Nahodha wa timu ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Ruaha RUCO cha mjini Iringa Said Mohamed, akiwa na kombe la ushindi wa Pool table (mchezo wa meza) kitaifa, mashindano yaliyoandaliwa na kampuni ya bia ya Tanzania Breweries Limited TBL.
Said Mohamed- akiwa na baadhi ya wachezaji wa RUCO wenye furaha kwa kulinyakua kombe hilo kitaifa, baada ya kuzigalagaza zaidi ya timu 10 zilizoshiriki katika mashindano hayo ya POOL yaliyodhaminiwa na kampuni ya TBL, kupitia kinywaji chake cha bia ya SAFARI.
Mmoja wa wachezaji wa timu ya chuo kikuu cha RUCO akionyesha medali ya ushindi na kombe walilolitwaa katika mashindano ya mchezo huo ambao ulishirikisha zaidi ya timu 10 nchini.
Nahodha wa timu hiyo ya RUCO Said Mohamed.
"Tumelichukua kombe, sisi ni washindi" Ni kama wanajinasibu wakiwa na kombe lao.
Meneja mauzo wa kampuni ya TBL. Reymond Degera akizungumza na washindi hao, katika hafla ya kuwapongeza washindi, iliyoandaliwa na kampuni hiyo ya TBL kupitia kminywaji chake cha SAFARI, ambayo ilifanyika katika Hotel ya GENTLE HILL, Gangilonga mjini Iringa.
Reymond Degera akizungmza na washindi wa POOLTABLE
Waziri wa sheria na Katiba wa serikali ya chuo kikuu cha RUAHA ..RUCO Paul Mligo akitoa neno juu ya ushindi huo, kwa kampuni ya TBL huku akitoa wito kwa wanachuo na washindi wa kombe hilo kitaifa.
Baadhi ya wageni waalikwa, wakiwa katika hafla hiyo, iliyofanyika katika Hotel ya GENTLE HILL ya mjini Iringa, hafla ya kuwapongeza washindi wa POOLTABLE chuo kikuu cha RUCO.
Waziri wa katiba na sheria Paul Mligo.
Afisa michezo mkoa wa Iringa Kenneth Komba, akizungumza jambo katika hafla ya kuwapongeza wanafhunzi wa chuo kikuu cha RUCO, walioshinda kombe la mchezo wa Poooltable
Afisa michezo mkoa wa Iringa Kenneth Komba.
Mgeni rasmi wa hafla hiyo kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhan Mungi akitoa neno kwa washindi.
Kombe la ushindi wa mchezo wa Pooltable.
Viongozi mbalimbali wakiwa katika meza kuu, wakisikiliza ujumbe kutoka kwa viongozi wa timu ya RUCO.
"Tunawasikiliza kwa makini sana washindi wetu mliotuletea heshima katika mkoa wa Iringa" Ni kama wanasema viuongozi wa meza kuu, katika hafla ya kuwapongeza wanachuo wa RUCO kwa kunyakua kombe la Kitaifa la Pooltable.
Mwandishi wa habari nguri wa gazeti la Tanzania Daima, Denis Mlowe, akiwa na mwanahabari kutoka jijini Dar es salaaam Bw. Machella wakijipongeza mara baada ya kumaliza kazi yao, katika Hotel ya GENTLE HILL katika hafla ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya chuo kikuu cha Ruaha RUCO cha mjini Iringa.
Kombe la ushindi wa mchezo wa Pool lililotolewa na kampuni ya bia nchini ya TBL, ambalo limenyakuliwa na timu ya chuo kikuu cha RUCO, likitembezwa mjini Iringa kuihamasisha jamii kupenda michezo hasa mchezi huo wa Pool.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni