Tunisia
inakabiliwa na adhabu ya kufungiwa kushiriki michuano ijayo ya Kombe la
mataifa Afrika baada ya kukaidi kuomba radhi kwa kosa la kushutumu
shirikisho la soka Afrika CAF kujihusisha na vitendo vya udanganyifu.
Tunisia
ilitoa madai hayo baada ya Mchezo wa robo fainali walipokutana na
wenyeji Guinea ya Ikweta, hasa baada ya mwamuzi kutoa Penalti katika
dakika za lala salama za mchezo huo ambapo mpaka kipyenga cha mwisho
kinapulizwa Tunisia ilikuwa imefungwa magoli 2-1.
Mwamuzi wa mchezo huo naye amefungiwa kwa miezi sita kwa kuchezesha vibaya mchezo huo.
Tunisia ilikua imepewa mpaka siku ya Alhamisi kuomba radhi vinginevyo adhabu ya kufungiwa michuano ya mwaka 2017 ingewakabili.
Baada
ya mkutano siku ya Jumatano, Shirikisho la Soka Tunisia ilikataa kuomba
radhi huku Msemaji wake akisema kuwa Timu yake haikutendewa haki na
Waamuzi wa mchezo.
Caf,iliyowapiga faini Tunisia baada ya
Wachezaji kumzonga na kumfanyia vurugu Mwamuzi Rajindraparsad Seechurn
baada ya kipyenga cha mwisho, ilitaka mabingwa hao wa mwaka 2004 kuomba
radhi baada ya kudai kuwa Shirikisho hilo na maafisa wake wana upendeleo
na hawana maadili vinginevyo wapeleke vigezo vya kuthibitisha madai
yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni