Baadhi ya majengo ya chuo kikuu cha Iringa zamani kilifahamika kama Tumaini.
Tula Tweve, Muhadhiri wa Kiswahili chuo kikuu cha Iringa (Tumaini) akizungumza na wanafunzi wa chuo siku ya uzinduzi wa chama cha wanafunzi wa Kiswahili wa vyuo vikuu Afrika Mashariki.
Albert Chalamila mkuu wa idara ya Lugha na Stadi za mawasiliano, akizungumza na wanachuo siku ya uzinduzi wa chama
cha wanafunzi wa Kiswahili wa vyuo vikuu Afrika Mashariki.
Enock Ugulumo - naibu makamu mkuu wa chuo utawala na fedha chuo kikuu cha Iringa, akitoa wosia kwa wanafunzi wa Kiswahili Afrika mashairiki, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu cha Iringa.
Dr. Newton Kyando mkuu wa kitivo cha Sayansi na taaluma za ualimu, akizungumza na wanafunzi wa chuo siku ya uzinduizi wa chama
cha wanafunzi wa Kiswahili wa vyuo vikuu Afrika Mashariki.
Gervas Amos- Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa, akizungumza na wanafunzi wa chuo siku ya uzinduizi wa chama
cha wanafunzi wa Kiswahili wa vyuo vikuu Afrika Mashariki.
Keki ikikatwa kuashiria uzinduzi wa CHAWAKAMA.
Keki ya uzinduzi wa CHAWAKAMA.
Tula Tweve, Muhadhiri wa Kiswahili chuo kikuu cha Iringa (Tumaini)
akiandika kumbukumbu za changamoto zinazotolewa na wanafunzi katika hafla ya uzinduzi wa chama cha wanafunzi
wa Kiswahili wa vyuo vikuu Afrika Mashariki.
Aggnes Ernest Kowi mmoja wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa, akiwa na wenzake katika hafla ya uzinduzi wa CHAWAKAMA.
Baadhi ya wanafunzi washiriki wa hafla hiyo wakisikiliza jambo katika siku hiyo ya Uzinduzi wa CHAWAKAMA.
Philicanus Lukinga. Mwenyekiti mstaafu wa chama cha Kiswahili chuo kikuu cha Iringa (Tumaini), akiwa katika hafla hiyo, kulia ni Tula tweve muhadhiri wa Kiswahili chuo kikuu cha Iringa.
Baadhi ya wanafunzi washiriki wa hafla hiyo wakisikiliza jambo katika siku hiyo ya Uzinduzi wa CHAWAKAMA.
Baadhi ya wanafunzi washiriki wa hafla hiyo wakisikiliza jambo katika siku hiyo ya Uzinduzi wa CHAWAKAMA.
<<<HABARI>>>.
CHAMA cha wanafunzi wa
Kiswahili, wa vyuo vikuu Afrika mashariki (CHAWAKAMA), kimeitaka jamii kutumia
lugha ya Kiswahili, katika mawasiliano, ili kuitangaza zaidi Tanzania katika
mataifa mengine.
Hayo yamezungumza na wanachuo,
katika uzinduzi wa chama hicho cha CHAWAKAMA, uliofanyika katika ukumbi wa chuo
kikuu cha Iringa (Tumaini) kilichopo manispaa ya Iringa., uzinduzi
uliohudhuriwa na wasomi mbalimbali.
Dr. Newton Kyando mkuu
wa kitivo cha sayansi na taaluma za ualimu amesema Kiswahili ni hazina ya
maendeleo, na kuwa Lugha hiyo ni zaidi ya utamaduni ambao unaweza kukuza soko
na hivyo kuinua uchumi wanchi.
Dr. Kyando amesema
katika kioo cha utandawazi Lugha hiyo ya Kiswahili inaonekana kuwa ni nyenzo ya
kiuchumi, na hivyo cham hicho kionekane kama ni chama cha watumiaji wa Lugha ya
Kiswahili, pasipo kuwaachia wanafunzi wa Kiswahili pekee.
Aidha amesema lugha
hiyo si tunu pekee ya watanzania bali niya sfrika mashariki, na inapaswa
kulindwa na kutoiona kama ni lugha au somo pekee, hatua ambayo jamii inaiona
lugha hiyo niya wasomi pekee, huku akiwataka wataalamu wa lugha kuondoa dhana
ya kuwa Kiswahili ni finyu na hakijitosherezi.
Albet Chalamila mkuu wa
idara ya Lugha na stadi za mawasiliano amesema Kiswahili kinapaswa kutumika
kama lugha ya maarifa, na si kama inavyoonekana sasa kuwa ni lugha ya
mawasiliano pekee.
Chalamila amesema
wasomo wanatakiwa wasipindishe lugha hiyo kwa makusudi , huku akiiasa jamii
kuacha kasumba ya kusahau utaifa wao kwa kuthamini lugha za kigeni ambazo
baadhi yake hazina uwanja mkubwa kama ilivyo kwa lugha hiyo ya Kiswahili.
“Hoja yangu ya msingi
hapa ni kuwa tunapaswa kuifahamu vyema lugha ya Kiswahili lakini pia tunapaswa
kuifahamu vyema lugha ya kiingereza, kwa sababu moja tu ya kozi ya sarufi
linganishi,” Amesema Chalamila.
Naye muhadhiri wa
Kiswahili wa chuo kikuu cha Iringa Tula tweve, amesema watanzania ifike wakati
waepukane na dhana ya kuwa Kiswahili ni somo dhaifu tofauti na masomo mengine,
na kuwa somo la Kiswahili ni somo bora.
Tweve ametoa wito kwa
wajumbe wa bunge la katiba, viongozi pamoja na wananchi kuzingatia matumizi
bora na sahihi ya lugha ya Kiswahili nchini, kwa madai kuwa lugha hiyo ni Lulu
ya Taifa, na kutoegemea lugha nyingine za kigeni.
“Nitoe wito hasa katika
mchakato huu wa katiba mpya, wajumbe wa bunge la katiba, viongozi mbalimbali
pamoja na wananchi wote kwa ujumla, natamani sana kipengele moja wapo katika
katiba kikazingatia matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili, nina maana katika
Nyanja zote hasa Nyanja ya kielimu,” amesema Tweve.
………..Wanazuoni
mbalimbali na wanachuo mbalimbali siyo kwamba wanashindwa kufaulu katika masomo
yao siyo kwamba hawana uwezi, hapana!!Kwa sababu lugha ya Kiswahili ni lugha
yao ya Taifa ambayo wanaitumia kila siku katika shughuli mbalimbali, lakini
lugha hii endapo ingekuwa inatumika katika mtaala kuanzia shule ya msingi hadi
vyuo vikuu naamini tungekuwa tunawanazuoni bora zaidi kuliko lugha nyingine,” Alisema.
Enock Ugulumo - naibu makamu mkuu wa chuo utawala na fedha chuo kikuu cha Iringa,amesema wanafunzi wanapaswa kujifunza lugha kwa ufasaha zaidi ili wawe wa kimataifa wakubalike kwa kuwafunza na wageni kutoka nje ya nchi wanaokuja nchini.
Ugulumo amesema Kiswahili kikichukuliwa kwa hali halisi na kuthaminiwa kitaongeza nafasi kubwa za ajira kwa watanzania, kwani ni lugha niya utandawazi inayokuza biashara kimataifa.
Kenneth Komba afisa
michezo mkoa wa Iringa ambaye alikuwa mgeni rasmi wa uzinduzi huo wa CHAWAKAMA
amesema hata mikataba mibovu inayoingiwa na baadhi ya viongozi nchini
inatokana na changamoto ya lugha.
“Unakuta kitabu kina
kurasa zaidi ya miamoja, kiingereza chenyewe cha kuokotaokota, kwa sababu lugha siyo yakwetu, unasaini mambo mengine
kumbe ni bomu, lakini kama ingekuwa inatumika lugha ya Kiswahili ambayo
tunaielewa vyema hizo changamoto ambazo zipo kwenye mikataba ingekuwa rahisi
kuzibaini,” Alisema Komba.
Hata hivyo amesema
katika suala la kudidimiza Kiswahili, hakuna mtu wa kurushiwa lawama, kwani wao
wasomi ndiyo wanaongoza katika kuidharau lugha hiyo, kwa kutokizungumza mara
kwa mara, na badala yake wamekuwa wakitumia zaidi lugha za kigeni ili kujikweza
na kujitofautisha na watu wengine.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni