Jumamosi, 8 Machi 2014

AIRTEL YAKABIDHI VITABU TOSAMAGANGA




 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Tosamaganga- Iringa

 Viongozi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakiwa na baadhi ya walimu wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiana vitabu.
 Meneja wa kampuni ya Airtel Beda Kinunda akitoa ufafanuzi juu ya msaada huo wa vitabu kwa shule hiyo ya sekondari ya wavulana ya Tosamaganga.

 
  Afisa mauzo (Biashara) wa kampuni ya Airtel mkoa wa Iringa Hudson Kamenya akiwa shuleni hapo Tosamaganga.
 Mkuu wa shule ya sekondari Tosamaganga - Iringa Damas Mgimwa akipokea baadhi ya vitabu kutoka kwa afisa mauzo wa kampuni ya Airtel Hudson Kamenya.
 Mmoja kati ya wanafunzi wa sekondari Tosamaganga akipokea baadhi ya vitabu vya masomo ya Hisabati na Sayansi.
 Mmoja kati ya wanafunzi wa sekondari Tosamaganga akipokea baadhi ya vitabu vya masomo ya Hisabati na Sayansi.
 Mmoja kati ya wanafunzi wa sekondari Tosamaganga akipokea baadhi ya vitabu vya masomo ya Hisabati na Sayansi.
 Mmoja kati ya wanafunzi wa sekondari Tosamaganga akipokea baadhi ya vitabu vya masomo ya Hisabati na Sayansi.
 Baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya Tosamaganga wakiwa na vitabu, walivyokabidhiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel
 Baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya Tosamaganga wakiwa na vitabu, walivyokabidhiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel.
 Meneja wa Airtel mkoa wa Iringa Beda Kinunda akimkabidhi Box  la Vitabu mkuu wa shule ya sekondari Tosamaganga damas Mgimwa
 Meneja wa Airtel mkoa wa Iringa Beda Kinunda akimkabidhi Box  la Vitabu mkuu wa shule ya sekondari Tosamaganga damas  Mgimwa
 Mkuu wa shule ya Sekondari Tosamaganga - Damas Mgimwa akishuhudia wanafunzi wakishangilia msaada huo wa vitabu kutoka kampuni ya Airtel.


 

 <<<HABARI>>>

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imekabidhi vitabu vya masomo ya Sayansi, kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Tosamaganga, kwa lengo la kupungua ukali wa tatizo la vitabu shuleni hapo.

Akikabidhi msaada huo meneja wa kampuni ya Airtel mkoa wa Iringa Beda Kinunda amesema kampuni yake imejiwekea mikakati ya kusaidia sekta ya elimu, kwa kutoa vitabu ambavyo ni tatizo sugu kwa shule nyingi za sekondari hapa nchini.

Kinunda amesema  Airtel imetoa msaada huo kupitia mpango wa “Shule yetu” ambapo  kampuni hutoa msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa shule zenye uhitaji - lengo likiwa ni kuinua kiwango cha elimu nchini.


Hudson Kamenya- Afisa biashara wa Airtel mkoa wa Iringa  na kuwa shule ya Tosamanganga ni kati ya shule zenye changamoto za vitabu na Tosamaganga ni shule yenye bahati zilizochaguliwa na kampuni hiyo.

Hiraly Sandagila mwalimu wa taaluma Tosamaganga amesema kuna upungufu mkubwa wa vitabu vya masomo ya Sayansi, Somo la Physicia kuna vitabu 23 uhitaji ni 3527 na hisabati 24 ambapo kitabu kimoja uwiano  nikwa wanafunzi 17 huku uhitaji 529.

Sandagila amesema kwa somo la Chemia kuna afadhari kwani vitabu vilivyopo ni 300 huku mahitaji yakiwa vitabu 100 na vitabu vya Biologia vipo 38 mahitaji ni zaidi ya vitabu 260, na kuwa msaada huo utasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa vitabu hususani vitabu vya Hesabu na Pysicia.

Sandagila ameishukuru kampuni ya Airtel kwa kuliona tatizo hilo, kwa madai kuwa baadhi ya wanafunzi wanmwamko wa elimu lakini wamekuwa wakikwamisha na hali ya upungufu wa vitabu, na hivyo kushindwa kujisomea.


Mkuu wa shule hiyo ya Sekondari Tosamaganga  Damas Mgimwa amewataka wanafunzi hao kuvitunza vitabu hivyo ili viwasaidie kujisomea zaidi na kuongeza kiwango cha ufaulu.

Nao wawakirishi wa wanafunzi hao wa sekondari ya Tosamaganga - Dominic Kamugisha na Frolian Mwebesa wameishukuru kampuni hiyo ya Airtel kwa msaada huo.

MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni