WATANGAZAJI na
wanahabari wa kituo cha radio cha Ebonby Fm, cha Iringa, kituo kinachorusha
matangazo yake katika mikoa zaidi ya sita nchini, wamesherekea kutimiza miaka 8
ya uwepo wa redio hiyo hewani.
Hafla hiyo iliyofanyika
katika Club ya La- Part ukumbi wa burudani wa kisasa uliopo eneo la Gangilonga, manispaa ya mji wa Iringa.
Sherehe hiyo ilikuwa ya
aina yake, huku watangazaji, wanahabari, na wafanyanyakazi wa kada mbalimbali
pamoja na baadhi ya wadau wa redio hiyo.
Sherehe hiyo iliyokuwa chini
ya mshereheshaji MC Bonny Zakaria Nyatoka “Bonny Slay” ambaye ndiye alikuwa
mratibu wa sherehe, pia ilishereheshwa na “Sogg Dog Hanter” maarufu kwa jina la
Kibanda cha Simu ambaye aliipamba sherehe hiyo kwa rafudhi ya Kichaga.
Baadhi ya wafanyakazi wa
kike waliong’ara kwa mavazi yenye nakshi zenye mvuto na zinazokwenda na wakati
ni Neema Msafiri, Aisha Sandiga, Glory Pelle, Gracy Mwabulesi, Tinna a.k.a “Tinatinna”
Bertha Denis, Kabulah, Farida Ismail nk.
Kwa upande wa baadhi ya
watumishi wa kiume ni Austine Nyondo, Reymond Chali, Eddo Bashiri, Abery
Mponela, Dr. Joh, DJ Kwasa, na mdau ninayemkumbuka Danny Manjiwa, ambapo katika
sherehe hiyo kuliluwa na vinywaji vya kila aina.
Uzuri wa sherehe
walisema waswahili ni Chakula na vinywaji, sherehe hii ilikuwa na vyakula na
vinywaji ambavyo wanywaji na walaji, mabibi na mabwana walikula na kusaza, huku
wakijisuuza kwa muziki na disco la nguvu, lakukata na shoka”.
Kila La Kheri miaka
8000 Ebony fm na maisha marefu yenye Baraka kuifikia mikoa yote ya TANZANIA,
ili kutimiza lengo la Kuhabarisha, Kuelimisha, Kuburudisha – Kufundisha na
Kuonya, kwa kuwatoa watu Polini na kuwasogeza Barabarani.
MWISHO
.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni