Dr. Retisia Warioba kaimu mkuu wa Mkoa wa Iringa, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa akiwahutubia wananchi wa Ulata, juu ya umuhimu wa chanjo kwa watoto.
Dr. warioba akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ulata, kilichopo Kata ya Wasa Iringa vijijini.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ulata, waliofika na watoto wao kupatiwa huduma ya chanjo wakimsikiliza Dr. Warioba, aliyezindua rasmi shughuli za chanjo mkoa wa Iringa.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, wakijitambulisha kwa wananchi wa kijiji cha Ulata, ambako maadhimisho ya siku wiki ya chanjo yamefanyika huku kimkoa.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ulata wakisikiliza jambo kutoka kwa Dr. Warioba katika uzinduzi wa wiki ya chanjo.
Watatu kulia ni mganga mkuu wa Wilaya ya iringa- Dr. Ignus Mlowe akiwa na watumizshi wenzake wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, katika kijiji cha Ulata siku ya chanjo ambayo kimkoa ilifanyika katika kijiji cha Ulata Kata ya Wasa.
<<<<HABARI>>>>
WANANCHI wa kijiji cha Ulata na Ngonamwasi vilivyopo Kata ya Wasa katika Halmashauri ya Wilaya
ya Iringa wanakabiliwa na changamoto kuwa ya upatikanaji wa huduma ya fya, kwa
kulazimika kutembea umbali wa zaidi ya km 30.
Wananchi hao wanalazimika kutembea umbali wa km 32
kuifikia huduma ya afya katika Zahanati ya Wasa, jambo linalowafanya akinamama
wajawazito na wagonjwa kushindwa kupata huduma hiyo muhimu.
Licha ya umbali, pia upatikanaji wa usafiri ni
mgumu, huku miundombinu ya barabara ikiwa si rafiki kwa maendeleo na usalama wa
wananchi, kwani baadhi ya maeneo ya barabara yamebomoka na hivyo wananchi kuwa
ndiyo wenye jukumu la kuyafanyia ukarabati.
Wananchi hao wameyazungumza hayo katika uzinduzi wa
zoezi la chanjo, lililofanyika katika kijiji cha Ulata, zoezi lililozinduliwa
na kaimu mkuu wa Wilaya ya Iringa Dr. Retisia Warioba ambaye ni mkuu wa Wilaya
ya Iringa.
“Hapa unaona
tumekuja watu wachache, siyo kama hawataki, wanakwepa kutembea mwendo mrefu , kilomita 16 kwenda na kurudi ni km 32, sasa
unakuta wale wasio na uwezo wa kutembea hawawezi, na hiyo ndiyo inasababisha
wengine kudiriki kutumia hata dawa za kienyeji kwa sababu kwenda Wasa na kurudi
hizo mk 32 hawezi,” Walisema.
Mwenyekiti wa
serikali ya kijiji cha Ulata Stanley Mgao amesema changamoto kubwa inayowakabiri
ni uhaba wa zahanati, huku akiiomba serikali kukiangalia kwa jicho la huruma
kijiji hicho, kwa kuwa wananchi wake wanapata shida.
Akizungumzia
hali hiyo, diwani wa Kata ya Wasa Masumbuko Choga amesema ni kweli wananchi wa
kijiji cha Ulata na Ngonamwasi hutembea kilomita 32
kuifuata huduma ya afya, huku baadhi yao wakipoteza maisha kwa kuimosa huduma
hiyo muhimu.
“ Kata yangu
inavijiji saba, na katika vijiji hivyo saba kuna Zahanati tatu tu, Wasa,
Ihomasa na Usengerindete, na kutoka Ulata hadi Wasa ni mwendo wa km 32 kwenda
na kurudi, sasa inakuwa ni tatizo kwa akinamama wajawazito na wazee na hata
wagonjwa, kwani hata miundombinu ya barabara zetu ni changamoto kubwa ambazo
zinakwamisha hata uwepo wa usafiri,” Alisema Choga.
Aidha amesema
kumekuwa na matukio ya vifo vya wagonjwa majumbani na hata njiani wakati wakifuata
huduma na matibabu na kutokana na hilo jitihada za wananchi tayari wamefyatua
tofari kwa ajili ya kujenga zahanati katika kijiji cha Ikungwe jingo lipo hatua
ya kupauliwa na katika kijiji cha
Ufyambe mvua zikimalizika wataanza ujenzi.
Amesema ili
kukabiliana na changamoto ya vifo, wamekuwa wakiwahamasisha wananchi
kuwafikisha wagonjwa na wahitaji wa huduma ya fya mapema katika Zahanati na vituo
vya afya, kwa lengo la kuepukana na vifo vitokanavyo na ukosefu wa matibabu.
Choga ameiomba
serikali kutenga fungu la fedha za kutosha upande wa sekta ya afya, ili
kufanikisha mpango wa ujenzi wa Zahanati kila kijiji, ili kuwawezesha wananchi
kuipata huduma ya afya mapema.
Mganga mkuu wa
Wilaya ya Iringa Dr. Ignus Mlowe amesema changamoto ya umbali na miundombinu ya
barabara, na kuwa tayari wananchi kwa kutumiua nguvu zao wameanza ujenzi wa
zahanati ili kujikwamua na adha hiyo.
Dr. Mlowe
amesema Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ina Hospitali moja pekee Teule ya
Tosamaganga, Zahanati zikiwa 63 na kuwa Vituo
vya afya ni 10, na kuwa mpango mkakati wa Wilaya kufikia 2015/ 2016 ni kuwa na Vituo vya afya 14 huku kila kijiji
kikiwa na Zahanati.
Mratibu wa
chanjo mkoa wa Iringa Naftari Mwalongo akisoma taarifa ya chanjo mbele ya kaimu
mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Iringa Dr. Retisia warioba
amesema- Changamoto inayowakabiri katika utoaji wa huduma ya chanjo ni baadhi
ya halmashauri kutokufikia kiwango cha uchanjaji kwa asilimia 95 kiwango cha
kitaifa.
Mwalongo amesema
changamoto nyingine ni huduma ya mkoba kutokufanyika kikamilifu, hasa katika vijiji na vitongoji kwenye baadhi
ya Halmashauri, huku tatizo la upungufu wa watumishi waliopata mafunzo na
ujunzi wa kutoa chanjo kwenye vituo wakiwa hawaendani na ongezeko la chanjo
nchini.
Amesema kuna upungufu
wa majokofu na vifaa vingine kwa ajili
ya kuhifadhia chanjo kwa baadhi ya Zahanati, uhaba wa vyombo vya usafiri kwa ajili
ya huduma ya Mkoba “Out reach Services”.
Pia amesema kuna
wanakabiliwa na upungufu wa nishati ya Gesi kwa ajili ya majokofu ya Chanjo,
huku baadhi ya vituo kutokufikika hasa wakati wa masika, na hivyo baadhi ya
watoto kutokufikiwa na huduma hiyo muhimu ya chanjo.
Hata hivyo
Mwalongo amesema pamoja na changamoto hizo mkoa umeweza kufanya jitihada za
kuimarisha huduma na ulinzi elekezi katika Halmashauri na vituo vya kutolea
huduma, kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya chanjo katika mpango kabambe wa
huduma za afya kwa halmashauri.
Na kuwa mkoa
umezishauri Halmashauri kutenga fedha kwenye bajeti zao kwa ajili ya kununua
majokofu pamoja na nishati ya Gesi na kuajiri watumishi wenye elimu na ujuzi wa
kutosha.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni