Alhamisi, 26 Juni 2014

KILOLO YAZINDUA MIRADI YA ZAIDI YA SH. MILIONI 841.


 Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerlad Guninita akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru tayari kwa kuanza mbio katika vijiji 9 vya Wilayani humo.
 Katikati ni Setty Mwamotto mwenyekiti wa CCm Wilaya ya Kilolo- akiwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Joseph Muhumba(Kushoto) huku kulia akiwa ni kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Rachel Kassanda.
 Viongozi wa Wilaya ya Kilolo wakishika Mwenge kama ishara ya kuupokea na kuanza mbio katika Wilaya hiyo.
Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Rachel kassanda akizungumza na wananchi wa Ilula Wilayani Kilolo, hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya mbio za mwenge wa Uhuru.

<<<HABARI>>>
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imefanikiwa kujenga nyumba  nne za watumishi, kwa lengo la kuharakisha utekelezaji wa majukumu ya kazi ili kufanikisha mpango wa matokeo makubwa sasa- yaani BRN.

Hayo yamezungumzwa na mkuu wa wilaya hiyo ya Kilolo Gerlad Guninita wakati akitoa taarifa ya shughuli za maendeleo katika Wilaya hiyo- kwa wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka 2014,  ambapo nyumba hizo ni kati ya miradi iliyozinduliwa na mbio za Mwenge.

Guninita amesema kukamilika kwa ujenzi wa nyumba hizo nne kumegharimu zaidi ya shilingi 227,  huku nyumba tatu zikijengwa kwa gharama ya shilingi milioni 150 sawa na kiasi cha shilingi Milioni 50 kila nyumba moja, na nyumba moja pekee ikigharimu shilingi 68.

Aidha  amesema zaidi ya shilingi Milioni 172 ni mchango kutoka  ruzuku maalumu ya maendeleo (CDG)  huku shilingi milioni 55 zikitoka katika mfuko wa mpango wa afya ya msingi MMAM.

Amesema Mwenge huo utakimbizwa katika Vijiji 9, Kata 4 na tarafa 3 kwa umbali wa km. 273 kwa kuzindua jumla ya miradi 9 yenye thamani ya shilingi Milioni 841, 577, 350.05

Naye kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Kilolo Ulbad Wampembe amesema pia Halmashauri hiyo imefanikiwa kujenga vyumba vitatu vya madarasa na nyumba moja ya mkuu wa shule ya sekondari ya Ilula.

Wampembe amesema kukamilika kwa ujenzi huo kumegharimu zaidi ya shilingi Milioni 143 huku mpango huo ukitekelezwa na mradi wa benki ya dunia kwa kushirikiana na serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Aidha Wampembe amesema lengo la ujenzi huo ni kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu kwa wanafunzi na walimu yawe rafiki ili kuinua kiwango cha elimu.

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Rachel Kassanda ameitaka halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kutopokea majengo hayo kutoka kwa mkandarasi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule ya sekondari Ilula kwa madai kuwa sakafu yake ina nyufa kabla ya kukabidhi jengo hilo.

Hata hivyo Kassanda amekubaliana na jengo la nyumba ya mkuu wa shule Ilula, kwa madai kuwa imejengwa kwa kiwango kizuri kinachoendana na thamani halisi ya fedha.

MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni