Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano wa kuilalamikia manispaa juu ya idadi kubwa ya kodi na ushuru, ambao umedaiwa unatishia uhai wa biashara zao.
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa katika ukumbi wa Orofea- Iringa
Mmoja wa wafanyabiashara akisikiliza jambo kwa umakini mkubwa katika mkutano wa malalamiko juu ya kodi na ushuru rukuki ambao zimedaiwa kuwa ni mzigo kwao na tishio kwa biashara zao.
Baadhi ya kundi la wafanyabiashara wakiwa katika ukumbi wa Orofea Kitanzini mjini Iringa - wakisikiliza jambo katika mkutano baina yao, maofisa wa Manispaa ya Iringa na mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa.
Viongozi wa wafanyabiashara mwenye sati jeupe jackson Kalole ambaye ni katibu wa umoja wa wafanyabiashara Iringa akisikiliza jambo katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Orofea Kitanzini mjini Iringa.
Afisa
biashara wa Manispaa ya Iringa Ipyana Kabuje akitoa majawabu ya maswali
yaliyoulizwa na wafanyabiashara juu ya uwepo wa idadi kubwa za kodi na
ushuru.
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) akizungumza na wafanyabiashara wa Iringa katika ukumbi wa Orofea "Jumba la maendeleo" lililopo Kitanzini Iringa mjini, mkutano uliokuwa niwa malalamiko ya wafanyabiashara wakilalamikia uwepo wa idadi kubwa ya kodi na ushuru .
Mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara wa manispaa ya Iringa Odilo Ngamilaga akizungumza jambo katika mkutano wa wafanyabiashara, maofisa wa Manispaa ya Iringa na mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa.
Afisa
biashara wa Manispaa ya Iringa Ipyana Kabuje akitoa majawabu ya maswali
yaliyoulizwa na wafanyabiashara juu ya uwepo wa idadi kubwa za kodi na
ushuru.
Wakiwa katika picha ya makundi na mbunge mchungaji Peter Msigwa na maosisa wa Manispaa kitengo cha biashara.
Wakiwa katika picha ya makundi na mbunge mchungaji Peter Msigwa na maosisa wa Manispaa kitengo cha biashara.
Wakiwa katika picha ya makundi na mbunge mchungaji Peter Msigwa na maosisa wa Manispaa kitengo cha biashara.
<<<<HABARI>>>>
WAFANYABIASHARA
mkoani Iringa, wametangaza mgomo wa kufunga maduka kwa zaidi ya siku saba,
endapo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa itaendeleza utitili wa kodi na ushuru ambao
ni mzigo kwao.
Hayo
wamezungumza na wafanyabiashara wa Mji wa Iringa katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Orofea-
Kitanzini mjini Iringa, uliowakutanisha wafanyabiashara, watumishi wa manispaa
ya Iringa kitengo cha boiashara na mbunge mchungaji Msigwa.
Zain Yusuph
amesema kumekuwa na idadi ya kodi na ushuru ambao hauna tija, huku baadhi ya
huduma za wananchi zinazotakiwa ziboreshwe na manispaa hiyo zikidorora.
Zain amesema
kutapakaa kwa takataka katika manispaa ya Iringa wakati wao wakitozwa ushuru wa
taka ngumu, ni jambo ambalo haliwaingii akilini juu ya utaratibu huo wa manbispaa
ya Iringa.
“ Hivi hii
Halmashauri yetu hamna mipango endelevu, maana kuna wakala alipewa tenda ya kukusanya
kodi na ushuru, lakini baada ya muda wakala huyo amekula hela zetu na
mnatuambia akimbia, sasa tunauliza hela zetu inamaana zinakusanywa kwa ajili ya
kuwanufaisha watu wachache au vipi, mie mambo hayo hayaniingii akilini, kuna
kodi ya Mabango yaliyopo madukani kwetu, elimu, takangumu, tunataka mtueleze
hizi hela zinapelekwa wapi ili tuweze kuhoji matumizi yake,” alisema Zain.
Nicolaus Punjili
amesema kumekuwa na tofauti ya huduma baina ya Manispaa ya Iringa na nyingine,
kwani licha uwepo wa ushuru na kodi mbalimbali zinazodumaza hali ya uchumi wao
lakini huduma za afya Hospitalini zimekuwa ni duni, na huku wafanyabiashara
wanakamulia kodi hadi wengine wanaamua kufunga maduka yao na kukimbia na baadhi
yao wanakufa kwa ajili ya kodi, huku hakuna mabadiliko mazuri mitaani.
“Sisi hatukatai
kulipa kodi lakini tunataka kodi zetu tunazokamuliwa ziwe na tija, tunaambiwa
tunatakiwa kulipia Servics Leavy, kodi hii imekuwa ikitozwa kila mwaka kwa
maelezo kuwa niya huduma, kitu ambacho mtoa kodi haambiwi ni huduma gani na ipi
atapewa baada ya kulipia kodi hii, na kama ni huduma mbona kila kitu tunalipia
hata zile ambazo hatustahili kulipia??,” Alisema Punjili.
Baraka Kimata
amesema utitiri wa kodi hizo hauendani kabisa na huduma zinazotolewa na hivyo
kuna haja ya kuishtaki Manispaa hiyo pindi inapodhorotesha huduma kwa wananchi,
kwa kuwa hali ya mji wa Iringa kwa sasa uchafu haulingani na makusanyo ya kodi
na ushuru uliopo.
“Kwakweli
inafika mahali inasikitisha, sheria hizi inabidi ziwe zinambele na nyuma, maana
sisi tunabanwa na sheria kulipa kodi lakini tukilipa huduma hazipo na wala
hazipatikani, kuna haja sasa ya kuwabana pindi smamlaka husika inapokiuka kwa
kushindwa kutekeleza wajibu wake,” alisema Kimata.
Maneno Mbuma
amesema hawaelewi kodi zao zinafanya kazi gani, kwani baadhi ya huduma ambazo
zinatakiwa kutolewa bure kwa wananchi baada ya wafanyabiashara kukatwa kodi na
ushuru, huduma hizo zinadaiwa zilipiwe tena jambo ambalo linawakosesha imani na
uongozi wa Manispaa hiyo ya Iringa.
“Kwa mwezi
tunalipa lakitatu na 65 kwa magari yetu madogo haya “Pick up” lakini hoja ni
kuwa hela zinakwenda wapi, tunajua vifaa vilivyonunuliwa kama Greda nikwa ajili
ya kuboresha barabar zetu, kwa kuwa vifaa hivyo vinanunuliwa kutokana na kodi
na ushuru tunaolipa, lakini unakuta Manispaa pindi wananchi wanapohitaji
kutengenezewa barabara zao wanalipishwa tena kila mtaa shilingi laki mbili na hamsini,”
Alisema Mbuma.
David Butinini
amesema ulipaji wa kodi umekuwa haufuati taratibu, ambapo watendaji wa mitaa
wamekuwa wakijikusanyia kodi za majengo pasipo kutoa Stakabadhi, na hivyo fedha
nyingi kuishia mifukoni mwa viongozi hao.
“Michango na
kodi za Propart Tax, wanachukua watendaji tena bila kutoa risiti tuna nyumba
hapa manispaa zaidi ya elfu 4 zil;izoandikisjhwa kwenye daftari, lakini
zinakusanywa kiholela na hatujui zinakwenda wapi, kwani pesa yoyote inayoingia
kwenye Halmashauri ni lazima ipite Benki!! Kwa sababu haiwezekani fedha ya
serikali ikakusanywa kiholela holela tu, unakuta unaotoa kodi lakini baada ya
kuja mtendaji mwingine naye anakuja kukudai kodi hiyo hiyo ambayo umeshalipa, tunasema
sasa fedha yoyote ya serikali lazima ipite Benki, hatuwezi kupeana hela ya
serikali kamatunauziana Maandazi,” Alisema Butinini.
Clement Mbala amesema “mfano pale Soko kuu
kuna utaratibu wa kulipa pango elfu sita kila mwezi, na kuna mkataba ambao
tunaingia na Manispaa, lakini safari hii wametubadilishia na kututaka tulipe kodi
ya pango miezi sita sita, na usipolipa miezi sita wanatupiga faini nusu ya
kodi, kweli huu hii ni sawa??,” Alihoji Mbala.
Katibu wa
wafanyabiashara hao Jackson Kalole amesema licha ya idadi kubwa ya kodi na ushuru
ambao unatishia hali ya uwepo wa biashara zao huku baadhi ya
wafanyabiashara wakifunga maduka kwa
kufirisika, na wengine wakihama mji huo kutokana na utitili huo wa kodi.
Kalole amesema
kamwe hawatasita kufunga maduka yao, endapo usumbufu unaofanywa na watumishi wa manispaa hiyo utaendelea, na
kuwa kilio kikubwa cha wafanyabiashara ni ongezeko la idadi ya kodi na ushuru
ambao hauna tija kwa maendeleo ya wananchi.
“Lakini kitu
kingine kuna tatizo la Mgambo, hawa mgambo wanawanyanyasa sana wajasiliamali,
huku wakiwanyang’anya mali na bidhaa zao, badala ya kuwaonyesha maeneo stahiki
ya kufanyia biashara,” Alisema.
Kalole amesema
kitu kingine ambacho kimewaongezea mzigo ni uwepo wa kodi ya mfuko wa elim,
kodi ambayo hawajashirikishwa wao na wananchi wanaulipishwa, ili waweze
kutathmini namna watakavyoweza kushiriki.
Amesema uwepo wa
kodi hiyo umezua sintofahamu kwao kwani haifahamiki kodi hiyo imelenga kutatua maeneo
yapi ya elimu, huku akihoji sababu za kulipa kodi hiyo ya mfuko wa elimu wakati
matatizo ya sekta hiyo bado yanazidi kuongezeka badala ya kupungua.
Kalole ameeleza kuwa mfanyabiashara amekuwa ni mtu wa kulundikiwa mzigo wa kodi, wakati sekta hiyo
ya elimu inayo bajeti yake kila mwaka, na wananchi na wazazi wakichangia huko
mitaani.
Akiorodhesha
aina ya kodi hizo Kalole amesema kuna kodi ya huduma “Service Lavy” kodi ya zimamoto “Fire extinguisher” Leseni
ya biashara, Makadilio ya mapato “TRA TIN, Kodi ya ongezeko la Thamani “VAT” ,
Ununuzi wa mashine za EFD, Kodi ya pango ambayo wanatakiwa wafanyabiashara
walipe asilimia 10 ya kiwango kinacholipwa kwa mwenyenyumba, Kodi ya mabango,
Ushuru wa maengesho ya magari “ Car Packing”,
Ushuru wa kuegesha magari mbali na maeneo ya biashara pamoja na Ushuru
wa takangumu.
Mwenyekiti wa
umoja wa wafanyabiashara hao Odilo Ngamilaga amesema ushuru na kodi hizo Odilo
amesema kuna idadi ya ushuru na kodi zaidi ya 13 ambao ni Leseni, Fire
extinguisher- ambacho ni kifaa cha kuzimia moto, Makadilio ya mapato yaani TRA TIN, Kodi ya
ongezeko la thamani yaani VAT.
Amesema Kodi
nyingine ni ununuzi wa mashine za EFD, Kodi ya pango ambayo wanalipishwa
asilimia 10 TRA, ushuru wa maegesho ya magari, Kodi ya mabango ya matangazo,
ushuru wa taka ngumu na kodi ya huduma yaani Service Levy, na kuwa endapo watumishi wa manispaa na TRA wataendelea kuwasumbua kwa kodi na ushuru huo basi watafunga maduka yao na kusitisha kutoa huduma kwa wiki nzima.
Afisa biashara
wa Halmashauri ya manispaa ya Iringa
Ipyana Kabuje amewataka wafanyabiashara hao kuandika kwa maandishi kero
zao ili kuzifanyiakazi kwa muda muafaka, huku akiwasihi wafanyabiashara hao
kutochukua uamuzi huo wa kufunga maduka.
Hata hivyo
mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa ameitaka Halmashauri
hiyo ya manispaa ya Iringa kuhakikisha inaboresha huduma zake kwa jamii, ikiwa
pamoja na kufuata taratibu za ukusanyaji wa kodi, kwa kufungua akaunti ili kodi
zote ziingizwe benki na kujenga imani kwa walipa kodi hao.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni