Kufuatia hatua ya Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Sospeter Muhongo kujiuzulu katika nafasi hiyo ya uwaziri, mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mh Zitto Kabwe amepongeza uamuzi huo wa Prof Muhongo ambapo amesema kuwa hatua hiyo ni heshima kubwa kwa bunge.
"Napenda kuchukua nafasi hii kutambua busara aliyochukua ambayo
naamini itasaidia harakati za kujenga demokrasia yenye uwajibikaji.
"Naamini uamuzi wa Ndugu Muhongo umewezesha kulinda heshima ya Bunge na
maazimio yake. Kwa muda mfupi alioongoza Wizara hiyo, Ndugu Muhongo
ameweza kuongoza mabadiliko kadhaa muhimu ya kiutendaji katika wizara
hiyo na taasisi zake.
"Hata hivyo, nafasi ya Wizara aliyokuwa anaongoza
katika suala la Tegeta Escrow imemtia doa kubwa ambalo ilikuwa lazima
awajibike.
"Naamini Rais Kikwete atamteua mtu mchapakazi na makini zaidi
atakayeweza kuendeleza yale mazuri ya Ndugu Muhongo na kurekebisha
mapungufu yaliyojitokeza." Amesema Zitto kupitia ukurasa wake wa
Facebook.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni