Alhamisi, 17 Julai 2014

JWT KUWABANA WAFANYABIASHARA WANAOKWEPA KULIPA KODI


 Baadhi ya wafanyabiashara wa Iringa wakisikiliza jambo katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Hinghland mjini Iringa.
 Baadhi ya wafanyabiashara wa Iringa wakiwa katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Hinghland mjini Iringa.
 Baadhi ya wafanyabiashara wa Iringa wakiwa katika ukumbi wa Hinghland mjini Iringa, wakiwa katika mkutano wa kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabiri.

  Baadhi ya wafanyabiashara wa Iringa wakiwa katika ukumbi wa Hinghland mjini Iringa, wakiwa katika mkutano wa kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabiri.
 Mwenyekiti wa  jumiya ya wafanyabiashara JWT - Odilo Ngamilaga akifanyiwa mahojiano na mtandao huu - juu ya dhamira ya kuwakutanisha wafanyabiashara wa mkoa wa Iringa siku ya mkutano huo.
 Mwenyekiti wa  jumiya ya wafanyabiashara JWT - Odilo Ngamilaga akifanyiwa mahojiano na mtandao huu - juu ya dhamira ya kuwakutanisha wafanyabiashara wa mkoa wa Iringa siku ya mkutano huo.
 KATIBU wa  jumiya ya wafanyabiashara JWT - Jackson Kalole akitoa ufafanuzi wa dhamira ya wafanyabiashara na mfumo wa ulipaji wa kodi nchini.
  
  Mchungaji Silver Kiondo ambaye ni mwenyekiti wa chama jumuiya ya wafanyabiashara mkoani Dodoma akizungumza na wafanyabiashara mkoani Iringa.
 Baadhi ya viongozi wa  jumiya ya wafanyabiashara JWT - kulia ni Edward Materu akiwa na Jackson Materu wakisikiliza jambo katika mkutano huo.
 Mchungaji Silver Kiondo ambaye ni mwenyekiti wa chama jumuiya ya wafanyabiashara mkoani Dodoma akizungumza na wafanyabiashara mkoani Iringa.
Baadhi ya viongozi wa  jumiya ya wafanyabiashara JWT - kulia ni Edward Materu akiwa na Jackson Materu wakisikiliza jambo katika mkutano huo.
 KATIBU wa  jumiya ya wafanyabiashara JWT - Jackson Kalole akisikiliza jambo katika mkutano huo.
 Mtunza hazina wa  jumiya ya wafanyabiashara JWT - Edward Materu akisikiliza jambo katika mkutano huo.

 Mtunza hazina wa  jumiya ya wafanyabiashara JWT - Edward Materu akisikiliza jambo katika mkutano huo.

<<<HABARI>>>

JUMUIYA ya wafanyabiashara Tanzania ( JWT)  imesema inaandaa mkakati wa kuwabana   wafanyabiasahara wakubwa wote wanaokwepa kodi na kuisababishia serikali hasara ambayo inafidiwa na wafanyabiashara wadogo kwa kurundikiwa mzigo huo wa ulipaji wa kodi- na kuwa huo utakuwa mwarobaini wa kutibu changamoto hiyo ya ukwepaji kodi.


Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa kamati kuu ya Taifa ya jumuiya ya wafanyabiasahara – Jackson Kalole- ambaye pia ni Katibu wa jumuiya ya wafanyabiasahara mkoa wa Iringa – katika mkutano mkuu wa wafanyabiasahara Hinghland mjini Iringa, mkutano uliohudhuriwa na zaidi ya wafanyabiashara 200 mkoani humo.

Kalole amesema endapo mfumo na sheria za kodi zitaboreshwa,  pamoja na kuwepo kwa uwazi – hakuna mfanyabiashara yoyote atakayekataa kulipa kodi, kwa  kununua na kutumia mashine za kielektroniki EFD, kwa kuwa hali iliyopo sasa inatokana na mzigo mkubwa anaobebeshwa mfanyabiashara mdogo pekee.


Naye mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya wafanyabiasahara mkoa wa Iringa Odilo Ngamilaga- akitaja sababu za awali kufunga maduka ilikuwa ni kufikisha ujumbe kwa serikali, kwani wafanyabiashara wake hawapingi kodi bali wanahitaji marekebisho ili shughuli zao ziwe na tija- na sasa hawaoni sababu ya kufunga maduka tena.

Hata hivyo mchungaji Silver Kiondo ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara – mkoani Dodoma amesema hatua ya wao kuhusika katika ukusanyaji wa kodi, utafanana na Polisi jamii,  na hapo hakuna atakayekwepa tena sheria za kodi, kwani wao ndiyo watahusika katika ukusanyaji huo na lengo likiwa ni kuongeza mapato ya kodi serikalini.

Awali wafanyabiasahara mkoa wa Iringa wakiungana na mikoa mingine- waligoma kufungua maduka na hivyo kusitisha utoaji wa huduma mbalimbali kwa muda wa siku tatu- wakilalamikia mfumo wa ulipaji wa kodi kuwa ni kandamizi .

KATIKA NUKUU YA TAARIFA YAO.

Ndugu wafanyabiashara wa Iringa ikumbukwe kwamba mwaka  huu 2014 kulitokea mgomo mkubwa wa wafanyabiashara wote Tanzania ukiwemo na mkoa wetu wa Iringa.

Mgomo huo ulipelekea kufunga maduka yote kwa madai ya Mashine za EFD's ambazo mamlaka ya mapato Tanzania TRA walitoa agizo la kununua mashine hizo kwa wafanyabiashara wa awamu ya pili kwa maana ya "Fase two".

Mashine hizo zilipelekea kutokea kwa mgomo mkubwa wa Kihistoria ambao hjaujawahi kutokea - Iringa tangu nchi hii ipate Uhuru.

SABABU ZA MGOMO.

Ndugu wafanyabiashara ieleweke kwamba sababu kuu zilizosababisha wafanyabiashara kugoma ni mfumo ambao ni mgumu kwa upande wa wafanyabiashara na si rafiki mwema pia kwa mfanyabiashara.

Hali iyo ilipelekea mkuu wa mkoa wa Iringa kuingilia kati mgomo huo, ambao uliwaathiri wananchi wengikwa kukosa huduma kutokana na mgomo huo.

Wafanyabiashara walipewa fulsa ya kutoa maoni yaliyosababisha wao mpaka wakafunga huduma zao, ambapo kati ya michango yote malalamiko makubwa yalikuwa ni kwamba kwa muda mrefu wamekuwa wakinyanyaswa na kulazimishwa na TRA kuzinunua mashine hizo ambazo kimsingi wafanyabiashara waliuona kwamba mfumo huo utawagharimu mitaji yao.

Walisema mfumo huo unasababisha wafanyabiasahara wengi kushindwa kuendelea na biashara kutokana na mitaji yao kuwa midogo na sheria zikiwalazimisha kununua mashine hizo bila kuangalia kiwango cha mtaji wa mfanyabiashara.

Kutokana na sheria inayotutaka wafanyabiashara wenye mauzo ya  shilingi Milioni 14 kwa mwaka hadi shilingi Milioni 40 ni lazima anunue mashine hiyo.

MAONI YA WAFANYABIASHARA.

Baadhi ya maoni ya wafanyabiashara yalisema pamoja na changamoto za kodi kutoka serikali kuubado mfanyabiashara huyu ana mzigo mzito wa kodi zilizo ndani ya halmashauri ambazo nazo kodi nyingine zilionekana kero kwani zilimuongezea mfanyabiashara mzigo mkubwa.

Baadhi ya maoni yalipendekeza kuwepo uongozi wa wafanyabiashara ambao utashughulikia masuala ya wafanyabiashara  moja kwa moja.

Sasa basi.. baada ya maoni hayo tulichagua uongozi wa mpito ambao umekuwa ukisimamia na kuendesha shughuli hii mpaka hapa tulipofikia.

VIONGOZI.
Mwenyekiti- Odilo Ngamilaga
Makamu Mwenyekiti- Peter Mtalo
Katibu- Jackson Kalole
Makamu katibu- Cola Benitho.
Mweka Hazina- Edward Materu.

JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA TANZANIA- JWT.

JWT- Iliainisha masuala mbalimbali yahusuyo mfumo mzima wa utozaji wa kodi pamoja na changamoto zinazosababisha mfumo kuwa mgumu kiutekelezaji, na baadhi ya changamoto hizo ni-:

1. Sheria ya VAT- value added tax kuwa na sheria nyingi kandamizi, kama faini kuwa kubwa tofauti na muundo wa kosa lenyewe.

2. Bidhaa moja kutozwa VAT zaidi ya mara moja.

3. Kiwango cha usajili wa VAT kwa mfanyabiashara ambacho kilikuwa ni mauzo ya sh. Milioni 40 yaani mauzo ghafi na kupendekeza kiwango kicho kwani kimepitwa na wakati kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi tangu sheria hiyo ilipotungwa.

Kuzitambua gharama zisizo na lisiti kwa mfanyabiashara, kwa mfano ubebaji wa mizigo, usafirishaji, chakula kwa mama ntilie na maeneo mengine ambayo sijayataja yanayoendana na hayo, kwamba yaingizwe kwenye mahesabu.

5. Kutozwa kodi kutokana na faidi, tofauti na hali ya sasa inayozingatia muundo wa mauzo ghafi.

NINI TULIFANYA.
Ndugu wafanyabiashara ...tulichokifanya ni kuitisha mkutano wa dharura kupitia JWK na JWT ili tupate baraka kutoka kwa waliotutuma, ili kama watakubaliana au laa, ieleweke kwamba sisi viongozi hutuzuii mashine za EFD's kuuzwa isipokuwa wananchi waliotutuma wanataka maboresho kwanza halafu ndipo mashine hizo zitumike.

Ndugu wanaIringa, msimamo wa wafanyabiashara wote wa Dar es salaam kwamba hawapo tayari kununua mashine katika mfumo unaolalamikiwa ila mfumo huu uboreshwe ili zitumike kwa maslahi ya wafanyabiashara nakwa maslahi ya Taifa letu la Tanzania.  

Kwa hiyo huu ndiyo msimamo wa wenzetu, je!! ninyi wana iringa mnasemaje juu ya hili?? 
Baada ya kusema haya ninawashukuru kwa usikivu wenu.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki JWT
Mungu uwabariki wafanyabiashara wote
Ahsanteni sana!!
MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni