Jumatatu, 16 Juni 2014

SERIKALI KUPELEKA MUSWADA WA HABARI BUNGENI

  Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo Assah Mwambene

 Mmoja wa wahadhiri wa chuo kikuu cha Iringa akizungumza na wahitimu wa kitivo cha habari katika siku ya habari chuoni hapo- ambapo mgeni rasimi alikuwa mkurugenzi wa idara ya habari maelezo Assa Mwambene.

<<<HABARI>>>
 
BAADA ya kilio cha muda mrefu cha wanahabari juu ya sheria ya habari nchini, serikali imeibuka na kusema tayari muswada huo upo tayari huku ikiahidi kuupeleka bungeni ili kujadiliwa mara tu baada ya bunge la bajeti kumalizika.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa idara ya habari maelezo Assah Mwambene, wakati akizungumza na wanafunzi wahitimu wa mwaka wa tatu wa chuo kikuu cha Iringa, katika maadhimisho ya siku ya habari chuoni hapo.

Mwambene amesema muswada huo upo tayari na utapelekwa, na kuwa kikao chochote kinachohusika na kutungwa kwa sheria muswada huo utajadiliwa,

Amesema sambamba na sheria ya kusimamia vyombo vya habari, serikali imekamilisha utafiti wa sheria ya haki ya kupata habari, ambapo imejifunza kutoka kwa nchi ambazo tayari zina sheria  kama hiyo ili kujidhatiti na kupata sheria nzuri itakayofaa zaidi.

Mwambene amesema katika sheria hiyo ya kusimamia vyombo vya habari kuna mapendekezo ya kuwepo kwa bodi ya kusimamia taaluma ya habari ili kuwadhibiti watu ambao hawana vigezo ambao   wamekuwa wakiiharibu taaluma ya habari.

Amesema katika sheria hiyo ambayo ndiyo itakuwa msingi pia wamependekeza kuwe na bodi itakayosimamia taaluma ya uandishi wa habari ili kuweka vigezo vitakavyosimamia wanaofaa na wasiofaa kuwa waandishi wa habari na wale watakaokosa vigezo kamwe hawataruhusiwa kufanya kazi hiyo kama ilivyo sasa.

Mwambene amesema lengo kuu la kuweka udhibiti na  kuongeza heshima katika taaluma hiyo ili ithaminiwe kama zilivyo taaluma nyingine, kwani watakuwa wamepunguza uwepo wa wavamizi wa taaluma ya habari ambao wanafahamika kama “Makanjanja”.

“Katika sheria hiyo ya uandishi wa habari ambayo ni msingi pia tumependekeza kuwe na bodi ambayo itakayosimamia taaluma hii ya uandishi wa habari,  bodi hiyo itasaidia kuweka vigezo vya msingi vitakavyosimamia nani atakayefaa kuwa mwandishi hwa habari na wale watakaokosa vigezo kamwe hawataruhusiwa kufanya kazi hiyo, hii bodi itaweka udhibiti pamoja na kuongeza heshima katika taaluma hii ya habari ili ithaminiwe na jamii kama ilivyo kwa taaluma nyingine, kwani bodi itapunguza uwepo wa “Makanjanja”, Alisema.

Aidha Mwambene amewataka wanachuo hao wahitimu pindi waingiapo katika taaluma ya habari  kufanya kazi kwa weredi wa hali ya juu, kwa madai kuwa jamii imekuwa ikiwategemea wanahabari katika kupata masuala yenye uhakika kwa kuwa kada hiyo ina wajibu na umuhimu mkubwa katika jamii.

Amewataka kuwa makini na kutofanya kazi kwa ushabiki pasipo kucheza na taaluma yao ili kuondoa changamoto zitokanazo na baadhi ya wanataaluma kutofanya kazi zao kwa kufuata maadili ambayo ni miiko ya kazi yao.

Tumaini Msowoya na Solomoni Lekui wanafunzi wa mwaka wa tatu wa chuo kikuu cha Iringa ambao ni wasomi wa tasnia ya habari wamesema Muswada huo ni muhimu na umekuja katika wakati muafaka, kwani utasaidia kupunguza changamoto zinazowakabiri wanahabari, ikiwa pamoja na changamoto inayotokana na sheria ya mwaka 1976 inayotoa mamlaka makubwa kwa waziri husika kukifungia chombop cha habari wakati wowote.


Nao Wahadhiri wa chuo kikuu cha Iringa kitivo cha habari - Simon Berege na Rachel Yusuph wamesema muswada huo ni mkombozi wa wanahabari, kwani hicho kimekuwa ni kilio cha muda mrefu cha waandishi na kuwa sasa itasaidia wanahabari kufanya kazi kwa ufanishi, ikiwa pamoja na kujenga demokrasia ya kweli nchini.

“Muswada huo ukipitishwa na kuwa sheria utakuwa ni ukombozi kwa tasnia yetu, kwani itaitengenezea heshima kwa kuweka viwango vya elimu na pia itasaidia kuwasukuma wanahabari kwenda kusoma ili kukidhi vigezo vya kuwa wanahabari wanaotambulika,”

Hata hivyo wameitaka serikali kuongeza muda wa kipimo cha uandishi kwa madai kuwa muda wa  miaka 63 ni mfupi  na badala yake waongeze na kufikia  miaka sita ili kutoa nafasi kwa wanahabari kujiandaa na kujipanga kusoma na kufikia kiwango cha elimu ya shahada na Stashahada (Diploma na Degree). 
MWISHO.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni