Ijumaa, 23 Mei 2014

“CHAI BORA” YANG'ARISHA KOMBE LA MUUNGANO.

 Mkurugenzi wa kampuni ya Chai Bora Mufindi- Iringa Petronilla Alphonce akipeana mkono wa shukrani na  Lambardo Mvanda, mwakirishi wa timu ya Black Cheeter ya Iringa mjini- wakati timu zinashiriki Kombe la Muungano zilipopatiwa msaada huo wa jezi seti 6 na mipira kumi na kampuni ya Chai Bora.
  Mkurugenzi wa kampuni ya Chai Bora Mufindi- Iringa Petronilla Alphonce akipeana mkono wa shukrani na  Maulid Mwanyange, mwakirishi wa timu ya Mucoba Kids.
  Mkurugenzi wa kampuni ya Chai Bora Mufindi- Iringa Petronilla Alphonce akipeana mkono Mose Masas, mwakirishi wa timu ya Incomet VTC FC ya mjini Mafinga- wakati timu zinashiriki Kombe la Muungano zilipopatiwa msaada huo wa jezi seti 6 na mipira kumi na kampuni ya Chai Bora.
  Akipokea Mpira, jezi na soksi.
  Mwakirishi wa timu ya Mbeya City ya jijiji Mbeya- Dotto Sanga- akipokea jezi ya timu yake, mara tu baada ya timu zinashiriki Kombe la Muungano kupatiwa msaada huo wa jezi seti 6 na mipira kumi na kampuni ya Chai Bora.
  Soud Mlindwa mwakirishi wa timu ya Mbaspo Academy ya jijini Mbeya, timu iliyochukua ubingwa wa kombe hilo la Muungano, akipokea jezi na mpira kutoka kwa mkurugenzi wa Chai Bora Petronilla Alphonce.
  Soud Mlindwa mwakirishi wa timu ya Mbaspo Academy ya jijini Mbeya, timu iliyochukua ubingwa wa kombe hilo la Muungano, akipokea mpira kutoka kwa mkurugenzi wa Chai Bora Petronilla Alphonce.

 Shukuru Millinga - mwakirishi wa timu ya Zamaleck ya mjini Njombe, akipeana mikono ya shukrani mkurugenzi wa Chai Bora Petronilla Alphonce.
  "Ninashukuru sana" Ni kama anasema...Shukuru Millinga wa Zamaleck FC.
 Mratibu wa mshindano ya "Kombe la Muungano"  Daud Yasin, akizungumza na wawakirishi wa vilabu shiriki, mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo- Jezi seti 6 na mipira 10.
  Wawakirishi wa timu zinazoshiriki kombe la Muungano, wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chai Bora, pamoja na mratibu wa mashindano hayo Daud Yasin.

Wakiwa katika  Picha ya pamoja.
 Jane Ndosa- mhasibu wa kampuni ya Chai Bora, akiwa na Dotto Sanga, mwakirishi wa timu ya Mbeya City, mara baada ya timu shiriki kupatiwa misaada na kampuni ya Chai Bora ya Mufindi- Mafinga mkoani Iringa.
 Kulia ni Moses Masasi wa timu ya Incomet VTC FC akiwa na mwakirishi mwenzie katika uwanja wa kiwanda cha Chai Bora.
 Moulid Mwanyange (Kushoto) mwakirishi wa Mucoba Kids, akiwa na Soud Mlindwa mwakirishi wa timu ya Mbaspo Academy ya jijini Mbeya.
 Moulid Mwanyange (Kushoto) mwakirishi wa Mucoba Kids, akiwa na Soud Mlindwa mwakirishi wa timu ya Mbaspo Academy ya jijini Mbeya.
 Francis Mlowe mwakirishi wa timu ya Igowole Fc (wa kulia) ya Wilayani Mufindi, akiwa na Lambardo Mvanda wa timu ya Black Cheeter ya mjini Iringa.

 Kulia ni shukuru Millinga na Francis Mlowe.

 Maboksi ya  Chai Bora, majani ambayo yalitolewa kwa timu shiriki za kombe la Muungano, hiyo ikiwa ni hamasa kwa wachezaji kutumia kinywaji cha Chai na kuepuka vinywaji vyenye kileo.

 Wakisikiliza jambo.
 Bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni ya Chai Bora.
 Bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni ya Chai Bora.

 Mkurugenzi wa kampuni ya Chai Bora Mufindi- Iringa Petronilla Alphonceakizungumza jambo na wawakirishi wa timu zinazoshiriki kombe la Muungano.
 Aloyce Mnoga  mwakirishi wa Incomet VTC FC akiwa na Francis Mlowe wa Igowole FC wakisikiliza ujumbe kwa makini kutoka kwa mkurugenzi wa Chai Bora- Petronila alphonce(hayupo pichani).
 Jane Ndosa mhasibu wa kampuni ya Chai Bora akiwa na Lambardo Mvanda, wakifuatilia jambo katika hafla hiyo ya kukabidhiwa vifaa vya michezo.




<<<HABARI>>>
KOMBE la Muungano “Muungano Cup” ambalo limeanza kutimua vumbi katika uwanja wa Igowole  katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa limepigwa jeki na kampuni ya  Chai Bora, kwa kupatiwa msaada wa jezi seti 6 pamoja na mipira 10 kwa ajili ya kuboresha mashindano hayo.

Akikabidhi jezi na mipira hiyo kwa mratibu wa mashindano hayo ya kombe la Muungano- Daud Yasin, mkurugenzi wa kampuni ya Chai Bora Petronilla Alphonce, amesema lengo la msaada huo ni kuyafanya mashindano hayo kuwa na muonekano wa pekee, shughuli iliyofanyika katika uwanja wa Chai Bora mjini Mafinga,.

Petronida amesema vijana hao wanapaswa kujituma katika michezo ili kuonyesha vipaji  na uwezo nyanda za juu kusini, ikiwa pamoja na kutotumia vinywaji vyenye kileo ili kuwafanya wawe na nguvu imara.

Aidha amesema misaada hiyo imegharimu jumla ya shilingi Milioni 7.7  na kuwa kampuni kwa kutambua hilo imetoa msaada huo kwa wachezaji wote, na mchango huo ni katika kuunga mkono mashindano hayo kwa kuiwakirisha kampuni kwa kiwango cha hali ya juu.

“Kampuni kwa kuthamini michezo imeona ni vema itoe jezi seti 6 na mipira kumi, vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni 7.7,  .. mchango huu tulioutoa tunajua una manufaa na utatuletea ushindi mkubwa, niwawaombeni pia vijana mtumie Chai kwani ina manufaa sana kwenye mwili wa binadamu kwani  inachangamsha na inaburudisha, ” Alisema Petronilla.

Akipokea msaada huo- mratibu wa mashindano hayo ya Kombe la Muungano Daud Yasin amesema kampuni ya Chai Bora tangu mwaka  1998  imekuwa ikichangia kwa hali na mali sekta ya michezo mkoani Iringa, na kuwa ni Kampuni ya  kwanza kuyadhamini mashindano ya kombe la Muungano kwa miaka yote.

Amewataka wachezaji kuthamini vifaa hivyo kwa ubora wake kwani vina ubora wa hali ya juu, na kuwa matumaini yake ni vilabu shiriki kufanya vyema ili kuitangaza kampuni hiyo kupitia michuano hiyo inayozishirikisha timu za mikoa ya nyanda za juu kusini.

Amesema mashindano hayo ambayo yamezinduliwa Mei 24 katika uwanja wa shule ya msingi Igowole ambapo mashindano hayo yataendeshwa katika viwanja viwili,  kwa maana ya kiwanja cha wambi cha mjini Mafinga na kiwanja Igowole shule ya msingi,

Uwanja wa Igowole utachezewa na timu ya Mbeya city ya jijini Mbeya, Zamalek na timu ya Igowole   sekondari,  huku mjini Mafinga katika uwanja wa Wambi kutakuwa na mechi ya timu ya Benk ya wananchi Mucoba, timu ya chuo cha Incoment na timu ya Black Cheeter ya mjini Iringa.

Amesema timu ya Mbaspo ambayo ni mabingwa watetezi waliochukua kombe la Muungano mwaka 2013 wamepewa fulsa ya kuingia moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali, ambapo amewataka wapenzi wa soka na mashabiki kujitokeza kwa wingi kuangalia vipaji vya vijana wa nyanda za juu kusini.

Hata hivyo amesema mashindano hayo yamekuwa na msisimko kwa kuwa yanahusisha vijana walio na umri chini ya miaka 20, huku akiwataka wapenzi na mashabiki wa nyanda za juu kusini, kujitokeza kwa wingi kutazama vipaji vya vijana wa nyanda za juu kusini.

Daud Yasini amesema kwa mwaka huu  niwa mwisho kwake kuratibu mashindano ya kombe la Muungano kwani anastaafu na kuwa bingwa atachukua Kombe hilo moja kwa moja, kama ni kumbukumbu kwa timu ya uratibu wake wa mashindano hayo.

Hata hivyo yasin amesema mashindano hayo yatakamilika  june 11, ambapo fainali ya kombe hilo mchezo wake utakachezwa katika uwanja wa Wambi wa mjini Mafinga.

Nao wawakirishi wameonyesha tambo zao huku kila mmoja akijikweza kulichukua kombe hilo, huku wakiwaomba wadau kuchangia michezo mbalimbali hasa ya soko ambayo imekuwa na mvuto kwa kundi kubwa katika jamii. 

 MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni