Kocha wa Arsenal, Arsene
Wenger, amesema bado hajajua lini mchezaji wa kiungo Jack Wilshere
atarejea uwanjani baada ya
Wilshere hajacheza tangu
Novemba alipoumia kifundo cha mguu katika mechi ya Ligi Kuu ya England
ambapo Arsenal ilifungwa mabao 2-1 na Manchester United.
Alikua
arejee mazoezini lakini kabla ya mechi ya Jumanne dhidi ya Leicester
City, Wenger alisema: "Lazima tumchunguze kila siku. Sijui lini ataweza
kurejea uwanjani."
Kuhusu mchezaji mwingine Alexis Sanchez ambaye
tayari amefunga mabao 18 msimu huu, Wenger alisema, “ Atajiunga na
kikosi “ kitakachocheza na Leicester na kwamba hakukuwepo majeruhi
wowote katika mchezo wa Jumamosi ambapo Arsenal walishindwa na watani
wao wa jadi Tottenham.
Kwa kupoteza mechi hiyo Arsenal sasa inashiikilia
nafasi ya sita katika Ligi Kuu.
Mbali na Wilshere na Sanchez
Arsenal pia inamkosa Alex Oxlade-Chamberlain ambaye aliumia wakati
Arsenal ilipopambana na Manchester City mnamo mwezi uliopita.
Wilshere akishangilia kwa mashabiki baada ya kumalizika mpambano.
Kocha wa arsenal arsene wenger
By Caunter Mgaya Jr.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni