Jumatatu, 23 Juni 2014

JIWE LA AJABU LATOA TIBA ZA MARADHI MBALIMBALI


 Baadhi tu ya eneo la jiwe la Liganga lya Mtwivila- lililopo wilaya ya kilolo mkoani Iringa.
 Jiwe la Liganga lya Mtwivila.
 Wenyeki wa kijiji cha Kihesamgagao wakiwa katika eneo hilo la jiwe la ajabu.
 Mmiliki wa mtandao huu bi. Oliver Motto ambaye ni mwandishi wa habari wa Star Tv, RFA nk. akiwajibika kwa kupata picha za kuijulisha jamii juu ya uwepo wa kivutio cha jiwe hilo lenye ukubwa wa ajabu pamoja na maajabu yake.
 Laulian Mkumbata mwandishi wa habari wa ITV na radio One, akiwajibika.
 Joseph Muhumba mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kihesamgagao.

 Yerfred Muyenzi mkurugenzi wa haki ardhi akiwa na kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Ubald Wampembe wakiwa katika kijiji cha Kihesamgagao, wakitoa elimu ya umuhimu wa ardhi.
 Isdoly Kindole mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kihesamgagao ambaye pia ni diwani wa kata hiyo akizungumza na wananchi wake katika mkutano wa elimu ya haki ardhi.
 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kihesamgaga.
 Wakisikiliza kwa umakini zaidi.
 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kihesamgagao wakiwa katika mkutano wa Haki ardhi wakipatiwa elimu pamoja na hati miliki za kimila.
  Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kihesamgagao wakiwa katika mkutano wa Haki ardhi wakipatiwa elimu pamoja na hati miliki za kimila.
 Wakishukuru baada ya kupatiwa elimu hiyo ya haki ardhi.

 Wakipokea hati miliki za kimila za umiliki wa ardhi kwa mkurugenzi wa Haki ardhi Yefred Muyenzi.


  Isdoly Kindole mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kihesamgagao ambaye pia ni diwani wa kata hiyo akipokea hati miliki ya kimila, na kuishukuru ofisi ya Haki ardhi kwa kuwapelekea elimu hiyo ambayo itakuwa ni mkombozi kwao.
 Baadhi ya wananchi wakiwa na hati miliki za kimila ambazo zitasaidia kuiongezea thamani ardhi yao wananchi wa kijiji cha Kihesamgagao- Kilolo- Iringa.
 "Ninayo hati yangu sasa" ni kama anajivuna kwa kuwaza hivyo- Mwananchi wa kijiji cha Kihesa mgagao, baada ya kupokea hati miliki za kimila.

  Baadhi ya wananchi wakiwa na hati miliki za kimila ambazo zitasaidia kuiongezea thamani ardhi yao wananchi wa kijiji cha Kihesamgagao- Kilolo- Iringa.


 <<<HABARI>>>
LICHA ya kuwa Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi vya Utalii, zikiwemo hifadhi za wanyamapori, kumbukumbu za kihistoria za mambo ya kale - bado kuna baadhi ya vivutio havijatambuliwa na vingine vilivyotambulika havithaminiwi.

Jiwe “Liganga Mtwivila” lipo katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa -ni moja ya kivutio kikuu cha utalii, ambacho kingeliingizia Pato Taifa, na hivyo uchumi wa kijiji, Wilaya, mkoa na hata Taifa kukua.

Lakini kutokana na kutopewa kipaumbele kwa kivutio hicho cha jiwe la "Liganga lya Mtwivila" kumesababisha kutokuwepo kwa  manufaa na umuhimu wa uwepo wa jiwe hilo, kwani halina tija, licha ya watalii kumiminika kuliona jiwe hilo la ajabu.

Baadhi tu ya maajabu ya jiwe hilo la "Liganga lya Mtwivila" ni kutumika kama dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali, kwakuwa mimea iliyoota juu ya jiwe  hilo wananchi wa kijiji cha Kihesamgagao wanaitumia kujitibu maradhi yanayowasumbua.

Aidha jiwe hilo la ajabu licha ya kuota majani ambayo ni tiba, pia linatiririsha maji ambayo nayo pia hutumika kuponya magonjwa ya kila aina, ama hakika jiwe hili lina kila sababu kuwa ni kivutio kikubwa.

Wenyeji wa kijiji cha Kihesamgagao pia wanalitumia jiwe hilo la Liganga Mtwivila kwa kuomba mahitaji mbalimbali mizimu kutokana na imani zao, Huko mkoani Iringa katika kijiji cha Kihesamgagao kama hitaji la Mvua ikiwa pamoja na kuendeshea ibada za kimila kwa maana ya matambiko.

Philimon Kagine ni mkazi wa kijiji cha Kihesamgagao amesema hawana shida ya kuhangaika na matibabu, kwani mimea yote ilioota katika jiwe hilo ni dawa, ambazo zimekuwa zikitibu kwa uhakika.

Kagine amesema dawa hizo wanaziamini zaidi kule zile za kitaalamu kwa madai kuwa hizo hawatumii kwakuwa zina Kemikali na kuwa kuna wakati jiwe hilo lilikuwa linamwaga neema ya fedha ambazo walikuwa wanaokota na hivyo kuwa na unafuu wa maisha.

Afisa ardhi wa wilaya ya Kilolo Elinaza Kiswaga amesema kumekuwa na tatizo kubwa la baadhi ya wananchi kuuza ardhi kwa wawekezaji, na hali hiyo inatokana na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa rasilimali hiyo ardhi.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kihesamgagao ambaye pia ni diwani wa Kata hiyo Isdory Kindole amesema hakuna faida yoyote itokanayo na jiwe hilo- kwani watalii kutoka nje ya nchi wamekuwa wakifika kuliona jiwe hilo pasipo kulipia chochote.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Joseph Muhumba amesema sasa ni marufiku wananchi kufanya shughuli za kibinadamu katika eneo hilo- kwani kwa kufanya hivyo historia ya jiwe hilo inaweza kupotea.

Muhumba amesema ipo haja kwa watanzania kufika katika kijiji cha Kihesa mgao ili kuliona jiwe hilo la ajabu na lenye ukubwa wa aina yake.

Ofisi ya haki ardhi kupitima mkurugenzi wake mtendaji Yefed Muyenzi  - inatoa onyo la uuzaji wa ardhi kiholea kwani kuna dalili za kuliuza eneo hilo la utalii.

Muyenzi kupitia ofisi yake ya ardhi wametoa elimu ya matumizi bora ya ardhi, ikiwa pamoja na kuacha kuwaonya wananchi kuacha tabia ya kuuza kiholela ardhi, kwa madai kuwa wao wanavyozaliana na kuongezeka lakini ardhi haiongezeki jambo ambalo siku za baadaye litachangia migogolo mingi ya ardhi.

Hata hivyo Muyenzi amewaasa wananchi kuwa makini na wawekezaji wanaofika vijijini na kuwarubuni kwa fedha ili kupata ardhi kwa madai kuwa baadaye wananchi hao wanaweza kugeuzwa watumwa na wakimbizi katika vijiji vyao.

MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni