, na kufungwa rasmi na makamu wa rais Mohamed Bilal.

MWISHO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni