Jumatano, 6 Agosti 2014

TAKUKURU YAWASHIKILIA VIONGOZI WALARUSHWA


 
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dr. Retisia Warioba akiwa katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, wakati wakijadili suala la mgogolo wa wafugaji na wakulima wilayani humo. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Steven Mhapa- akizungumzia mgogolo huo wa wakulima na wafugaji katika kikao cha baraza la madiwani.  
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Pedensiana Kisaka akiwa katika kikao hicho cha baraza la madiwani, kilichojadili masuala mbalimbali likiwemo jambo la mgogolo wa wakulima na wafugaji.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Costantino Kihwele- akisikiliza jambo katika kikao cha baraza la madiwani.  

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya iringa Steven Mhapa. akifafanua jambo.
Kushoto ni mkuu wa Wilaya Dr. Retisia Warioba akiwa na makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya iringa wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani ambacho kimetolewa taarifa ya baadhi ya viongozi kushikiliwa na TAKUKURU.

<<<HABARI>>>
BAADHI ya viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa, wametupiwa lawama kwa kujihusisha kugombanisha baina ya kundi la wakulima na wafugaji, na hivyo kusababisha maisha yao kuwa hatarini.

Hayo yamezungumzwa katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa – wakati wakijadili masauala mbalimbali ya amendeleo na changamoto zinazowakabili, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa “Siasa ni Kilimo” mjini Iringa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Steven Mhapa amesema wamebaini uwepo wa baadhi ya viongozi kupokea rushwa kwa kundi la wafugaji kutoka nje ya mkoa wa Iringa, na kisha kuwaruhusu wafugaji hao kuingiza mifuho jambo linalozua migogoro ya hatari ya mara kwa mara.

Mhapa amesema kukithiri kwa tabia hiyo hasa kwa baadhi ya viongozi katika Tarafa ya Pawaga kumekuwa kukisababisha viongozi ngazi ya Wilaya kutofanya kazi kwa kushindia kutatua migogolo hiy.

“Kwa kweli kule Pawaga kuna matatizo ambayo tunaimba serikali ifanye juhudi za maksudi na haraka kutatua tatizo, kwani kuna uvamizi unaotoka nje ya Wilaya, uvamizi huu unafanywa na wafugaji, ambaop wana nnakuna viongozi wengine tumepata taarifa kuwa wanajishughulisha na rushwa, wale wafugaji wanakuja na fedha wanawapa viongozi na viongozi wanawaruhusu wafugaji kuingiza mifugo yao,  viongozi hao lazima wachukuliwe hatua kali sana za kisheria,” Alisema.

Amesema ili kuondokana na tatizo hilo la mgogolo Halmashauri yake imemejipanga kufanya sensa ya mifugo katika Wilaya hiyo lengo likiwa ni kutambua idadi ya wafugaji na kuwawezesha  kutambua eneo watakalotenga kwa ajili ya malisho.

Mhapa amesema wilaya yao ni ndogo na kuwa hawahitaji wavamizi wowote wala mifugo kutoka nje - na kuwa mgogolo huo zaidi upo Kata ya Itunundu, na suluhu ya tatizo hilo katika kuepusha mauaji ni kuchukuliwa maeneo ya zamani ya wachungaji ili kusaidia kupunguza tatizo hilo.

Amesema tayari wameandika barua kwa Waziri mwenye dhamana ikiwa pamoja na nakala kuifikisha katika ofisi ya Waziri mkuu ili kuifahamisha serikali juu ya hatari iliyopo katika Halmashauri yao.
Diwani wa Kata ya Itunundu Halfani Lulimi amesema mgogolo huo ambao unaigusa na kata yake, unachangia maendeleo kudhorota, kwa kuwa kuna wakati vurugu hizo zilitaka kusababisha maafa ambapo hata askari polisi alitaka kuuawa katika vurugu hizo.

“Kuna tatizo kubwa sana hasa kule kule kwenye Kata ya Mlengo na Itunundu, na mwingiliano huo niwa maeneo ya machungo na kilimo, hasa msimu wa kilimo Kata ya Itunundu na Mlenge zinazoingiliana katika matumizi ya miundombinu ya kilimo,” alisema Lulimi.

Amesema madhara ambayo tayari yametokea ni pamoja na wananchi kupigwa huku askari wakitishiwa kuuawa, mara tu unapozuka mgogolo huo.

Diwani Lulimi amesema awali aliishauri serikali kutoa eneo la “Lunda Kaskazini Mkwambe” ili wafugaji wakakae huko, na kuwaachia wakulima eneo lenye mgogolo, na kuwa hilo litakuwa ni suluhu ya mgogolo huo- kwani kiini cha mapigano ni mwingiliano wa maeneo ya kilimo na mifugo.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dr. Retisia Warioba amesema viongozi wanaosababisha wakulima na wafugaji kuingia katika mgogolo ambao umedumu kwa zaidi ya miaka mitatu sasa, tayari wanashilikiwa na taasisi ya kudhibiti na kuzuia Rushwa TAKUKURU.

Dr. Warioba amesema migogolo iliyopo katika kata za Pawaga niya hatari hasa katika Kata ya Magozi ambapo wafugaji huchungia mifugo kwenye mashamba ya wenzao, na kuwa kila mwezi kamati ya ulinzi na usalama wanakwenda mara tatu Pawaga kutatua mgogolo huo.

Dr. Warioba amesema wahusika wa matukio ya kupokea fedha wametajwa na wafugaji kuwa ni  Mtendaji na mwenyekiti ambao sasa wamekabidhiwa mikononi mwa TAKUKURU, na kuwa wamefanya doria kubwa ya kuwaondoa wavamizi wote.

Kwa mujibu wa bajeti ya mwaka 2013/2014 Tanzania inakadiliwa kuwa na zaidi ya  ng’ombe zaidi ya milioni 22, mbuzi zaidi ya milioni 15, Kondoo zaidi ya milioni 7 na Nguruwe zaidi ya milioni 2, ambapo Wizara husika imezitaka Halmashauri kuandaa Mipango ya Matumizi ya Ardhi na kutenga maeneo ya ufugaji, kwa ajili ya kuendeleza malisho ya mifugo ili kuepusha migogoro ya mara kwa mara .


MWISHO.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni