Jumatatu, 8 Septemba 2014

CWT YAITANGAZIA MKWARA SERIKALI - YATOA SIKU 14 ILIPE MADENI YOTE

Jengo la chama cha walimu CWT Mkoa wa Iringa. 
 Mwenyekiti wa Chama cha walimu CWT Mkoa wa Iringa Mwalimu Stanslaus Mhongole, akisikiliza jambo katika mkutano wa kutoa tamko baina ya uongozi wa CWT na baadhi ya wanahabari mkoani Iringa.
 
 Katibu wa CWT Mkoa wa Iringa Mshamu Ally Mshamu akiwa katika mkutano baina ya baadhi ya wanahabari mkoani Iringa na uongozi wa CWT - wakati wakitoa tamko.
 Baadhi ya viongozi wa CWT mkoa wa Irinbga wakisikiliza jambo kutoka kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati wa utoaji wa tamko.

 Frenk Leonard- Mwandishi wa habari wa gazeti la Habari leo na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani Iringa akiwa katika mkutano huo wa CWT.
 Geofrey Nyang'olo- mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi akiwajibika katika mkutano huo wa CWT.
Heriety mwandishi na mtangazaji wa kituo cha redio County fm  akisikiliza jambo kutoka kwa viongozi wa CWT mkoa wa iringa.
 Yohana Mgaya mtangazaji na mwandishi wa habari wa kituo cha redio Furaha akiwa kazini katika mkutano huo.
 Victory Meena mtangazaji na mwandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru fm akiwajibika kazini.
 Eliasa Ally mwandishi wa habari wa gazeti la Majira akifuatilia jambo katika mkutano huo baina ya viongozi wa CWT na wanahabari.
 Silvanus Kigomba mwandishi wa habari wa Televisheni ya ITV na radio One, akiwa kazini katika mkutano huo wa CWT.

Yuvenary  Kimario mwandishi wa habari wa kituo cha radio Country fm na mwakirishi wa gazeti la Nipashe. akiwa kazini

 

 


 


<<<HABARI>>>

CHAMA cha walimu Tanzania- CWT mkoa wa Iringa kimetoa siku 14 kwa Serikali mkoani humo, iwe imelipa madeni  yote inayodaiwa na walimu wake– huku kikitishia kutofanyakazi  kuanzia Septembe 15 endapo agizo hilo halitatekelezwa.

CWT imesema kamwe haiwezi kuendelea kuifumbia macho serikali, huku walimu wake wakiishi maisha duni na yenye kukatisha tamaa, na mbaya zaidi kikilalamikia punguzo la fedha za mifuko ya jamii, ambazo huwasaidia watumishi pindi wanapostaafu.

Akisoma tamko hilo mbele ya baadhi ya waandishi wa habari mkoani Iringa – Mwalimu Stanslaus Muhongole ambaye ni mwenyekiti wa CWT mkoa wa Iringa amesema…

“Chama cha Walimu Mkoa wa Iringa kinaunga mkono Tamko la Chama makao makuu (CWT) na chama cha wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) kwa tamko lao walilolitoa kwa pamoja katika kupinga mpango wa serikali wa kupunguza Mafao ya wastaafu kupitia Mifuko ya hifadhi ya jamii.

Muhongole amesema wao kama walio wa mkoa wa Iringa wanasisitiza kuwa mpango huo wa serikali hauna nia njema kwa maendeleo ya nchi, hasa kwa walimu ambao wamekubali kulipwa mishahara midogo isiyokidhi mahitaji.

Amesema licha ya walimu kuwa na mishahara duni lakini wamekubali kukatwa sehemu ya mishahara hiyo na kuiwekeza katika mifuko ya hifadhi ya jamiiili iwe na manufaa pindi wanapostaafu.

…..“Chakushangaza serikali badala ya kuboresha mafao ya walimu ndani ya mifuko hiyo, tena inashiriki kuchukua fedha kwenye mifuko yetu kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake na hivyo kuwaacha walengwa wa mifuko wakiambulia fedha kiduchu tofauti na hali halisi ya uwekezaji,” amesema.

Mhongole amesema Wizara ya kazi na ajira kwa kushirikiana na Mamlaka ya mifuko ya hifadhi ya jamii (SSRA) inadiriki kuandaa mpango wa kupunguza mafao ya wanachama wastaafu wa mifuko hiyo ya pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF) na watumishi wa serikali za mitaa (LAPF) ili kuibeba Serikali dhidi ya madeni inayodaiwa na mifuko.

Amesema mpaka sasa Serikali inadaiwa takribani shilingi Tilioni 7, Bilioni 134, Milioni 300 ilizokopa kwenye mifuko hiyo ambayo watumishi hukatwa mishahara yao kwa lengo la kuhifadhi kwa matumizi wakati wanapostaafu.

Akitaja mifuko na kiwango cha fedha zilizochukuliwa na serikali, amesema...
Mfuko wa PSPF inadai shilingi 4, 827, 800, 000, 000/=
Mfuko wa LAPF unadai shilingi 2017, 700, 000, 000/=
Mfuko wa NSSF unadai shilingi 1, 333, 600, 000, 000/=
Mfuko wa PPF unadai shilingi 288, 600, 000, 000/=
Mfuko wa GEPF unadai shilingi 18, 000, 000, 000/=
Mfuko wa NHIF (wa afya) unadai shilingi 458, 600, 000/=

Aidha amesema hali mbaya ya mifuko hiyo inatokana na fedha nyingi zilizochotwa na serikali pasipo kuzirejesha kwa wakati, na sasa imeanza kupunguza malipo ya Pensheni ya mkupuo kutoka asilimia 50 ya sasa hadi asilimia 33.3 ya mshahara kabla ya kustaafu.

Pia amedai kuwa serikali inatumia wastani wa mshahara wa miaka 3 badala ya mshahara wa mwisho kukokotoa Pensheni.

Na kuwa imekuwa ikipunguza makadirio ya umri wa kuishi – badala ya kustaafu kutoka miaka 15.5 hadi miaka 12.5.

Amesema pia iunafanya hira katika kurekebisha vikokotoo limbikizi (Accrual rates ) vya mifuko kutoka 540 kwenda 580 kwa mifuko ya PSPF na LAPF, na kuwa hali hiyo kamwe haikubaliki.

Hata hivyo amesema kama chama wanaisihi serikali iachane kabisa na mpango huo dharimu kwani unaua nguvukazi ya Taifa la leo, kesho nala miaka ijayo.

Naye katibu wa CWT Mkoa wa Iringa Mwalimu Mshamu Aly Mshamu amesema serikali inatakiwa ilipe madeni yake yote inayodaiwa na walimu, ifikapo septemba 14, na kama haitafanya ivyo Septemba 15 walimu wa Wilaya zote watakutana katika ofisi ya mwajiri wao kwa kila Wilaya.

Mshamu amesema lengo la kufanya hivyo ni kuishinikiza serikali iwalipe stahiki zao walimu, kwani madeni hayo yanachangia kudhorotesha utendaji kazi wa walimu, na kuwa sasa kila mwalimu amdai mwajiri wake mpaka anapomlipwa.

Mshamu amesema tamko hilo linaitaka serikali kuanzia Septemba 1 mwaka huu mpaka 15 iwe imekamirisha madeni yote, kwani bila kufanya hivyo walimu watakaa katika ofisi za waajiri wao mpaka kutimia kwa sharti hilo.

Amesema walimu wilayani Mufindi wanadai serikali zaidi ya shilingi Milioni 159, huku Manispaa ya Iringa ikidaiwa na walimu wake zaidi ya shilingi Milioni 279, na Walimu wa Wilaya ya Iringa wakiidai Halmashauri hiyo zaidi ya shilingi Milioni 160.

Mshamu amesema Wilaya ya Kilolo nayo inadaiwa deni la zaidi ya shilingi Milioni 270 na walimu wake, na hivyo walimu mkoani Iringa kuidai Serikali jumla ya shilingi Milioni 871, 639, 188 na senti 70.

MWISHO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni