Jumatatu, 26 Mei 2014

MAMA BAHATI FOUNDATION KUWAFIKIA WAJASIRIAMALI


 Japhet Makau - mkurugenzi mtendaji wa Mfuko wa Mama Bahati Foundation (MBF) akizungumza na viongozi wa vikundi.
  Japhet Makau - mkurugenzi mtendaji wa Mfuko wa Mama Bahati Foundation (MBF), akiwa katika ukumbi wa mkutano wa chuo kikuu huria Iringa katika mafunzo ya viongozi wa vikundi vya mfuko wa MBF.
  Askofu mkuu mstaafu wa Kanisa la Kianglikana Tanzania Donald Leo Mtetemela (Kushoto) ambaye ni mwanzirishi wa MBF akiwa na mkurugenzi mtendaji Japhet Makau, wakati wa mafunzo kwa viongozi wa vikundi vya MBF, mafunzo yaliyofanyika chuo kikuu huria Iringa.
  Askofu mkuu mstaafu wa Kanisa la Kianglikana Tanzania Donald Leo Mtetemela (Kushoto) akiwa na Marco Vingilah - ambaye ni mshauri wa Biashara na fedha, akifungua kwa Sala mafunzo ya  viongozi wa vikundi vya MBF, mafunzo yaliyofanyika chuo kikuu huria Iringa.
 Marco Vingilah - mshauri wa Biashara na fedha, mwezeshaji wa mafumnzo hayo akianza kazi hiyo kwa sala, iliyoongozwa na  Askofu mkuu mstaafu wa Kanisa la Kianglikana Tanzania Donald Leo Mtetemela.
 Mmoja wa viongozi wa MBF akitoa elimu kwa viongozi wa vikundi vya mfuko huo wa Mama Bahati Foundation.

Baadhi ya viongozi wa mfuko wa Mama Bahati Foundation wakimsikiliza mwezeshaji wa mada.

 Baadhi ya viongozi wa Center za mfuko wa Mama Bahati Foundation MBF wakimsikiliza mwezeshaji wa mada katika mafunzo ya viongozi wa mfuko huo.
  Bi. Anita Ndendya mwenyekiti wa Center ya Kitwiru akizungumza jambo katika mafunzo hayo ya kuwanoa viongozi wa vikundi vya mfuko wa MBF.
 Viongozi wa vikundi wakiwa katika ukumbi wa chuo kikuu huria Iringa, wakati mfuko huo wa Mama bahati Foundation ukiwapatia mafunzo.
 Bi. Anita Ndendya mwenyekiti wa Center ya Kitwiru akizungumza jambo katika mafunzo hayo ya kuwanoa viongozi wa vikundi vya mfuko wa MBF.
 Mmoja wa viongozi wa Mfuko wa Mama Bahati Foundation, akifuatilia jambo.
 Mareges Gilishoni mtangazaji wa kituo cha radio Ebony ya mjini Iringa akifurahia jambo katika mafunzo ya viongozi wa vikundi vya mfuko wa Mama Bahati Foundation.
 Wakifurahia jambo katika mafunzo hayo.
  Kalistus J. Lugenge afisa mikopo wa MBF akiwa katika ukumbi wa chuo kikuu huria Iringa, wakati mfuko huo wa Mama bahati Foundation ukiwanoa viongozi wake.
Baadhi ya viongozi wa Center za mfuko wa Mama Bahati Foundation wakimsikiliza mwezeshaji wa mada katika mafunzo ya viongozi wa mfuko wa MBF
 Baadhi ya viongozi wa Center za mfuko wa Mama Bahati Foundation wakimsikiliza mwezeshaji wa mada katika mafunzo ya viongozi wa mfuko wa MBF
  Baadhi ya viongozi wa Center za mfuko wa Mama Bahati Foundation wakimsikiliza mwezeshaji wa mada katika mafunzo ya viongozi wa mfuko wa MBF.
 Kulia ni Bi. Anita Ndendya mwenyekiti wa Center ya Kitwiru, kuwakirisha mfuko wa Mama Bahati Foundation, akisikiliza jambo katika semina ya viongozi.
  Kila mmoja yupo makini akifuatilia somo, katika ukumbi wa chuo kikuu huria, kilichopo mtaa wa Mama Titi Gangilonga mjini Iringa, ambapo viongozi wa Center ya mfuko wa Mama Bahati Foundation walipewa elimu ya kiuchumi.
  Baadhi ya viongozi wa Center ya mfuko wa Mama Bahati Foundation wakiwa makini katika darasa la kuwanoa kuendesha shughuli za kiuchumi.
  Baadhi ya viongozi wa Center ya mfuko wa Mama Bahati Foundation wakisikiliza somo.
  Baadhi ya viongozi wa Center ya mfuko wa Mama Bahati Foundation wakifurahia jambo kutoka kwa mwezeshaji wa mada.
 Baadhi ya viongozi wa Center ya mfuko wa Mama Bahati Foundation wakisikiliza somo.

Taasisi za kifedha jinazojihusisha na utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali nchini, zimetakiwa kuacha mfumo wa kuwakandamiza wanachama wake kwa riba kubwa, kwa madai kuwa  zinachangia kudumaza  shughuli za kiuchumumi na mstakabari wa maisha ya wateja wake.

Rai hiyo inatolewa na Japhet Makau-mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa Mama Bahati Foundation- BMF, katika mafunzo ya wanachama viongozi wa vikundi vya asas hiyo, yaliyofanyika katika chuo kikuu huria cha mjini Iringa.

Makau amesema taasisi za kifedha zisitegemee zaidi kujiendesha kwa riba za wanachama, kwani hatua hiyo itawafanya wateja kufirisika kwa kushindwa kurejesha mikopo, na kuishia kufirisiwa mali zao na kurejea katika hali ya umasikini.

Aidha amesema kukiwa na idadi kubwa ya wadau wa taasisi za kifedha na mabenki mbalimbali, mitaji yao ikiwa imekufa baada ya kushindwa kurejesha riba ya mkopo waliopangiwa na hivyo kufilisiwa mali zao.

Zaidi ya shilingi Bilioni 5 kwa wanawake wa Manispaa ya Iringa, Iringa vijijini na Wilaya ya Kilolo, na kuwa kusudio kubwa ni kuwainua wanawake na wajasiriamali wadogo, na mfuko huo si kutengeneza faida bali ni kuwawezesha wafanyabiashara wenye mitaji midogo.

Amesema wananchi wanapaswa kuwa makini na asas zenye lengo la kujiendesha kifaida, Mfumo unaotengenezwa kwa ajili ya utoaji mikopo ni sehemu kubwa ya kuonyesha namna walengwa watakavyonufaika au laa.

“Wito wangu kwa asas za kifedha (Microfinance Institutions) wanapofanya shughuli zao na wateja wao hao wadogo wadogo lengo kuu linapaswa liwe ni kuwasaidia masikini kwa kumtoa katika hali duni na kumuwezesha kuwa katika hali nzuri, tusiweke suala la faida mbele kwani ukiweka lengo la faida utamdidimiza masikini na kuwa masikini zaidi,” Alisema.

Amesema jumla ya akinamama elfu kumi wamefikiwa na mkopo huo wa Mama Bahati Foundation na kutokana na mfumo wa mfuko huo wote biashara zao ziko imara na wamejijenga kiuchumi, kutokana na riba ndogo za asas hiyo

Anita Ndendya mwenyekiti wa kituo (Centre) cha Kitwiru ambaye ni mmoja wa akinamama wanufaika wa mfuko huo amesema amefanikiwa kujenga nyumba ya vyumba saba na kuedesha biashara mbalimbali, kupitia mfuko huo wa Mama Bahati Foundation, huku akiwaasa akinamama kujishughulisha katika biashara ili kuongeza pato katika familia.

“Mimi hapa ni bimkubwa, nina miaka zaidi ya 70, lakini sibweteki ninafanya biashara mbalimbali, ninauza maandazi, bagia, ninaduka, kwa hiyo wanawake wasichague kazi, na wale wenye umri kama wangu wasikae bure kutegemea misaada ya watoto wao, tunatakiwa kujishughulisha,” Alisema Ndendya

Aidha aliwataka wanawake katika kuomba mikopo wawashirikishe waume zao ili kupata ushauri, kwani baadhi ya wanawake wamekuwa wakifanya siri katika mikopo jambo ambalo linawaletea shida katika familia pindi wanapopiga hatua au kushindwa.

“Wengine siku anayopata mkopo ndiyo wanatumia hela hiyo kwa kununua vitu, je ataweza kurudisha deni hilo..hapana, na wabi mkubwa tuungane tusibweteke, tufanye hata shughjuli za kilimo, na hata hizi ndogo ndogo kama kupika Maandazi, Vitumbua, Bagia na serikali itatuunga mkono,” alisema.

Pia amesema maono ya askofu Donald Mtetemela kwa kuanzisha mfuko huo wa Mama Bahati Foundation -(BMF) na kuwa mpango huo ni mwema kwani umewasaidia wanawake kupiga hatua katika maendeleo.

Hilaris Lihawa amewataka wanawake waache kubweteka majumbani kwa kutegemea fedha ya matumizi kutoka kwa waume zao, kwani jambo hilo litawafanya washindwe kujikwamua kiuchumi.

“Kwa mfano mimi ni mjane niliachwa na watoto, bahati nzuri nimeweza kusomesha watoto wangu, nilianza na mkopo wa shilingi elfu 50 lakini sasa nimefikia milioni 5, kupitia mkopo huu huu wa Mama Bahati, cha msingi ni kujituma zaidi,” Alisema.

Atilia Kihaga katibu wa kituo cha Mwembetogwa amesema baadhi ya wanawake wamekuwa wanashindwa kufanya biashara kwa kutegemea waume zao, na baadhi yao wakikopa wanaelekeza fedha hizo katika mambo yasiyo na maana na mwisho wa siku wanajikuta wakishindwa kurejesha mikopo walikokopa.

“Akinamama wengi wanahitaji mikopo, lakini mikopo hiyo haina faida kwao,  kwani wanachukua mikopo na wanakwenda kununua vitenge kama Wax, wakati mambo mengi ya kufanya yapo, sasa unakuta ni mtu wa madeni kila siku, anachukua mkopo huku anarudisha kule, mimi niwasihi tu wanawake wenzangu tuwe na malengo kwenye mikopo yetu na tuache tamaa ya kununua vitu, mimi mkopo wa mama Bahati umenisaidia sana kusomesha watoto, nina watoto watatu mwanangu mkubwa yupo mwaka wa  tatu kwa masomo ya Kompyuta Sayansi, na mtoto wa pili yupo Seminari Donbosco Mafinga… mimi mwenyewe tayari nimeanza shughuli ya ujenzi na nimefanya mambo mengi sana,” Alisema. 

Mwanzilishi wa BMF ni Askofu mkuu mstaafu Donald Leo Mtetemela ambaye alimsaidia fedha kiasi cha shilingi elfu 10 mjasiriamali mdogo aliyekuwa akitembeza ndizi mitaani, aliyefahamika kwa jina Diana Mbembela "mama Bahati", fedha iliyotolewa na askofu kwa mama huyo lengo likiwa ni kumuongezea mtaji mama Bahati ambaye kwa sasa ni marehemu.

Askofu Mtetemela aliona upo umuhimu wa kuendeleza mpango huo kwa akinamama ili kuwainua kiuchumi, baada ya kuona uaminifu mkubwa wa mama Bahati, kwani alikuwa akirejesha fedha hiyo kwa wakati na uaminifu mkubwa, hatua iliyomfanya askofu kumuongezea kiwango cha fedha hadi shilingi elfu 50.

BMF ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 2007 na asilimia 80 ya wanawake kutoka vijijini wamepatiwa mikopo, na asilimia kubwa wamekuwa waaminifu, wabunifu wa biashara huku wakiwa tayari kujifunza.
 
MWISHO.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni