Alhamisi, 26 Juni 2014

MIRADI YA ZAIDI YA SH. BIL. 3 KUZINDULIWA NA MWENGE


 Mwenge wa Uhuru ukiwa mpaka mwa mkoa wa Iringa na Morogoro- katika Kata ya Ruaha mbunyuni Iringa.
 Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma akitoa taarifa ya mbio za mwenge mkoani Iringa, muda mfupi mara baada ya kuupokea kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera.
 Askari akionyesha utii, heshima, nidhamu kama ni sehemu ya  uzalendo wa Mtanzania, kwa kuulinda Mwenge ambao ni alama ya uhuru wa Tanzania.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Dk. Christine Ishengoma (Kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerlad Guninita katika eneo la Ruaha Mbuyuni mara tu baada ya kuupokea mwenge huo kutoka mkoani Morogoro.


<<<HABARI>>>

 MWENGE wa Uhuru ambao upo mkoani Iringa ukitokea mkoani Morogoro- unataraji kuzindua miradi  42 ya maendeleo yenye thamani zaidi ya shilingi Bilioni 3 na Milioni 109.

Hayo yamezungumzwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Dk. Christine Ishengoma wakati akipokea Mwenge huo wa Uhuru eneo la Ruaha Mbunyuni- katika wilaya ya Kilolo, kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera.

Dk. Ishengoma amesema miradi inayozinduliwa na mbio za Mwenge mkoani Iringa- niya sekta ya maji, sekta ya afya, elimu na miradi ya maendeleo ya jamii - yote ikiwa na umbali wa km 1159.

Aidha amesema fedha za miradi ya maendeleo itakayozinduliwa  ni michango mbalimbali kutoka serikali kuu, wadau wa maendeleo, Halmashauri na manispaa, huku  mwenge huo akiukabidhi kwa mkuu wa Wilaya ya Kilolo kama ni sehemu ya kuanza rasmi kwa kazi za kukimbiza Mwenge  mkoani Iringa.

Hata hivyo Dk. Ishengoma alimkabidhi Mwenge huo wa Uhuru mkuu wa Wilaya ya kilolo Gerlad Guninita kwa minajiri ya kuwa unaanza kazi ya kuzindua miradi ya maendeleo katika Wilaya hiyo ya Kilolo.
MWISHO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni