Alhamisi, 5 Februari 2015

JIONEE MAAJABU KATIKA SOKA LA MWAKA 2015.......

Katika hali ya kushangaza na isiyo ya kawaida imetokea tena katika ulimwengu wa soka duniani baada ya timu ile ambayo katika ligi kuu nchini kwao kushikilia mkia ikitarajiwa kushuka lakini ndio inayofanya vizuri katika michuano ya UEFA .

Klabu ya Borussia Dotmund sio ngeni masikioni na machoni mwa kila mwana soka anayefuatilia michuano mbalimbali, na hii ndiyo timu iliyofunga mwaka ikiwaacha watu na wachambuzi mbalimbali midomo wazi kutokana na matokeo yake katika Bondes liga.

Borussia Dotmund ambayo imemaliza katika hatua ya makundi ya UEFA ikiwa kileleni mwa kundi D kwa jumla ya pointi 13 ikiwaacha nyuma Arsenal,Anderlecht pamoja na Galatasaray, maajabu yameibuka katika ligi ya Ujerumani maarufu kama Bondesliga baada ya kujikuta timu hiyo ikishikilia mkia.

Dortmund tangu uanze msimu wa 2014/2015 wameambulia pointi 16 tu kati ya michezo 19 huku waliokuwa wapinzani wao msimu uliopita Bayernmunich wakiwa kileleni kwa jumla ya pointi 46, tofauti ya pointi 30.

Aidha kutokana na hali hiyo kuna baadhi ya viongozi wameibuka na kusema kuwa tatizo kubwa ni UKATA wa fedha uliopo klabuni hapo


UEFA HATUA YA MAKUNDI

1Borussia Dortmund6411144+1013
2Arsenal6411158+713
3Anderlecht6132810-26
4Galatasaray6015419-151

BONDESLIGA MSIMAMO

1Bayern Munich191441439+3446
2Wolfsburg1911533819+1938
3Borussia M.Gladbach199642716+1133
4Augsburg1911082622+433
5Bayer Leverkusen198832920+932
6Schalke 04199463022+831
7Hoffenheim197573130+126
8Hannover 96197482228-625
9Eintracht Frankfurt196673639-324
10FC Cologne196581923-423
11Werder Bremen196583040-1023
12Mainz 051941052524+122
13Hamburger SV195591221-920
14Paderborn194782134-1319
15Freiburg193972127-618
16VfB Stuttgart194692033-1318
17Hertha Berlin1953112438-1418
18Borussia Dortmund1944111827-916

Hiki ndicho kikosi cha Borussia Dortmund kinachoonekana kipo vizuri lakini sio kwa Bondesliga.


Lewandowiski akishangilia goli alipokuwa Dortmund kabla ya kuelekea Bayern msimu huu wa mwaka 2014/2015.



Staili mbali mbali za ushangiliaji wa wachezaji wa Borussia Dortmund wakipata ushindi.


Wachezaji wa Dortmund wakitaka kulianzisha gozi baada ya kufungwa huku Maiko Reus akilia upande wa kushoto.

Na Caunter Mgaya Jr.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni