MWANAHABARI
FRANK KIBIKI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE
MWANAHABARI
FRANK KIBIKI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE
na mwanahari wetu,iringa
MWANAHABARI
Frank Kibiki, aliyewahi kuwa Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi
(UVCCM) ngazi ya wilaya kwa zaidi ya miaka 10.
Akizungumza na
mtandao huu MWANAHABARI
FRANK KIBIKI alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wakibweteka
kwa kutojituma kufanya kazi na kuendelea kuilaumu serikali.
“Eti asubuhi
unawakuta vijana wamekaa kwenye vijiwe wakizungumza siasa na kucheza mabao
wakati hawajui mchana watakula wapi na jioni watarudi na nini nyumbani”alisema MWANAHABARI FRANK KIBIKI
MWANAHABARI
FRANK KIBIKI ameendelea kuwaomba vijana wengi wenye fursa
ya kurudi au kuingia shuleni upya warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi
wengi kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na sayansi na teknolojia na ndio
sababu inayopelekea hata watu wazima kurudi shuleni.
“Vijana
mnatakiwakujifunza kutoka kwa watu wazima ambavyo wamekuwa wakijituma kufanya
kazi kwa bidii na kujituma ilimradi kuwatengenezea watoto maisha mazuri pamoja
na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla”alisema MWANAHABARI FRANK KIBIKI
Lakini
MWANAHABARI
FRANK KIBIKI amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi
kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa
kumi mwaka huu.
MWANAHABARI
FRANK KIBIKI ameeleza kuwa wanawake waondoe hofu ya
kugombea hasa kukiwa na ushindani wa wagombea wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa
kwa mambo yasiyokuwepo.
Ameendelea kusema
kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na badala yake wachague
viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika chama chochote.
Aidha ameongeza kuwa
viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea haki wapiga kura wao hali
itakayowafanya waaminike katika jamii.
Mbali na hayo MWANAHABARI FRANK KIBIKI amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na
baadhi ya wanasiasa katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea
uchaguzi mkuu na badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa
kiongozi kutokana na sera za chama chake.
Ameendelea kusema
kuwa vijana wajitokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo katika katiba
iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wa haki na amani pia
kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura pamoja na kupiga
kura.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni