Jumatano, 11 Machi 2015

MTOTO MDOGO ANUSURIKA KATIKA AJALI ILIYOUA 43

 Mtoto ambaye amempoteza mama yake katika ajali ya basi la Mjinja iliyotokea Changalawe katika mji wa Mafinga Wilayani Mufindi katika Mkoa wa Iringa - ajali iyopoteza uhai wa watu 43- akiwa na mmoja wa wasamalia wema katika Hospitali ya Mafinga.
Mwanahabari Fahady Mgunda akiwa na mtoto ambaye hakujulikana jina lake.. ambaye amenusurika katika ajali ya basi la Majinja basi lililosababisha vifo vya watu 43 na majeruhi 22, mtoto huyu alitoka mzima akiwa hana hata mchubuko- licha waliokufa kudaiwa kuwa katika siti za mbele akiwemo mama mzazi wa mtoto huyo.



 Roli lililoangukia basi katika eneo la Changalawe- mjini Mafinga katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa- ajali iliyopoteza uhai wa watu 43, wakati basi hilo likitokea jijini Mbeya kuelekea jijini Dar es salaam.

<<<HABARI>>>

MTOTO mwenye umri unaokadiliwa kuwa niwa zaidi ya mwaka mmoja amenusurika kifo katika ajali iliyoua zaidi ya watu 40, iliyotokea katika bonde la eneo la Changalawe, njia kuu ya Iringa Mbeya. 

Mtoto huyo ambaye hajafahamika jina lake kamili, alikuwa na mama yake ambaye amepoteza maisha katika ajali hiyo, na hivyo kuwa chini ya uangalizi wa wauguzi wa Hospitali ya Mafinga- Wilayani Mufindi- katika mkoa wa Iringa.

 Kunusurika kwa mtoto huyo limekuwa ni jambo la kushangaza kutokana na ajali hiyo kusababisha vifo vya abiria wote waliokuwa wamekaa viti vya mbele vya basi la Majinja lenye namba za usajili T 438 CDE Scania- akiwemo mama wa mtoto huyo aliyekuwa mmoja kati ya abiria waliokaa viti hivyo vya mbele.

 Aidha uongozi wa Hospitali ya Mafinga umeweza kufanya mawasiliano na baba wa mtoto huyo, ambapo kwa mujibu wa mmoja wa wauguzi mpaka majira ya saa kumi - baba wa mtoto alikuwa njiani akitokea jijini Mbeya kwenda Mafinga kwa ajili ya taratibu za kuchukua mwili wa mke wake pamoja na mtoto huyo.

 Ajali ya bus la Majinja – linalofanya safari za Mbeya ..Dar es salaam limegongana uso kwa uso na Lori la mizigo, ajali ambayo pia imesababisha majeruhi 22, wanawake wakiwa 6, wanaume 33 na watoto3 . 

 Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mafinga Dr. Boazi Peter Mnenegwa amesema kati ya majeruhi 27 aliowapokea hospitalini hapo - watano wamefariki. 

 Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema ajali hiyo imetokana na magari hayo kugongana uso kwa uso wakati wakikwepa shimo lililokuwa barabarani. 

 Naye Amina Masenza mkuu wa mkoa wa Iringa amesema ajali hiyo ni mbaya kutokea mkoani Iringa na kuwa huo ni msiba wa watanzania wote. Elias Mwakapalala na – Samson Obeid wakazi wa jiji la Mbeya –ni miongoni mwa wamajeruhi walionusulika katika ajali hiyo ya basi la Majinja, ambao wamelazwa katika hospitali ya Mafinga, wamesema sababu za ajali hiyo ni mwendokasi na uwepo wa idadi kubwa ya Abiria.

Asilimia kubwa ya abiria wakiokuwa wakisafiri na basi hilo la Majinja inasadikika kuwa wengi wao walikuwa ni wanafunzi walikuwa wamepandia katika kituo cha mabasi cha Uyole jijini Mbeya – na sababu za idadi kubwa ya vifo- ni kutokana na Kontena la roli kuwafunika abiria waliokuwa kwenye busi hilo.

Hata hivyo idadi ya waliofariki katika ajali hiyo imeongezeka baada ya mmoja wa majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa  kufariki na hivyo kuwepo kwa vifo 43 kutoka 42 vilivyotajwa awali.
MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni