Zao la Pareto likiwa Shambani.
Ramani ya Tanzania ikionyesha mikoa ambayo inalima zao la Pareto
Kushoto ni Ephraem Mhekwa Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Pareto akiwa na Gerlad Chuwa (Kulia) ambaye ni mdhibiti wa zao la Pareto nyanda za juu kusini.
Ephraem Mhekwa Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Pareto akiwa na Gerlad Chuwa (mwenye miwaniKulia) ambaye ni mdhibiti wa zao la Pareto nyanda za juu kusini.
Semu Kalekezi mtaalamu wa maabara ya Pareto akiwa na Tumaini Ngajilo (Mwenye kofia) Mtakwimu bodi ya Pareto akitoa maelezo juu ya bidhaa zitokanazo na zao la Pareto.
Semu Kalekezi mtaalamu wa maabara ya Pareto.
Shamba la Pareto.
Kutoka kulia ni Semu Kalekezi, mtaalamu wa maabara (katikati) ni Innocent Mogha na wakwanza kushoto ni Tumaini Ngajilo mtakwimu wa bodi ya pareto, wakiwa katika shamba la Pareto.
Kutoka kulia ni Semu Kalekezi, mtaalamu wa maabara
(katikati) ni Innocent Mogha mkaguzi wa zao la Pareto, na wakwanza kushoto ni Tumaini Ngajilo
mtakwimu wa bodi ya pareto, wakiwa katika shamba la Pareto.
Semu Kalekezi, mtaalamu wa maabara.
Innocent Mogha mkaguzi wa zao la Pareto.
Tumaini Ngajilo
mtakwimu wa bodi ya pareto.
Pareto ikiwa shambani
Bango likionyesha hatua za shughuli za kilimo cha zao la Pareto, kuanzia shambani hadi kusafirisha kwenda nyumbani na namna ya kuanika.
HABARI.
TANZANIA
imeng’ara katika soko la dunia kupitia zao la Pareto, zao ambalo
baadhi ya wakulima wameligeuzia kisogo, licha ya zao hilo kuwa na mauzo mazuri kwa kilo,
ukilinganisha na mazao mengine ambayo yamezoeleka.
Hayo yamezungumzwa
na Ephraem Reuben Mhekwa, ambaye amesema kwa sasa Tanzania ipo juu kwa kuuza zao
hilo la Pareto kwa kiwango kikubwa katika soko la dunia, huku bei ya kilo moja
ya Pareto ikipaa kulingana na kiwango cha sumu kilichopo katika maua ya zao
hilo.
Mhekwa amesema Tanzania imefanikiwa kukusanya tani
elfu 6700 za zao la Pareto, na kuwa miongoni mwa nchi chache zinazofanya vizuri
kwa kulima zao hilo, huku ikiipita nchi ya Kenya ambayo awali ilikuwa ni bora
zaidi, huku kilo moja ikifikia zaidi ya shilingi 1500 hadi 2500.
Amesema Kenya
awali ilikuwa inaongoza kulima zao hilo na sasa wamefikia tani 2000 pekee huku Tanzania ikifikia tani elfu 6700 na
mahitaji ya dunia yakiwa ni tani elfu 20 za Pareto kwa mwaka, huku Pareto
iliyopatikana ni tani elfu 13200.
Amesema zao la Pareto
kwa takwimu za kuanzia june 30 liliingiza zaidi ya dola milioni 10 hadi 15, na
kuwa asilimia 90 ya soko la Pareto lipo nchini Marekani na sasa Mmarekani huyo amenunua
kiwanda cha Mafinga.
Amewasihi wakulima
kuchangamkia fulsa hiyo, kwa kulima zao hilo kwa wingi, licha ya kukabiliwa na changamoto
katika uendeshaji wa kilimo cha zao hilo la Pareto, hasa katika upatikanaji wa Pembejeo na vikaushio.
Mhekwa ameitaja Mikoa
inayolima zao la Pareto kwa Wingi Tanzania kuwa ni Mbeya, Njombe, Manyara, Arusha, Kilimanjaro,
na mkoa wa Iringa, huku mkoa wa Rukwa, Moro, Ruvuma, Kagera na mkoa wa Tanga kwa sehemu ya Rushoto, ikiwa imefanyiwa
utafiti amb ao umeonyesha uwezo wa kulima zao hilo.
Mhekwa amesema Changamoto
kubwa kwa upande wa wakulima ambo ndiyo wazazilishaji wa zao hilo ni upatikanaji wa pembejeo hasa mbegu,
vitendea kazi vya kukaushia Pareto, kwani zao hili hulimwa katika maeneo yenye
baridi, na hivyo hatua ya ukaushaji ukitakiwa
kuwa niwa umakini zaidi.
Aidha amesema
Sekta ya Pareto imeanzisha mfuko wa kuendeleza zao la Pareto, mfuko
unaochangiwa na wakulima, wafanyabiashara, Halmashauri na serikali kuu na lengo
kuu la mpango wa mfuko huo ni kugharamia utafiti, nyenzo za kufanyia kazi kama
vikausha nk ili kuwawezesha kupata Pareto bora zaidi.
Aidha katika mkutano huo mkuu, mfuko wa kuendeleza kilimo
cha zao la Pareto, umeadhimia kupandisha
kiwango cha bei ambacho kitajikita katika ubora, huku azimio likiwa ni wakulima watakaozalisha Pareto nzuri watalipwa bei nzuri na
watakaozalisha Pareto mbaya, wataadhibiwa
kwa ubaya wa Pareto yao.
Amesema hatua hiyo
imelenga pia kuongeza hamasa ya kuitunza vizuri Pareto tangu ikiwa shambani
mpaka inapofikia hatua ya kuuzwa, ambapo makubaliano yaliafikiwa kuwa kilo moja
ya Pareto yenye ubora wa 0.9 italipwa kiasi cha shilingi 1500 na Pareto yenye ubora
wa 1.8 na kuendelea italipwa kiasi cha shilingi 2500 kwa kilo moja.
Amesema matumizi
ya kuzalisha zao la Pareto ni kupata Sumu inayopatikana katika maua ya Pareto, sumu ambayo hutumika kuulia wadudu waharibifu wa
shambani na nyumbani na katika mazingira yanayozunguka nyumba, huku sumu hiyo
ikidaiwa kutokuwa na madhara yoyote kwa afya ya binadamu yeyote.
Amesema changamoto
inayowakabiri wanunuzi ni uwezo mdogo wa kumiliki vifaa vya kukamulia/
kuzindulia Pareto, kwani sheria inawataka wanunuzi kuwa na mitambo ya kuengua
sumu kwa kuwa mitambo hiyo inapatikana kwa gharama ya zaidi ya dola milioni 1
na hali hiyo imesababisha kuwepo kwa mnunuzi mmoja pekee aliyekidhi vigezo
hivyo, mnunuzi ambaye anapatikana Mafinga – Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Pia amesema changamoto
nyingine inayowakabiri wanunuzi ni ufinyu wa soko la Pareto kwa kuwa soko kubwa linalotegemewa
ni nchi ya Marekani, Ulaya, huku wafanyabiashara wadogo soko lao kubwa likipatikana
katika nchi ya Ruanda, Kenya na China.
Kwa upande wa
bodi amesema changamoto kubwa inayowakabiri ni uhaba wa fedha na vitendea kazi kutotoshereza
shughuli za utafiti, kwakuwa Fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kufanyia
utafiti hazitosherezi, na hiyo ni kutokana na zao hilo kuhitaji utafiri wa mara
kwa mara.
“Sisi kama bodi
tunashirikiana na mfuko wa kuendeleza zao la Pareto, ambapo fedha asilimia 30
zilizopatikana kutokana na michango huwasaidia wakulima kupatikana kwa mbegu na kugharamia
utafiti.
Amesema tangu zao
hilo liingie hapa nchini mwaka 1930 mpaka sasa kuna aina chache tu za Pareto
kwa ajili ya kufanya utafiti ili kupata ubora wa sumu inayokubarika katika zao hilo.
Amesema matumizi
ya Sumu ya Pareto ni kuulia wadudu kama Nzi, Mbu na mazalia yake, na mabaki yake au machicha hutumika kwa ajili ya chakula cha mifugo, huku sumu chache iliyopo katika mabaki au mashudu hayo husaidia
kuua minyoo na wadudu waliopo katika
tumbo la mnyama/mfugo.
Na kuwa mafuta yanayofahamika
kama “Pay Gris” hutumika kupambana
na wadudu wanawashambulia mifugo, kama
Ng’ombe, Mbuzi, Nguruwe, paka, wadudu kama Kupe, Viroboto nk.
“Kwa bahati
mbaya sana Kiwanda kimejengwa katika eneo ambalo uzalishaji wa Pareto ni hasi,
sio mkubwa sana, na kiwanda hicho kimejengwa tangu mwaka 1980 Mafinga katika
Wilaya ya Mufindi, wakitarajia wakulima watachangamkia kulima Pareto, lakini
kwa bahati mbaya wananchi wa Wilaya ya Mufindi hawana mwamko wa kulima zao hili
la Pareto, na hii ni kutokana na wakulima kuwa na mazao mengine mbadala, kama
zao la Chai na zao la Miti,” Amesema Mhekwa.
Hata hivyo Mhekwa
ametoa wito kwa wakulima kuendesha kilimo kwa kuendana na ubora ili kulifanya
zao kuwa na tija kwao kwa kuwaletea maendeleo na kulitangaza Taifa la Tanzania.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni