Jumapili, 15 Juni 2014

CCM - “STOP” WAKULIMA KUTOZWA USHURU WA MAZAO

 Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga - a.k.a "Mwarobaini" jina alilopewa na wananchi wa Pawaga baada ya kutatua changamoto zilizokuwa zikiwakabiri kwa muda mrefu.
 Diwani wa Kata ya Itunundu Halfan Lulimi (Mwenye shati la Kijani)  akiwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Steven Mhapa, katika mkutano wa hadhara wa wakulima na wananchi wa Itunundu Pawaga.
 Kulia ni mwenyekiti wa umoja "Tuungane" wa wakulima wa zao la Mpunga katika Kata ya Itunundu Pawaga- Wilaya ya Iringa akiwa na Twarib Abdlahaman Ubwa ambaye ni katibu wa Tuungane- wakiwa katika mkutano huo.
 Baadhi ya wananchi wa Pawaga wakisikiliza jambo kwa makini katika mkutano wa kujadili changamoto zinazowakabiri, mkutano uliohudhuriwa na katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga - aka. MWAROBAINI.
  Baadhi ya wananchi wa Pawaga wakisikiliza jambo kwa makini katika mkutano wa kujadili changamoto zinazowakabiri, mkutano uliohudhuriwa na katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga - aka. MWAROBAINI.


 Mzee Mussa Kibuga (Mwenye Shati la Blue) akisikiliza kwa makini masuala yanayojadiliwa katika mkutano baina ya wananchi, wakulima,  viongozi wa CCM na wale wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuhusiana  na changamoto zinazowakabiri.
 Baadhi ya wananchi wa Pawaga.
 Baadhi ya wananchi wa Pawaga wakisikiliza jambo kwa makini katika mkutano wa kujadili changamoto zinazowakabiri, mkutano uliohudhuriwa na katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga - aka. MWAROBAINI.
  Baadhi ya wakulima wa zao la Mpunga -Pawaga wakisikiliza jambo kwa makini katika mkutano wa kujadili changamoto zinazowakabiri, mkutano uliohudhuriwa na katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga - aka. MWAROBAINI.

   Baadhi ya wakulima wa zao la Mpunga -Pawaga wakisikiliza jambo kwa makini katika mkutano wa kujadili changamoto zinazowakabiri, mkutano uliohudhuriwa na katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga - aka. MWAROBAINI.
 Kulia ni mwenyekiti wa umoja "Tuungane" wa wakulima wa zao la Mpunga katika Kata ya Itunundu Pawaga- Wilaya ya Iringa akiwa na Twarib Abdlahaman Ubwa ambaye ni katibu wa Tuungane- wakiwa katika mkutano huo.



Baadhi ya wananchi wa Pawaga wakisikiliza jambo kwa makini katika mkutano wa kujadili changamoto zinazowakabiri, mkutano uliohudhuriwa na katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga - aka. MWAROBAINI.

<<<HABARI>>>.

CHAMA cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa kimemaliza mgogolo + malalamiko baina ya wakulima wa zao la Mpunga na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, yaliyotokana na ongezeko la tozo la ushuru.

Wakulima hao wa zao la Mpunga wa kata ya Itunundu na kata nyingine za Tarafa ya Pawaga wanaojihusisha na shughuli za kilimo cha Mpunga wamekuwa wakilalamikia ongezeko la tozo la ushuru kwa muda mrefu ushuru wa kutoka shilingi elfu moja hadi kufikia elfu mbili.

Wakifikisha malalakimo yao kwa katibu wa CCM aliyefika katika tarafa hiyo kusikiliza kilio cha wakulima hao, ambao wengi wao wapo chini ya Mwamvuli wa kikundi cha Tuungane, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kimande- baina ya wakulima na viongozi wa Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Iringa.

Twarib Abdulhaman Ubwa katibu wa kikundi cha Tuungane cha wakulima wa zao la Mpunga amesema kupandishwa kwa tozo la ushuru kumewafanya wanunuzi wa Mpunga kushindwa kuingia katika tarafa yao kwa kwenda katika maeneo mengine ambayo hayana kiwango hicho cha ushuru.

Ubwa amesema hali hiyo ni pigo kubwa kwao kwani sasa wamekosa wateja hali inayowafanya wauze Mpunga wao kwa bei ndogo kwa weanunuzi wachache wanaotokea, hali ambayo itawakwamisha kuendesha shughuli hiyo.

“Kama unavyoona kila nyumba ukipita ni magunia ya Mpunga, hayana wateja, hali hiyo imechangiwa sana na ongezeko la Ushuru, wanunuzi wote ambao huwa tunawategemea hawafuiki kwetu kununua Mpunga, wanakwenda katika maeneo mengine, hili ni janga na adhabu hii wenye kuumia ni sisi wakulima sio wafanyabiashara,” Alisema Ubwa.

Ubwa alisema kuna haja ya Halmashauri kupunguza tozo hilo na kufikia kiwango kile kile cha awali, kwani changamoto hiyo ya ushuru kwa mtazamo wa kina unaweza kuathiri masuala mbalimbali likiwemo la wakulima kushindwa kujikimu na hata kukwama kulipa adha za watoto wao kwa kukosa fedha.

Naye Festo Elioti Kulanga ambaye ni mwenyekiti wa kikundi cha Tuungane amesema gharama hiyo ya ushuru wa shilingi elfu mbili kwa gunia moja, itawafanya wakulima kushindwa kununua pembejeo na zana za kilimo za za kisasa.

Kulanga alisema baadhi ya wenye magari nao wamegoma kupeleka magari yao kuchukua mpunga katika eneo hilo kwa kuhofia ushuru mkubwa wa magari kwani gari moja limekuwa likitozwa hata zaidi ya shilingi Milioni moja jambo ambalo halina tija kwa mkulima, mfanyabiashara na hata msafirishaji.

“Katibu hapa kero yetu kubwa sisi ni ushuru, kero ambayo tumeilalamikoa kwa muda mrefu licha ya kupewa majibu kuwa wataitatua lakini hakuna kinachofanyika, ushuru ni mkubwa sana, lakini pia wakala anayetoza ushuru amekuwa pia akijihusisha na rushwa ambapo kila gari limekuwa likilipishwa shilingi milioni moja ,” Alisema.

Aidha alisema kuna gari ya Maprosoo T. 910 AMV ambayo ililipishwa  shilingi Milioni kwa gunia 120 alizopakia, ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi elfu 8 mia 8 na elfu 3 333 ilikuwa inaendeshwa na Feisary.

“Ilipita  gari ya mtu anaitwa Medy gari namba  T.600 AJV ililipa shilingi laki 642, 000 ambayo ukigawa kwa gunia moja ni sawa na shilingi 5352, na ilipita gari ya Massey ambayo ililipa shilingi milioni moja sawa na shilingi 8333, na wenye magari hao wamegoma kusafirisha mazao yetu mpaka tupate hitimisho la Ushuru huo”, Alisema Kulanga.

 Hata hivyo katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo, amepiga marufuku utozaji wa ushuru kwa mkulima anayesafirisha Gunia 1 hadi 6 za mazao, kwenda mjini au Sokoni, kwa madai kuwa kuwabana kwa ushuru huo wakulima kutakwamisha kupata fedha za kuendeshea shughuli hizo.

Mtenga ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kupitia mwenyekiti wake Steven Mhapa kuacha mara moja tabia ya kuwatoza wakulima kiwango hicho cha ushuru, na kuwa watafute namna nyingine ya kuongeza mapato ya Halmashauri pasipo kuwakandamiza wakulima, kwa madai kuwa gharama hizo za utozwaji wa ushuru zinafifisha kaulimbiu ya Kilimo kwanza.


Mtenga amesema tatizo la baadhi ya viongozi kutokuitisha mikutano ya hadhara, linasababisha malalamiko mengi kwa jamii, na hivyo baadhi ya wananchi kukimbilia vyama pinzani, kwa kukosa sehemu ya kupata ufumbuzi wa changamoto zinazowakabiri.

Na kuwa viongozi wote wanaokwepa majukumu ya kuwahudumia wananchi, atahakikisha anawachukulia hatua kali za kinidhamu, kwa madai kuwa viongozi wa aina hiyo  ndiyo wanaokwamisha jitihada za Chama cha mapinduzi katika kuwaletewa maendeleo wananchi.

Hata hivyo mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Iringa Steven Mhapa amesema ongezeko la ushuru huo umelenga kutatua changamoto mbalimbali za wakulima, kwa kuboresha huduma, huku akisema baadhi ya wakulima wamekuwa hawataki kubadilika pindi wanapogeuka kuwa wafanyabiashara na malalamiko hayo ni njia ya kukwepa kodi.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa umebaini ukubwa wa tatizo hilo, kwani kila nyumba katika Tarafa hiyo yamejazana magunia ya Mpunga ambayo hayana wateja, jambo ambalo linaweza likawakatisha tamaa ya kuendelea na shughuli za kilimo wakulima hao.

Kwa kawaida msimu huu wa mwezi 6 Mpunga huuzwa kwa zaidi ya shilingi elfu 50 hadi 70 lakini kutokana na hali hiyo wakulima hao wanalazimika kuuza shilingi 35 gunia lenye debe 7 huku baadhi yao wakiwa wamekata tamaa kabisa hata kuvuna na hivyo kuuacha Mpunga huo bado kwenye Majaruba ambayo yanamaji jambo ambalo ni hatari katika sekta hiyo ya kilimo.

MWISHO


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni