Alhamisi, 13 Februari 2014

MWANAHABARI AKAMATWA KATIKA KESI YA MAUAJI YA MWANGOSI


Jopo la wanahabari mkoani Iringa wakiwa katika viwanja vya Mahakama ya Rufaa mkoa wa Iringa, huku mwanahabari Frenk Leonard aliyevaa shati la draft na Suruali ya  kaki, kabla ya kupatwa na mkasa huo.

<<<<HABARI>>>>>

KATIKA hali isiyo ya kawaida, mwandishi wa habari wa gazeti la Habarileo, na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Iringa Frank Leonard amekamatwa na askari Polisi wanne waliokuwa wamevaa kiraia kwa madai ya kupiga picha mahakamani.


Tukio hilo limetokea leo asubuhi wakati jopo la wanahabari likiwa limefika mahakamani hapo ili kufahamu mwenendo mzima wa kesi ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten marehemu Daud Mwangosi, ambapo mshtakiwa wa mauaji hayo alifikishwa katika mahakama hiyo.


Baada ya kukamatwa mwanahabari huyo Frenk, alifikishwa katika kituo cha Polisi cha Kati mjini Iringa, na akizungumza na wanahabari baada ya kuachiwa huru, Leonard amesema hali hiyo inaonyesha kuwa bado wapo baadhi ya askari kwa makusudi wanataka kubomoa mahusiano yaliyopo baina ya wanahabari na jeshi la Polisi ambayo yanaendelea kujengwa na kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi.


Aidha Leonard amesema  kitendo cha kubambikiziwa tuhuma ndani ya muhimili wa dola unaojitegemea (mahakama) ni kitendo cha uzalilishaji kinachotaka kuaminisha umma kwamba wanahabari ni watu wasiotaka kufuata taratibu za kimahakama, ambapo mwanahabari huyo alikamatwa na askari akiwa ndani ya chumba cha mahakama pasipo idhini ya Jaji wa Mahakama Kuu.


Msajili wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Iringa, Dunstan Nduguru amesema ameshangazwa na Polisi kwa kuingia shughuli za mahakama kwa madai kumkamata mwandishi huyo kama alikuwa na kosa lilikuwa ni jukumu la Mahakama na polisi walipaswa kupewa agizo na Jaji Mfawidhi aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo, ambapo Leonard ameachiwa huru katika kituo hicho baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kile kilichodaiwa kuwa mwanahabari huyo alivunja taratibu na sheria za kimahakama.


Baada ya kukamatwa Leonard, alifikishwa kituo cha Polisi cha Kati mjini Iringa na kuachiwa huru baada ya kukosekana ushahidi,na akizungumza na wanahabari baada ya kuachiwa huru, Leonard alisema "wapo baadhi ya askari kwa makusudi wanataka kubomoa mahusiano baina ya wanahabari na jeshi la Polisi ambayo yanaendelea kujengwa na kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi."


Alisema kitendo cha kubambikiziwa tuhuma ndani ya muhimili wa dola unaojitegemea (mahakama) ni kitendo cha uzalilishaji kinachotaka kuaminisha umma kwamba wanahabari ni watu wasiotaka kufuata taratibu za kimahakama.


Alisema akiwa ndani ya chumba cha mahakama hiyo alikamatwa na askari hao bila idhini ya Jaji wa Mahakama Kuu wakati akizima simu yake ya mkononi iliyokuwa katika mtetemo.



"Nilikuwa nazima simu yangu hao askari hao kwasababu wanazojua wao wenyewe waligeuza suala hilo ili lionekane katika sura wanayoitaka na hatimaye wanifungulie mashtaka," alisema.


Alimshukuru Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Iringa, Ngoi kwa kumtendea haki na baada ya kupata ushahidi kufutilia mbali kesi hiyo.

Akizungumza na wanahabari, Msajili wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Iringa, Dunstan Nduguru aliwashangaa Polisi kwa kuingia shughuli za mahakama.

"Hata kama mwandishi huyo angekuwa anapiga picha, haikuwa kazi yao kumkamata mpaka wapewe agizo na Jaji Mfawidhi aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo," alisema.

Pamoja na askari hao kuwazuia wanahabari kuchukua picha mara baada ya mtuhumiwa huyo kufikishwa mahakamani, Nduguru alisema utaratibu wa mahakama unawaruhusu wanahabari kuchukua picha kabla shughuli kabla shughuli za mahakama hazijaanza na baada ya shughuli hizo kwisha.

"Kuwazuia wanahabari kufanya kazi zao kwa utaratibu huo sio sahihi; siku nyingine mkiona kuna dalili ya kupata bugudha kama hiyo naomba mnijulishe ili niondoe mzozo huo," alisema. 

Mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Iringa, Mary Shangali, Wakili wa upande wa mashtka, Adolph Maganga alisema Adolph Maganda alisema kwa kukusudia mtuhumiwa Pacificius Cleophace Simoni anatuhumiwa kumuua Mwangosi kinyume na kifungu cha sheria ya kanuni ya adhabu namba 196 sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Alisema katika tukio hilo lililotokea Septemba 2, 2012 katika kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi mkoani Iringa, mshtakiwa alifyatua bunduki yake na kusababisha kifo cha marehemu, papo hapo.

Alisema siku ya tukio marehemu alikuwa Nyororo kwa ajili ya kuripoti na kutoa taarifa kwa umma juu ya mkutano uliokuwa ufanywe na katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Alisema mshtakiwa akiwa mmoja wa wafanyakazi wa Polisi, waliwasihi Chadema wasifanye mkutano huo kabla wafuasi wake hawajaanza kurusha mawe kwa Polisi na baadhi yao kupata majeraha.

Kutokana na mzozo huo, wakili huyo wa serikali alisema polisi walipiga mabomu ya machozi ili kuwatawanya wafuasi hao kabla mshtakiwa huyo hajamfyatulia bomu marehemu.

Wakili huyo aliwasilisha ramani ya eneo la tukio, ripoti ya mtaalamu wa milipuko na ripoti ya daktari aliyechunguza mwili wa marehemu Mwangosi na gazeti la Mwananchi la Septemba 3, 2012 lililochapisha  picha ya tukio hilo katika ukurasa wa mbele kama vielelezo vinavyohusiana na kesi hiyo.

Wakili wa upande wa utetezi Lwezaula Kaijage alitaja mambo wanayokubaliana katika kesi hiyo kuwa ni jina na anuani ya mshtakiwa na kwamba marehemu Mwangosi alikufa kifo ambacho si cha kawaida.

Na kwamba mshtakiwa Simoni alikamatwa na amefikishwa mahakamani akihusishwa na mauaji hayo.

Wakili Kaijage alisema vielelezo vingine vilivyoletwa na upande wa mashtaka hawakubaliani navyo kwakuwa vinahitaji ushahidi kutoka kwa wahusika.

Jaji Shangali aliahirisha kesi hiyo mpaka kikao kingine cha mahakama kuu kitakapoitwa ili ianze kusikilizwa.

MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni