Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi. Evarista Kalalu akipeana mkono wa pongezi na kaimu meneja wa msitu wa Sao hill Mkoani Iringa Bw. Shedrack Bijuro kwa kupata vitendea kazi vitakavyoongeza tija katika utendaji wa kazi wa Shamba hilo la Taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi. Evarista Kalalu akipeana
mkono wa pongezi na mmoja wa watumishi wa shamba la Sao hill kwa
kupata Usafiri wa Pikipiki kama ni kitendea kazi cha kuharakisha majukumu ya kiutendaji katika Shamba hilo la Taifa.
Kaimu meneja wa msitu wa Sao hill Mkoani Iringa Bw. Shedrack Bijuro akitazama usafiri ambao serikali imewapatia watumishi wa shamba hilo kwa lengo la kuboresha utendaji wa kazi katika Msitu huo wa Taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi. Evarista Kalalu (mwenye suti za vitenge) akiwa na kaimu meneja wa shamba la Sao hill Bw. Shedrack Bijuro (wa pili kulia) wakitazama Magreda mawili ambayo pia yapo katika mgao huo, ambayo yametolewa kwa lengo la kuboresha miundombinu ya barabara za shamba la Msitu huo.
"Hivi vifaa kweli vitatusaidia sana kulikuza zaidi shamba letu, kama tuliweza wakati tunatumia vitendeakazi chakavu na duni, sasa tutaweza zaidi, watanzania wategemee mazuri kutoka Saohill" Ni maneno ya mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi. Evarista Kalalu wakati akibadilishana mawazo na uongozi wa Shamba.
Wakiwa katika picha ya pamoja
<<<HABARI>>>
SERIKALI imetumia zaidi ya shilingi Bilioni 2.3 kwa ajili ya
kununua magari kumi na Pikipiki 25 kwa ajili ya kuliboresha Shamba la Taifa la
miti la Sao hill Mkoani Iringa
Akitoa taarifa hiyo katika kikao cha makabidhiano ya vifaa
hivyo, kaimu meneja wa Shamba la Saohill lililopo Wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa
Shadrack Bijuro amesema magari hayo licha ya kuleta ufanisi mkubwa wa kazi pia
ni chachu ya ufanisi wa kazi.
Aidha amesema aina za usafiri huo ni pamoja na Greda moja
lenye thamani zaidi ya shilingi Milioni 561, gari aina ya Kijiko moja lililogharimu
zaidi ya shilingi Milioni 561, Nissan Patrol tatu zenye thamani zaidi ya
shilingi Milioni 300 na Basi aina ya Nisan Diesel lenye thamani zaidi ya shilingi
Milioni 272.
Bijuro amesema pia wamepata gari aina ya Nissan Pickup 3
zenye thamani zaidi ya shilingi milioni 271, Isuzu Lorry moja lenye thamani
zaidi ya milioni 206, pamoja na Pikipiki 25 aina ya Honda ambazo zimenunuliwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi
milioni 167 .
Naye mkuu wa Wilaya ya mufindi Bi. Evarista kalalu amewataka
watumishi wa Shamba hilo kuwa na nidhamu katika kuvitunza vifaa hicyo ili
viweze kudumu kwa muda mrefu.
Kalalu amesema serikali inayo malengo madhubuti katika shamba
hilo ambalo ni mali ya Watanzania, na hivyo wajibu mkubwa kwa uongozi wa shamba
hilo la Taifa la Saohill ni kujituma kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na weredi
wa kutosha.
Hata hivyo Kalalu amesema watanzania wategemea mambo makubwa
mazuri zaidi katika Shamba hilo, huku akiwaasa watumishi kufanya kazi kwa
ushirikiano kwani ndiyo siri kubwa ya mafanikio.
Flora Malekela na Willium Dafa wamesema wamekuwa wakipata
taabu ya kutembea kwa miguu umbali mrefu katika ulinzi wa shamba hilo jambo
ambalo lilikuwa ni changamoto kubwa kwao.
“Nikiwa kama mkuu wa safu ya Ihalimba, Pikipiki hizi
zitatusaidia sana, kwani awali tumepata taabu ya kutembea kwa miguu, na sasa usafiri
huu utaturahisishia kufanya kazi” Alisema Malekela.
Naye Dafa Meneja tarafa ya nne ya shamba hilo la miti amesema
…“Katika Tarafa yangu ninapanda kila mwaka Hekta elfu mbili za miti na lakini
mimi na wenzangu tumekuwa tukipata taabu sana ya kutembea umbali wa km 35 katika
kazi za ukaguzi na mimi nimepatiwa gari hii Nissan Patrol Station Wagon itanisaidia
sana kufanya kazi kwa uharaka zaidi,” Alisema.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni