Baadhi ya akinamama wajawazito wakiwa wodini, katika Hospitali ya Mafinga ya Wilaya ya Mufindi- mkoani Iringa.
Kitanda kimoja wanalala wajawazito watatu, na hiyo ni kutokana na uhaba wa vitanda uliopo katika Hospitali hiyo.
Baadhi ya akinamama wajawazit.
"Kitanda hiki ni halali kulalia mgonjwa mmoja, lakini wanazimika kulala wajawazito watatu, licha ya hali walizonazo, wanabanana mno".
"Hapa chini wanapolala usalama kiafya ni mdogo kwao, pia hata kwa watoto wao watarajiwa, kwani ni vyepesi kupata maambukizi ya maradhi hasa kwa mtoto mchanga" lakini tatizo lingine ni uhaba wa mashuka, kwani kila mgonjwa ametandika Khanga, Kitenge au shuka katika eneo lake la kulala.
Naibu Waziri wa maliasili na Utalii Mahamood Mgimwa, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini akizungumza jambo katika uzinduzi wa jengo la wodi ya wajawazito na watoto wachanga katika Hospitali ya Mafinga - Mufindi. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu, wakatikati ni mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mufindi na MNEC Taifa Marcellina Mkini, kushoto ni mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Willium Ntinika wakisikiliza jambo kwa umakini katika uzinduzi wa wodi hiyo ya akinamama wajawazito Wilayani Mufindi.
Moja ya eneo majengo ya zamani ya Hospitali ya Wilaya ya Mafinga.
<<<HABARI>>>
AKINAMAMA
wajawazito wanaofika kupata huduma katika Hospitali ya Mafinga iliyopo Wilaya
ya Mufindi mkoani Iringa, wanalazimika kulala Sakafuni, kutokana na Uhaba mkubwa wa vitanda unaoikabiri Hospitali
hiyo.
Wakizungumzia
adha wanayoipata, wajawazito hao wamesema tatizo la vitanda linawafanya baadhi
yao kulala watatu katika kitanda kidogo ambacho niche mgonjwa mmoja.
Maula Kifwe
amesema hali hiyo kwake inamsumbua kwani kila asubuhi amekuwa akiumwa mgongo,
na hivyo kuwa na hofu juu ya tatizo hilo ambalo hakutokanalo nyumbani wakati
anakwenda kupata huduma katika Hospitali hiyo.
Naye Anna
Ngalalekumtwa amesema hali walizonazo za ujauzito, na mbanano uliopo katika
wodi ya Hospitali hiyo, ni hatari kwa viumbe vyao vilivyopo tumboni, kwani
kitanda wanacholalia wagonjwa watatu ni kidogo na kinastahili kulala mjamzito
mmoja pekee.
Pelida Mkakanzi
naye amesema hali hiyo inasababisha baadhi ya vichanga kuanguka na hivyo kuwa
katika hatari ya kupata ulemavu watoto hao, kwani uangalizi unakuwa mdogo
kutokana na mbanano uliopo.
“Madhara
tunayoyapata hapa yanayoonekana ni zaidi ya yake yasiyonekana, kwa maana hapa
tunapata maradhi ya kuambukizana, jambo ambalo ni hatari, lakini ni hatari
zaidi kwa watoto wachanga, kama unavyoona tumebanana hivi, na sisi ni
wajawazito, kweli tunaiomba serikali
itusaidie vitanda, maana hii ni hatari kubwa sana,” Walisema.
Akitoa taarifa
za changamoto zinazoikabiri Hospitali hiyo, katika uzinduzi wa wodi ya wazazi
na watoto wachanga, Mganga mkuu wa Hospitali hiyo ya mafinga Dr. Eugene Lutambi
amesema tatizo lililopo ni uhaba wa vitanda kwani jengo hilo linahitaji jumla
ya vitanda 80 ili kukidhi mahitaji ya wajawazito.
Dr. Lutambi
amesema zaidi ya shilingi Milioni 800 (mianane)
zinahitajika kwa ajili ya kununuliwa vifaatiba, vikiwemo vitanda, ili
kukamilisha huduma za uzazi katika wodi hiyo mpya iliyogharimu jumla ya
shilingi Milioni 302.
Pia Dr. Lutambi
amesema changamoto iliyopo ni msongamano wa akinamama wajawazito wodini, ambao
wanalazimika kulala zaidi ya mmoja katika kitanda kimoja na kuwa kuna kipindi
wengine hulala chini.
Amesema wodi ya
awali ilikuwa ni ndogo zaidi ambayo ilikuwa na uwezo wa kuchukua vitanda 28
pekee, na kuwa kukamilika kwa jengo hilo ni msaada mkubwa utakaopunguza
mrundikano wa wagonjwa na hivyo wahudumu kufanya kazi katika mazingira bora.
Hata hivyo
amesema licha ya kukamilika kwa jengo hilo bado tatizo la upungufu wa vitanda
linabaki pale pale, kwani vitanda vilivyowekwa katika jengo hilo jipya ni vile
vilivyokuwa katika wodi nyingine.
Amesema wodi
hiyo yenye uwezo wa kulaza wajawazito 60 hadi 80 licha ya kukabiliwa na uhaba
wa vitanda, pia halina vifaatiba jambo linalokwamisha utoaji wa huduma bora
ambazo zimekusudiwa.
Na kuwa ..."Jengo hili linachumba cha upasuaji (Theatre), chumba cha akinamama wanaosubiri kujifungua (Antenatal room), chumba cha akinamama ambao tayari wamejifungua (Postnatal room), chumba kwa ajili ya watoto waliozaliwa kabla ya muda (Premature babies room), vyumba kwa ajili ya ofisi za madaktari na manesi, chumba cha kuzalia (Labour room) na pia kuna chumba cha kufulia nguo za wagonjwa.walio," alisema Dr. Lutambi.
Uzinduzi wa wodi huo umehudhuriwa na Naibu waziri wa maliasili na utalii, Mahamood Mgimwa, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni