Alhamisi, 17 Julai 2014

NYALANDU ATAKIWA KUFUTA VIBALI VYOTE SAO HILL


 Moja ya eneo la shamba la miti la msitu wa Sao hill.
 
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa - Jesca Msambatavangu, akizungumzia suala hilo la Vibali.

 Katibu wa CCM - Wilaya ya Mufindi- Miraji Mtaturu, akiwa katika kikao hicho cha Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Iringa.



 Ally Simba mmoja wa wajumbe wa kikao cha Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Iringa akisikiliza jambo.
 Katibu msaidizi wa CCM Mkoa wa Iringa - Jimson Mhagama akiwa katika kikao hicho ambacho kimetoa maazimio juu ya Vibali vya shamba la miti la Taifa- la msitu wa Saohill.

 

Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi - Miraj Mtaturu- ndani ya kikao hicho.

<<<HABARI>>>

WAZIRI wa maliasili na utalii Razalo Nyalandu– ametakiwa kufuta  vibari vyote vilivyotolewa katika msimu huu, vya shamba la miti la Taifa la Sao hill, lililopo Wilayani Mufindi mkoani Iringa, kwa madai kuwa utaratibu wa utoaji wa vibari uliotumika niwa rushwa na uliojaa ufisadi,  kwani hata watu waliokufa wameorodheshwa kupewa fulsa hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Chama cha mapinduzi CCM, kupitia mkutano mkuu wa Halmashauri ya mkoa wa Iringa,  ambapo wajumbe wa mkutano huo wamemtaka waziri  huyo wa wizara husika ya maliasili na utalii kuchukua hatua hiyo ya kuvifuta vibari hivyo, haraka ili kuwatendea haki wananchi wa Mufindi na mkoa wa Iringa.

"Ndugu wanahabari, tulikuwa na kikao cha kawaida cha kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabiri wananchi, tumekutana na wajumbe wa Halmashauri kuu ya mkoa, na kero kubwa  ilikuwa niya Vibali katika shamba la miti la taifa la Saohill, vibali ambavyo havikutolewa katika utaratibu unaotakiwa," Alisema Msambatavangu

Jesca Msambatavangu ambaye ni mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa akiwakilisha ujumbe wa mkutano huo mbele ya vyombo vya habari, ametoa tamko hilo, na kumtaka mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma kufikisha ujumbe huo kwa Waziri haraka iwezekanavyo, ili kupunguza ujanza unaotaraji kufanyika.


Aidha Msambatavangu ameongeza kuwa baadhi ya viongozi wameonekana majina yao katika orodha ya mgao wa vibali, huku wengine majina yao yakijirudia zaidi ya mara 20 (Ishirini) jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa msitu huo, kwakuwa asilimia kubwa ya kundi la vijana na wenyeji wa mkoa wa Iringa hawajapata fulsa ya kupatiwa Vibari.

“Tumesikia kuwa tayari kuna mbinu wanazifanya, eti waliotoa vibari wamewaambia waliopatiwa vibari hivyo walipie TRA mapema kama ni njia ya kuzuia kufutwa, tuwaambie tu wananchi kuwa wasikubari kuingizwa katika hasara hiyo, kwani hata wakisajiliwa hawawezi kupewa vibali watakuwa wameingia hasara bure,” alisema Msambatavangu.

Pia alihoji kujiamini kwa baadhi ya viongozi hao wa msitu wa sao hill wanaojihusisha na utaperi huo wa mali ya serikali, kwa madai kuwa wanalindwa na nani ambaye nawapa ujasiri wa kufanya ubadhirifu huo mara kwa mara pasipoi kuwa na shaka na woga wowote.

“Nasikia kuna wananchi waliambiwa watoe shilingi Milioni 3 kwa kila kibali ili kuwa na uhakika wa kupata nafasi hiyo ya kupata vibali, na watu hao waliolipa Milioni 3 kwa kila kibali, hela ambazo alikuwa anapokea mama mmoja na jina tunalo, tumepata taarifa kuwa wamepata wote, kweli hili ni jambo la aibu sana kwa kiongoai wa serikali kufanya ufisadi wa aina hii,” Alisema.

Katika safu ya meza kuu walimtaka mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Ishengoma kuangalia vyema safu ya uongozi wa bodi ya shamba – huku wakiitaka bodi hiyo wawepo wawakirishi wa wananchi kama madiwani na wabunge ili wapate nafasi ya kuwatetea wananchi wao, tofauti na bodi hiyo ilivyo sasa.

Pia Msambatavangu amehoji uwepo wa viongozi wa Wilaya hiyo ya Mufindi- kwa madai kuwa asilimia kubwa wanalifumbia macho tatizo hilo ambalo linawakosesha imani wananchi dhidi ya  serikali yao, hasa wananchi wa Wilaya ya Mufindi ambao ndiyo wazimaji wakubwa wa moto pindi unapoibuka katika shamba hilo la miti.

Pia amesema mfumo wa uongozi wa shamba  husika la Saohill ndiyo una matatizo na kuwa viongozi wote wa serikali watakaobainika kuhusika katika tuhuma hiyo watachukuliwa hatua ikiwa pamoja na kuondolewa katika nyadhfa walizonazo kwa madai kuwa hawawatendei haki wananchi.

Mapendekezo…wametaka katika vibari 800 vinavyotolewa katika msitu huo, angalau vijana wapewe fulsa ya vibali 300, ili kupunguza ukali wa changamoto ya ajira kwa kundi hilo, na asilimia 50 wanufaika wawe niwakazi wa mkoa wa Iringa na asilimia nyingine inayobaki iwe nikwa manufaa ya watanzania wote, kwani msitu huo ni mali ya Taifa ila wakazi wa Iringa wapewe kipaumbele zaidi.


Shamba la miti la Taifa saohill, limekuwa likikabiliwa na changamoto ya ugawaji wa vibari – kwa kupata tuhuma za kutoa fulsa hata kwa marehemu, huku baadhi ya wanufaika wakiwa ni viongozi, jambo ambalo mwaka 2012 liliilazimu Waziri mstaafu wa maliasili na utalii Barozi Hamis Kagasheki kuvifuta vibari 500 ambavyo vilionekana ni mamluki.
MWISHO


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni