Jumapili, 25 Mei 2014

ANGLIKANI YAINGILIA KATI SUALA LA WATOTO

Muhashamu askofu Joseph Ng'hambi Mgomi wa kanisa la Anglikani mkoani Iringa, akizungumza na waumini katika hafla ya uzinduzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi na magumu.
 Mchungaji Joseph Mayala Mitinje - ambaye ni mkurugenzi wa Compassion Taifa, akizungumza katika hafla hiyo.
 Mchungaji Canon Emmanuel Chapote- mchungaji kiongozi wa kanisa kuu la kikristo Mfalme Anglikani- Iringa.
 Agnes Hota- Mkurugenzi mteule wa Compassion Tanzania, akiwa na Askofu Joseph Ng'ambi Mgomi.
 Miriam Elisha- mwezeshaji wa ushirika wenza kati ya shirika la Compassion Tanzania, akiwa na Cuthbert Mono, meneja wa miradi ya kanisa kupitia shirika la Compassion.
 Cuthbert Mono (kushoto), meneja wa miradi ya kanisa kupitia shirika la Compassion, akiwa na Elieshi Kisinza.
 Agnes Hota- Mkurugenzi mteule wa Compassion Tanzania,(kulia) akiwa na Elieshi Kisinza.
 Isabella Mwakabonga- kaimu mkurugenzi wa shughuli ya uzinduzi wa vyumba vya madarasa ya watoto wanaohudumiwa na shirika la Compassion, Mwakabonga ni afisa elimu taaluma - msingi Manispaa ya Iringa, akiwa na mmoja wa viongozi wa kanisa la Anglikani.
 Josephine Ndabagoye- mwenyekiti wa huduma ya watoto wa kanisa kuu la Kristo Mfalme- Anglikani, akiwa na mchungaji Canon Emmanuel Chapote- mchungaji kiongozi wa kanisa la Anglikani Iringa.
 Mchungaji Samwel Willium Masaba (Kulia) wa kanisa la Afrikan Inland la mshindi akiwa na mchungaji Canon Charles Chilongani- ambaye ni naibu mwenyekiti wa SINODI kanisa la anglikani Ruaha- Iringa.
  Baadhi ya viongozi, wazazi, walezi na waumini wa kanisa la Anglikani wakisikiliza jambo.
 Mchungaji Samuel Willium Masaba, wa kanisa la African Inland Tanzania, la mshindo mjini Iringa.
  Baadhi ya wazazi, walezi na waumini wa kanisa la Anglikani wakisikiliza jambo.
 Baadhi ya wazazi, walezi na waumini wa kanisa la Anglikani wakisikiliza jambo.


 Wakisikiliza jambo katika hafla ya uzinduzi wa vyumba vya madarasa.

 Baadhi ya Viongozi wa kanisa la Anglikani wakiwa katika picha ya pamoja.
 Cuthbert Mono akiwa na Elieshi Kisinza, meneja mradi wa Compassion.
 Baadhi ya viongozi wa kanisa la Anglikan wakisikiliza jambo.
Baadhi ya viongozi wa Compassion wakisikiliza jambo.


 Uzinduzi.
 Moja ya vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwa ajili ya watoto yatima na waishio katika mazingira magumu na hatarishi, jengo lililopo katika uwanja wa kanisa la Anglikan Iringa, hiyo ikiwa ni mpango wa kuwapatia fulsa ya elimu watoto hao wenye uhitaji.
 Vyumba vya madarasa ambavyo vitasaidia kuwapatia elimu watoto yatima na waishio katika mazingira magumu na hatarishi, jengo lililojengwa na shirika la Compassion Anglikani Iringa.
Vyumba vya madarasa.


<<<HABARI>>>
KUSHAMIRI kwa vitendo vya ukatili katika jamii, vikiwemo vitendo vya mauaji, ubakaji na ulawiti, kumelilazimu kanisa la Anglikan nchini kuingilia kati, kwa kuitaka serikali kuwabana kwa sheria kali wahusika wa vitendo hivyo.

Hayo yamezungumzwa na viongozi wa kanisa la Anglikani nchini, katika uzinduzi wa vyumba vya madarasa ya watoto wenye uhitaji wa huduma muhimu ikiwemo elimu, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa kanisa la Anglikani mjini Iringa.

Askofu Joseph Mgomi- wa kanisa la Anglikani mkoani Iringa amesema kanisa halitaona vibaya kupata lawama wakati likiwatetea watoto, kwani baadhi yao wanatendewa uovu, matukio ambayo yanaharibu mfumo mzima wa maisha ya waathirika hao.

Mchungaji Joseph Mayala Mitinje wa kanisa la Anglikan- ambaye ni mkurugenzi wa shirika la Compassion Taifa, amesema pasipo kuwekeza kwa watoto ni sawa na kazi bure, na hivyo Taifa kukosa watu imara hapo baadaye.

Mchungaji Mayala amesema katika kuhudumia watoto kumekuwa na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo watoto, ikiwemo ya mila potofu ambazo hazimsadii mtoto katika makuzi na mstakabari mzima wa maisha ya mtoto katika siku za usoni.

“Tunafahamu si mila zote zinapotosha, zipo mila zenye kujenga na zenye kuleta maadili, lakini zipo mila ambazo zinaharibu kabisa mstakabari wa maisha ya mtoto ya maisha hapo baadaye, kwani haiba ya mwanadamu inajengwa asilimia 15 chini ya umri wa mtoto wa miaka 6....halafu asilimia 15 zinakuja baada ya hapo, sasa kama huyu mtoto anafanyiwa ukatili haiba ya mtoto itakujaje!!,” Alisema.

Pia amesema suala la ubakaji, ulawiti, ukeketaji na watoto kuuawa na sehemu za viungo vyao kuchukuliwa ni vitu ambavyo visivyo stahili katika jamii, na vinapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

Amesema kupitia kanisa wanatumia neno litokalo katika biblia kuihamasisha jamii kubadili tabia na mwenendo mbaya ili iachane na mila na desturi potofu ambazo zinaiharibu jamii,na badala yake imrudie Mungu kupitia mafundisho yake.

 Amewataka viongozi wengine wa dini na serikali kutumia fulsa walizonazo kuipa elimu jamii, ili itambue masuala ya haki za watoto na kutetea kwa kuwa sehemu ya waumini na viongozi ambao wanaishi na watoto hao katika maeneo yao.

“Kupitia kanisa sasa, nakwa kutumia neno la Mungu, biblia ambayo ndiyo inawapa mamlaka yapo mafundishoi mazuroi ambayo yanaweza kuhamasisha jamii kubadilisha tabia na kumjua Mungu wa mkweli na kuacha mila na hila mbaya,” Alisema.

Naye Mchungaji Canon Emmanuel Chapote, - Mchungaji kiongozi wa kanisa la Anglikani mkoani Iringa, amesema serikali inapaswa kutumia jitihada za hali na mali kuyatokomeza matukio hayo ambayo yanawafanya watoto wajitenge na jamii.

Mchungaji Chapote amesema tatizo la watoto juu ya ubakaji na vitendo ambavyo vinawadhalilisha maisha yao, na kuwa wao kama kanisa wanalaani hali hiyo, kwani inawafanya watoto waishi maisha ambayo hayawapi utukufu kama wanadamu.

Chapote amesema matukio ya aina hiyo yanawafanya watoto waishi kwa kutokujiamini, kuwa na mashaka, kutokupata mahitaji yao muhimu kama watoto, huku akiiomba serikali ichukue jukumu la kuwatetea na kujipanga kama inavyofanya katika masual mbalimbali kama Chaguzi mbalimbali na kampeni.

Aidha amesema kutokana na matukio ya udharimu wanayofanyiwa watoto hao ,yanawakosesha amani na furaha ndani ya nchi yao kama walivyo watoto wengine wenye wazazi na walezi.

Elizabeth Magalu mwakirishi wa watoto wa shirika la Compassio mkoani Iringa, ameiomba serikali katika mchakato wa kuipata katiba mpya kuhakikisha zinatungwa sheria kali za kuwadhibiti wale wote wanaowafanyia ukatili watoto.

Elizabeth amesema baadhi ya watoto wamekuwa wakifanyiwa vitendo viovu, kama kubakwa, kulawitiwa, pamoja na vipigo visivyofaa, na wahusika wanaotenda ukatili huo wakiwa watu wazima.

Asilimia kubwa ya jamii imekuwa ikiwatenga watoto yatima, wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi, ambapo shirika la Compassion limebeba  jukumu hilo, huku mkoani Iringa shirika likiwahudumia watoto 3600, katika vituo 12.

Hata hivyo Serikali kupitia Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na watoto hivi karibuni imekiri kuwepo kwa tatizo hilo la vitendo vya ukatili kwa kiwango kikubwa, na kuwa imeandaa sera na mikakati mbalimbali ili kukabiliana na tatizo hilo, kwa madai kuwa Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuanzisha madawati  ya Jinsia 417 ambayo yanatoa huduma kwa wanaofanyiwa ukatili.

MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni