MSANII wa muziki wa kizazi, kipya mjini Iringa, ONE LEE akitoa zawadi ya ngoma kwa mwandishi wa Habari
Frank Kibiki kwa niaba ya wasanii wenzake, ambaye hivi karibuni alitangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Iringa mjini.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa, wasanii hao walisema wameamua kutengeneza
wimbo huo kutokana na mchango mkubwa wa mwanahabari huyo, katika fani yao.
Msanii huyo Richard Kayombo ‘One Lee’ ambaye alikabidhi wimbo kwa niaba ya wasanii wenzake alisema wimbo
huo, unamtambulisha Kibiki, kama kiongozi wa kuigwa kutokana na tabia yake ya
ucheshi na kujichanganya na watu.
akizungumza wakati wa kukabidhi WIMBO huo msanii ‘One
Lee’ alisema kuwa FRANK KIBIKI amekuwa akiwapa elimu vijana juu ya
kujitambua na kuwasaidia jinsi gani ya kujiajili wao wenyewe na
kuonyesha njia ya kutokea kimaisha na dio imekuwa sababu ya wasanii wa
mkoani hapa kutunga wimbo huo.
“Wimbo
unaitwa ‘Kuwa mfano wa kuigwa’, tumempa kaka yetu kama zawadi, ili wengine
waige mfano wake.
Awali tulitamani uitwe Kibiki, lakini kwa sababu tunataka
kuuza tumeamua kuuita jina hilo,”alisema One lee.
Alisema miaka
miwili iliyopita, aliwahi kukutwa na jambo ambalo alihitaji msaada wa haraka,
alihangaika lakini alipokutana na Kibiki ambaye ni Mjumbe wa mkutano mkuu wa
CCM taifa, alisaidiwa jambo ambalo lilimfanya aanze kumuheshimu.
Alisema
aliposikia kuwa Kibiki ametangaza nia, aliamua kushirikiana na wenzake ili
watengeneze wimbo ambao hivi karibuni utaachiwa hewani.
‘One lee’alisena
ngoma yake itamtambulisha Kibiki kama alivyo, na kwamba wameamua kumsaidia bila
gharama yoyote kama sehemu ya mchango wao wakiamini ikiwa atafanikiwa kupenya
na kupata nafasi hiyo, ataweza kuwaunganisha na kuwainua wasanii.
kwa
upande wao wasanii wengine wa mkoani irnga walisema kuwa imefika wakati
sasa iringa mjini itawaliwe na kiongozi mwenye uelewa juu ya kukuza
uchumi wa mkoani na kuzingatia vipaji vya vijana kwa kuwa vijana ndio
taifa la leo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni