Alhamisi, 19 Juni 2014

"LION CLUB" YAWAOKOA WANANCHI ISIMANI




Uzinduzi wa mradi wa maji ya kuvutwa kwa nishati ya umeme wa jua- Soral.


Bw. Lion Karim Mitta wa kwanza kushoto akiwa na rais anayemaliza muda wake Bi. Nureen Nathoo katika siku ya uzinduzi wa mradi wa maji yanayovutwa kwa kutumia nishati ya umeme wa jua, katika kijiji cha mawindi.
 Bi. Shyrose Mitta, mke wa Lion Karim Mitta wa kwanza kushoto wakiwa katika siku ya uzinduzi wa mradi wa maji yanayovutwa kwa kutumia nishati ya umeme wa jua, katika kijiji cha mawindi.
 Naye waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uratibu wa bunge na sera Willium Lukuvi- akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mawindi katika uzinduzi wa mradi wa maji yanayovutwa kwa kutumia nishati ya umeme wa jua, katika kijiji cha mawindi.
 Baadhi ya wananchi wakisikiliza jambo kutoka kwa viongozi wa Lion Club waliofika katika uzinduzi wa mradi wa maji yanayovutwa kwa kutumia nishati ya umeme wa jua, katika kijiji cha mawindi.
 Baadhi ya wananchi wakisikiliza jambo kutoka kwa viongozi wa Lion Club waliofika katika uzinduzi wa mradi wa maji yanayovutwa kwa kutumia nishati ya umeme wa jua, katika kijiji cha mawindi.
 Mzee wa kabila la wahehe akisikiliza jambo kutoka kwa viongozi wa Lion Club waliofika katika uzinduzi wa mradi wa maji yanayovutwa kwa kutumia nishati ya umeme wa jua, katika kijiji cha mawindi.
 Lion Mathew Alex -rais mtarajiwa anayetaraji kuanza kazi Lion Club, akiwa katika uzinduzi huo.


Bi. Nureen Nathoo wa kwanza kulia akiwa na Lion Karim Mitta wakishuhudia upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa kijiji cha mawindi kilichopo Kata ya Nyang'olo katika Tarafa ya isimani Wilayani Iringa.
<<<HABARI>>>

WANANCHI wa kijiji cha Mawindi tarafa ya Isimani mkoani Iringa wameepukana na adha ya shida ya huduma ya maji iliyowafanya watembee umbali wa zaidi ya km 10 kuifuata na kusababisha hali ya  uchumi na maendeleo kudumaa.

Hatua hiyo umeilazimu mradi wa Lion Club host ya jijini Dar es salaam kuingilia kati, kupitia Waziri  wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge  Willium Lukuvi, ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo la Isimani.

Lion Club imejenga kisima cha maji kinachotumia nishati ya Umeme wa jua "Solar" katika kijiji cha Mawindi kilichopo Kata ya Nyang'olo tarafa ya Isimani, na hiyo nikutokana na jografia ya eneo hilo kuwa Kame.

Akizungumzia hali hiyo Waziri Lukuvi amesema imemlazimu kutumia kiwango kikubwa kubaini uwepo wa maji katika kijiji hicho cha Mawindi.

Lukuvi amesema shida kubwa katika tarafa ya Isimani ni kero ya upatikanaji mgumu wa huduma ya maji, na kuwa sasa tayari amechimba visima 25 katika tarafa hiyo ili kupunguza adha kwa wananchi.

Aidha amesema hali hiyo inatokana na vijiji vya kata ya Nyang'olo  kutopitiwa na mto wala bwawa-na hivyo ardhi yake kuwa kame na kushindwa kuwa na asili ya maji.

Lion Karim Mitta mmoja wa viongozi wa Lion Club amesema kupitia Waziri Lukuvi alibaini changamoto kubwa ya maji kwa wananchi wa Mawindi.

Karim Mitta amesema kuHayo yamezungumzwa na muhandisi wa maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Lukas Madaha wakati Waziri wa katiba na sheria Willium Lukuvi wakati akikabidhi mradi wa maji unaotumia nishati ya jua (Soral).

Lion Mathew Alex rais anayetaraji kuchukua nafasi ya urais wa "Lion Club" amewataka watanzania kujiunga katika Club hiyo na kuondokana na fikra ya kudhani kuwa kikundi hicho nikwa ajili ya jamii ya watu wa Kihindu "Wahindi".

Naye rais anayemaliza muda wake wa  "Lion Club" bi- Nureen Nathoo amesema msaada huo ni mfano, na wapo Lion ipo tayari kuwasaidia wananchi wa vijijini ambao wanakabiliwa na changamoto ya huduma ya maji na huduma ya afya.

"Tunatoa huduma mbalimbali kama ya afya, tumekuwa tukiwasaidia wagonjwa wa Moyo, lakini hili la maji kwa njia ya nishati ya umeme wa jua ni huduma ya mfano na tupo tayari kuwasaidia pia wananchi wa vijiji mbalimbali vya Isimani kupitia rafiki yetu waziri Lukuvi," Alisema Nureen. 

Upendo Tewele na Zamda Issah niwakazi wa kijiji cha Mawindi wamesema tatizo la uhaba wa maji katika kijiji chao - umesababisha shughuli za maendeleo kukwama, huku baadhi ya akinamama wakipata adha ya kuachwa na wenza wao.

Upendo amesema walikuwa na mpango wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa nyumba za walimu, lakini wamekwama kufikia lengo hilo kutokana na kero ya upatikanaji wa maji.

Wamesema hulazimika kutembea umbali wa zaidi ya km 10 kufuata maji katika kijiji cha Msosa, ambapo hujidamka usiku wa manane na kurejea na ndoo za maji nyumbani saa nane mchana jambo ambalo linadumaza hata kufanyika kwa shughuli nyingine.

Wamesema baadhi ya akinamama wajawazito wanaojituma kutafuta maji, wamekuwa wakijifungulia njiani, jambo ambalo lilikuwa hatari zaidi kwa usalama wa maisha yao na watoto wao, na kuwa ujio wa mradi huo ni ukombozi mkubwa kwao na salama ya kuvunjika kwa ndoa zao.

Muhandisi wa maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Lukas Madaha amesema wananchi wa kijiji  hicho cha Mawindi wanakabiliwa na  changamoto kubwa ya maji na kuwa Mawindi ni kati ya vijiji zaidi ya 100 ambavyo vilikuwa na adha ya upatikanaji mgumu wa huduma hiyo muhimu.

Madaha amesema hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya iringa ni wastani wa asilimia 68,  huku huduma hiyo ya maji ikipatikana kwa njia ya miradi ya maji ya bomba, Visima virefu, miradi ya maji ya visima vifupi, miradi ya maji inayotumia Pampu za injini za mafuta na umeme.

Hata hivyo Madaha ameiomba Lion Club iendelee kutoa ufadhili kwa vijiji vingine vyenye shida ya maji vilivyopo katika  Halmashauri hiyo kwa kuwa tatizo bado ni kubwa.

Naye waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uratibu wa bunge na sera Willium Lukuvi amesema mradi huo wa maji unaotumia nishati ya umeme wa jua umefadhiliwa na Lion Club Host ya jijini Dar es Salaam na lengo ni kupunguza changamoto zinazowakabiri wananchi wa jimbo lake.

Lukuvi amesema kwa ushawishi wake kama mbunge wa jimbo hilo la Isimani amewaomba Lion Club kuchimba visima 25 katika tarafa ya Isimani ambayo ina hali ngumu ya upatikanaji wa huduma ya maji.

MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni