Jumatatu, 9 Februari 2015

IPI NI NAFASI SAHIHI YA ROOONEY UWANJANI?? (ANGALIA HAPA)


Louis van Gaal aliamua kumrudisha Rooney kutoka katika nafasi yake ya mshambuliaji wa kati kumpeleka kuwa kiungo katika wiki za hivi karibuni, lengo lake kubwa likiwa ni kuwapa nafasi Robin van Persie na Radamel Falcao kucheza mbele yake.

Kucheza kama kiungo wa kulia siku ya jumapili Rooney, ambaye ameshindwa kupiga shuti hata moja lenye malengo kwa mwaka 2015, alishindwa kushika mpira katika eneo la boksi la wapinzani wao West Ham- hii ni hali ya ajabu kwa mchezaji ambaye aliweza kupachika mabao 10 katika michezo 9 iliyopita katika uwanja wa Upton Park.

Lakini Muholanzi Van Gaal anaamini kuwa kufanya hivyo kuna muwezesha yeye kutumia mfumo wake wa 4-3-1-2 ambao anaamini kuwa Rooney anafurahia kwa sababu atakuwa anaenana na mfumo wake.

“Sisemi kwamba kila siku atacheza kiungo hapana hii inategemeana na mfumo wa siku hiyo upoje na aina gani ya washambuliaji ninaotaka kuwatumia lakini katika mchezo unaofuata nitamtumia kiungo mwingine." alisema Van Gaal
“Nafikiri anapenda kucheza nafasi ya kiungo kwa sababu muda wote anatafuta mpira,lakini anauwezo wa kucheza nafasi nyingi tu."

Rooney hajafanikiwa kucheza vizuri akiwa nafasi ya kiungo.

Manchester Utd v Burnley

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni