Gari likipita katika barabara kuu ya kuelekea Wilaya ya Kilolo, moja kati ya maeneo korofi ambayo yanalalamikiwa na wanachi.
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo- Iringa Gerlad Guninita (kulia) akitoa taarifa ya roba mwaka kwa msimu wa mwaka 2014, katika kikao chake na baadhi ya wakuu wa idara na kamati ya ulinzi na usalama Wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo- Iringa Gerlad Guninita (kulia) akitoa taarifa ya roba mwaka kwa msimu wa mwaka 2014, katika kikao chake na baadhi ya wakuu wa idara na kamati ya ulinzi na usalama Wilayani humo.
Baadhi ya wakuu wa idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo- Iringa wakisikiliza kwqa makini taarifa ya mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerlad Guninita (Haonekani pichani).
<<<<<<<<<<<<HABARI>>>>>>>>>>>>
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
imekwama kutekeleza mipango mikakati yake ya ujenzi na ukarabati wa barabara,
baada ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kusitisha shughuli hizo.
Hayo yamezungumzwa na mkuu wa Wilaya ya Kilolo
Gerlad Guninita wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za serikali
kwa kipindi cha miezi mine, kuanzia January hadi april mwaka 2014.
Guninita amesema kushindwa kukamilika kwa
barabara hizo kunachangia hali ya uchumi kudumaa, kwa kuwa mazao mengi ya kilimo na biashara katika
Wilaya hiyo yanategemea kuuzwa katika masoko
ya nje ya Wilaya.
Amesema
kutokukamilika kwa wakati kwa barabar hizo kumeyafanya magari
yanayosafirisha mazoa na bidhaa mbalimbali kukwama, na hivyo kudumaa kwa uchumi
wa wananchi wa Wilaya ya Kilolo.
Akitaja barabar zilizotengewa fedha Guninita
amesema Wilaya ya Kilolo ilipanga kutekeleza shughuli mbalimbali za ujenzi, huku ikitenga jumla ya shilingi
Bilioni moja, miamoja sitini na sita,
laki tisa na elfu mbili (1, 196, 902, 000/= ambazo zingetumika kwa ujenzi wa
miradi ya barabara kwa kipindi cha 2013/2014.
Guninita amesema fedha hizo zilidhamilia
kukamilisha jumla ya miradi 12 ya ukarabati na ujenzi wa barabara, katika
maeneo mbalimbali, yakiwemo matengenezo ya barabara ya Idete- Kiwalamo, yenye
urefu wa km 16, ujenzi uliotengewa zaidi ya shilingi 367.
Ametaja ujenzi wa daraja la Kiwalamo, ujenzi wa Lami
katika barabara ya Ilula mjini, ambayo itagharimu zaidi ya shilingi Milioni
363, huku matengenezo ya barabara ya Ruaha Mbuyuni- Msosa yenye km 6, ambayo
ujenzi wake unaendelea na zaidi ya shilingi Milioni 53 zilielekezwa katika kazi
hiyo.
Ujenzi wa barabara ya Ibumu – Ilambo, Ilula- Image
km 16.5 iliyopangiwa kiasi cha shilingi Milioni 107, pamoja na ukarabati
wa barabara ya Kilolo mjini, Kitowo – Mwatasi na Kilolo- Nguruhe iliyotengewa
kiasi cha shilingi Milioni 101.
Pia amesema kuna ukarabati wa barabara ya Ihimbo-
Kising’a, Wotalisoli-Udekwa, Makungu- Mlafu km 23 fedha zilizopangwa zikiwa ni
zaidi ya shilingi Milioni 105, na barabara nyingine kama ya Ilula mjini-
Vitono, Uhambingeto na Kipaduka- Ikuka 12.5 fedha zaidi ya shilingi milioni 108, na kazi inaendelea.
Amezungumzia matengenezo ya barabara ya Kidabaga-
Bomalang’ombe, Ukumbi- Masege, mawambala- Winome na Bomalang’ombe- Mwatasi km
26 na kiasi cha fedha zilizoidhinishwa kwa ujenzi huo zikiwa ni shilingi
Milioni 94.
Aidha amesema kuna matengenezo ya barabara ya
Mtandika – Nyazwa, Mtandika – Msosa, Mahenge- Irindi- Magana na Irole- Kitumbuka
zenye km 27 kwa kiasi cha shilingi Milioni 206, 660,000/=.
Maeneo mengine yaliyopangiwa fedha kwa ajili ya
ukarabati wa barabara ni Mwatasi- Ng’ungula na Ng’ingula- madege km 23 kiasi cha
zaidi ya shilingi Milioni 209, huku barabara ya Idete- Mhanga na ujenzi wa
daraja la Mhanga kwa kiwango cha fedha kiasi cha shilingi Milioni 209, 291,
000/=.
Hata hivyo muhandisi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ya Kilolo injinia Wahabu Nyamzungu amesema mpango wa kufanikisha ujenzi huo ni kutoa tenda kwa wakandarasi kuanzia mwezi wa saba ili kutokwamisha na hali ya jiografia ya Wilaya hiyo.
"Wilaya ya Kilolo kama inavyofahamika jografia yake niya mvua kwa msimu mrefu, kwa hiyo ili kufanikisha ujenzi wa barabar zetu tutakuwa tunatoa kazi kwa wakandarasi msimu ambao mvua zimemalizika kunyesha," alisemaNyamzungu.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni