Jumapili, 13 Julai 2014

VIONGOZI WA DINI WAMTAKA SITTA KUWA MKWELI


 Viongozi wa kanisa la Pendekoste wakiwa katika moja ya mkutano mjini Iringa.
Sheikh Omary Nzowa- mdhamini wa Baraza la waislamu Tanzania BAKWATA, akizungumza na mtandao huu katika ofisi za blog hii mjini Iringa.
Mchungaji Elias Mbagata- Katibu wa umoja wa Makanisa la Pentekoste na mratibu wa huduma ya Go and Tell, akiwa katika moja ya mikutano yake ya awali kama ni maandalizi ya mkutano mkuu utakaofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Wilolesi mjini Iringa.
 Laurens Lagerwerf- mratibu wa Go and Tell ya kanisa la Pentekoste, akiwa katika mkutano mkoani Iringa.
Mchungaji Emmanuel D. Kanemba mwenyekiti wa maandalizi ya mkutano mkuu wa Go and Tell, akizungumza na mtandao huu katika moja ya mikutano yao ya maandalizi ya mkutano mkuu- mkoani Iringa.
  Mchungaji Elias Mbagata- Katibu wa umoja wa Makanisa la Pentekoste na mratibu wa huduma ya Go and Tell, akiwa katika moja ya mikutano yake ya awali kama ni maandalizi ya mkutano mkuu utakaofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Wilolesi mjini Iringa.
 Viongozi wa kanisa la Pendekoste wakiwa katika moja ya mkutano mjini Iringa.  
 Sheikh Omary Nzowa- mdhamini wa Baraza la waislamu Tanzania BAKWATA, akizungumza na mtandao huu katika ofisi za blog hii mjini Iringa.
 

 
<<<HABARI>>>

ZIKIWA zimepita siku kadhaa tangu mwenyekiti wa bunge maalumu la Katiba BMK- Samwel Sitta kutangaza kuwa ameteua Masheikh na Maaskofu ili kuwarejesha UKAWA Bungeni, viongozi hao wa dini wamemtaka Sitta kuwa mkweli, muwazi na mwenye dhamira ya dhati  katika kumaliza mpasuko wa bunge lake la katiba.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti- katika mahojiano na Blog hii- Viongozi hao wa dini wamesema hatua ya Sitta kuuona umuhimu wa kutafutwa suluhu kwa kuwashirikisha wao viongozi wa dini , ni jambo la busara na sahihi ambalo litaweza kuzaa matunda, endapo tu kiongozi huyo wa serikali Samwel Sitta atafuata kanuni na taratibu zote zinazopaswa katika kufikia muafaka wa jambo hilo.

Mchungaji Elias Mbagata ambaye ni katibu wa umoja wa makanisa ya Pentekoste na mratibu wa huduma ya Go and Tell, ametoa ushauri juu ya wazo hilo la wao viongozi wa dini kuhusishwa kuitafuta suluhu ya mtafaruku wa wajumbe wa bunge maalumu la katiba na kuwa wenye tatizo si UKAWA pekee, bali hata wale wajumbe wengine kuna haja ya kukaa nao kwa pamoja ili waache kauli za kuudhi.

Mchungaji Mbagata amesema ili kumaliza mtafaruku huo kuna umuhimu wajumbe wote wakahusishwa katika makatazo yatakayo lenga kupatikana kwa Katiba mpya ya Watanzania, na kuwa hakutakuwa na mafanikio endapo UKAWA pekee ndiyo wakakutana na viongozi hao wa dini.

“Si UKAWA pekee inapaswa wahusishwe  na wajumbe wengine wote wa bunge hilo la Katiba- tunajua katika nchi kama hakuna Katiba hakuna Amani, sisi kama viongozi wa dini pamoja na kuomba tunalazimika kuwasihi wanasiasa kutotanguliza maslahi yao binafsi, kwani  siasa ni muhimu - lakini watanzania ni muhimu zaidi ya siasa, yale tuliyoyaona katika bunge la katiba lililopita hatukuyatarajia, kwani badala ya kupafanya mahala pale sehemu ya kujadiliana na kukubaliana pakageuka ni mahali pa-kulumbana na kushindana, na tunafahamu kuwa kadri watu wanavyolumbana wanachochea hasira,” Alisema Mchungaji Mbagata.

Akinukuu baadhi ya vifungu vya biblia mchungaji Mbagata amesemakatika kitabu cha Mithali 15: 1 unasema Jawabu la upole hugeuza hasira bali neno liumizalo huchochea ghadhabu- … tunamshukuru sana rais Kikwete kwa hekima aliyonayo nakwa busara nakwa mwongozo alioutumia kuteua wajumbe wakujadili mchakato wa katiba mpya– ni jambo zuri sana, lakini yale tuliyoyaona katika bunge lililopita wengi  yalituumiza sana mioyo- cha msingi wale wote waliopewa dhamana hiyo na Rais ya kujadili mchakato wa Katiba mpya wakubali kuwa pamoja,  wawe ni UKAWA au wajumbe wengine wazungumze kwa upole nasi kwa hasira, hapo hawatafikia muafaka, kwani wasipofikia muafaka amani itavunjika, “Alisema mchungaji Mbagata.

Pia aliwataka wajumbe watambue kuwa wenye dhamana ya kuipigia kura rasimu hiyo kwa kuikubari au kuikataa ni wananchi na si wanasiasa ambao wanaendelea na malumbano, kwani sasa wote kwa pamoja wanapaswa kukubaliana ili kufikia muafaka wa kuipata Katiba mpya.

“UKAWA ni muhimu wakarudi bungeni lakini na hawa wengine wanapaswa  kuwa na Lugha ambazo haziwezi kuwaumiza wenzao ili pande zote mbili waweze kwenda pamoja, lakini hoja si kuongea na UKAWA peke yao wahusishwe pamoja na hao wengine,” Alisema mchungaji Mbagata.

Alimtaka rais asichoke, asikate tamaa kwa hekima na busara aliyonayo na badala yake atafute kila namna ili aweze kuwaita UKAWA waweze kukubaliana kwa kutumia nafasi aliyonayo kwa lengo la kunusuru mchakato mzima wa upatikanaji wa Katiba mpya.

Naye Sheikhe Omary Nzowa ambaye ni mdhamini wa baraza la Waislamu BAKWATA Taifa akirejea kauli ya Mwenyekiti wa bunge maalumu la Katiba Samwel Sitta – ya kutaka kuwaita  viongozi wa dini kukutana na kamati ya mashauriano july 24 - ili kusaidia suluhu ya utata na tofauti zilizopo- Nzowa amesema Samwel Sitta anatakiwa kuwa mkweli na muwazi ili suluhu ipatikane.

Sheikh Nzowa amemtaka mwenyekiti huyo wa Bunge Maalumu la Katiba BMK kuwa na dhamira ya kweli pasipo kuficha mambo ili kufikia muafaka wa mpasuko wa bunge lake, kwa madai kuwa ukweli ndiyo silaha ya muafaka katika tatizo hilo.

Aidha Sheikh Nzowa amesema mwenyekiti huyo anatambua wazi chanzo cha tatizo la UKAWA kuondoka bungeni, kwani kuna masuala ambayo yaliwakera wajumbe hao, na sasa ipo haja ya kutafuta suluhu kwa msaada wa Mungu kwani jambo hilo ni nito linastahili viongozi wa dini kuhusishwa.

Nzowa amesema kwa maoni yake anaona mwenyekiti huyo wa BMK ana dhamana kubwa kuona mtafaruku hautokei tena katika bunge lake, na kuwa wazo la Sitta linaweza kuleta suluhu, kwani inapotokea watu wawili wakazozani ni lazima akatokea mtu wa tatu mwenye nguvu ya kusikilizwa ili kutambua nani amekosea na kumaliza utata uliopo.


Amesema sababu kubwa ya viongozi wa dini kuwa na nguvu ya kumaliza tofauti ni kutokana na wanachama wote wa vyama vya siasa kuwa waumini wa dini- nakwa hali hiyo viongozi wa dini wanaweza kuwakutanisha na kufikia muafaka wa suala hilo, hasa suala la Ukweli likitangulizwa mbele.

“Matumaini yangu ni kuwa viongozi wa dini wanastahili na kama Samwel Sitta ameamua kwa nia thabiti kuwaita viongozi wa dini kwa maana ya kumsaidia kutatua mfarakano huo jambo hilo litafanikiwa, kwani viongozi wa dini wanazijua dhamana zao- lakini pia wanamuogopa Mwenyezi Mungu, matumaini yake mambo yatakwenda vizuri, lakini kama ukweli hautakuwepo hiyo ni kazi bure, kwani kwa ujanja ujanja haiwezi kupatikana suluhu kwani kwenye ukweli kuna msaada wa Mungu,” Alisema Nzowa.

“………Kwanza nimsihi mwenyekiti kuwa aliipata dhamana kubwa na anayo dhamana kubwa kwa Watanzania, na sisi viongozi wa dini tunapoona machafuko na mgongano tunajua nini kitatokea baadaye, nchi yetu hii ni nchi ya amani lakini ukitokea mfarakano mmoja wa watu watakaosononeka ni pamoja na mimi,” alisema.


Hata hivyo July 16 2014 Kanisa la Pentekoste nchini linataraji kufanya mkutano wa kuliombea Taifa ili liepukana na matukio mbalimbali yasiyo ya kawaida, – mkutano utakaofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Wilolesi mjini Iringa.
MWISHO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni