INAFAHAMIKA Kuwa afya ni suala mtambuka, ambalo kama litaenda mrama iwe kwa uzembe, kupuuzia au kwa kukosa kipato cha kuboresha mazingira, linaweza kugharimu usalama wa maisha na hata kusababisha kifo.
Wanafunzi wa shule
ya sekondari Malangali, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi- mkoani
Iringa, wao wapo katika hatari yakupata magonjwa ya mlipuko, yatokanayo na
uchafu, ukiwemo ugonjwa wa Kipindupindu,
na hiyo ni kutokana na vyoo vya shule hiyo ya sekondari ya Malangali kuwa na uchafu
uliokithiri.
Miundombinu duni
ya mazingira ya shule hiyo inatokana na uchakavu mkubwa uliopo, na hiyo
nikutokana na shule hiyo kuwa na zaidi ya miaka 50 tangu ianze kutoa elimu
mwaka 1928, licha ya ukweli kuwa ukongwe wa shule hiyo hauna thamani kwani ni
kama imetelekezwa.
Wakizungumzia
hali halisi ilivyo na namna wanavyokabiliana na mazingira ya shule hiyo,
ewanafunzi wa shule ya sekondari Malangali wamesema usalama wa maisha yao- sasa
wameukabidhi mikononi mwa mwenyezi Mungu na hiyo ni kutiokana na tatizo la vyoo
kuwa ni sugu.
Kwa hali ya kawaida
uchafu haujitengi na wadudu wanaopenda mazingira ya aina hiyo, kwani wanafunzi
wa shule ya sekondari Malangali kwa sasa wanalazimika kulala Sakafuni na
kuviacha vitanda kwa kuhofia taabu ya kuteswa na wadudu wanaoitwa Kunguni, huku
baadhi yao wakikimbia mabweni na kuhamia katika vyumba vya madarasa kwa hofu
hiyo ya Kunguni.
Shule ya
sekondari Malangali ni miongoni mwa shule kongwe nchini ambazo zinajivunia
kutoa viongozi mbalimbali hususani wa ngazi za juu serikalini, lakini mazingira
yaliyopo hayawiani na sifa ya shule hiyo.
Thomson Ngunyali
ni mkuu wa shule ya sekondari Malangali, anakiri kuwepo na changamoto ya
miundombinu dhaifu ya vyoo na kuwa idadi ya vyoo vilivyopo ambavyo vilijengwa
mwaka 1928 vilikuwa kwa ajili ya wanafunzi 280 na sasa wapo zaidi ya wanafunzi
700 – mara tatu ya idadi iliyotarajiwa awali.
Kuhusiana na changamoto
ya wadudu Kunguni Mwalimu Ngunyali anasema uongozi wa shule umeanza kulifanyia
kazi tatizo hilo, kwakupilizia dawa za kuua wadudu, licha ya kuwa wadudu haoi
wamekuwa wakiibuka mara kwa mara.
Hali ya
wanafunzi kimalazi katika Mabweni ya wanafunzi wa shule ya sekondari Malangali
ni tishio kwa sasa, kwani wanafunzi kila asubuhi hulazimika kutoa vitanda nje
ili kuwaua wadudu kwa njia mbadala ya nishati ya jua, huku dali la bweni nalo liking’olewa
kama ni sehemu ya kutafuta mwarobaini wa kukabiliana na wadudu hao ambao
chakula chao kikuu ni damu ya binadamu au mnyama yeyote awaye.
Changamoto hizo
zimeainishwa na wanafunzi, katika mahafali ya 18 ya kidato cha sita wa shule hiyo ya sekondari ya Malangali, ambapo
jumla ya wanafunzi 96 wameingia katika mtihani wa kuhitimu elimu yao ya kidato ycha
sita, katika shule hiyo ambayo inasifa ya kuwa na ufaulu mzuri, ikiongozwa na
sekondari ya wasichana ya Igowole zote za Mufindi- Iringa.
Albert Chalamila
muhadhiri wa chuo kikuu cha Iringa (Tumaini) miongoni mwa wanafunzi waliosoma
katika shule hiyo ya Malangali sekondari, aliyehudhuria mahafali hayo kama mgeni
rasmi wa mahafali hayo ya 18 ya kidato cha sita shuleni Malangali, amesema kuna
umuhimu wa kufanya kongamano la wanafunzi waliosoma katika shule hiyo, lengo
likiwa ni kuichangia shule hiyo ili kunusuru majengo yake yasianguke na
kupoteza Historia nzuri ya shule hiyo.
Hata hivyo
Malangali sekondari shule ni shule ya Serikali inayotoa elimu kwa wanafunzi wa
kiume, huku safu kubwa ya viongozi wa ngazi za juu wakiwa wa,mepata elimu katika
shule hiyo, elimu ambayo kwa sasa imeyopelekea mafanikio ya wao kuwa katika
ngazi hiyo za juu za uongozi.
Basi kuna
umuhimu kwa waliosoma katika shule hiyo ya Malangali Sekondari- kukumbuka
fadhila na kuigeukia shule hiyo, lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za
serikali za uanzishwaji wa shule- jitihada ambazo leo zimezaa matunda kwa
kuwapata viongozi hao waliotokana na shule ya sekondari Malangali.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni