Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Tosamaganga- Iringa
Viongozi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakiwa na baadhi ya walimu wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiana vitabu. Meneja wa kampuni ya Airtel Beda Kinunda akitoa ufafanuzi juu ya msaada huo wa vitabu kwa shule hiyo ya sekondari ya wavulana ya Tosamaganga.
Afisa mauzo (Biashara) wa kampuni ya Airtel mkoa wa Iringa Hudson Kamenya akiwa shuleni hapo Tosamaganga. Mkuu wa shule ya sekondari Tosamaganga - Iringa Damas Mgimwa akipokea baadhi ya vitabu kutoka kwa afisa mauzo wa kampuni ya Airtel Hudson Kamenya. Mmoja kati ya wanafunzi wa sekondari Tosamaganga akipokea baadhi ya vitabu vya masomo ya Hisabati na Sayansi. Mmoja kati ya wanafunzi wa sekondari Tosamaganga akipokea baadhi ya vitabu vya masomo ya Hisabati na Sayansi.
Mmoja kati ya wanafunzi wa sekondari Tosamaganga akipokea baadhi ya vitabu vya masomo ya Hisabati na Sayansi.
Mmoja kati ya wanafunzi wa sekondari Tosamaganga akipokea baadhi ya vitabu vya masomo ya Hisabati na Sayansi.
Baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya Tosamaganga wakiwa na vitabu, walivyokabidhiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel
Baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya Tosamaganga wakiwa na vitabu, walivyokabidhiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel.
Meneja wa Airtel mkoa wa Iringa Beda Kinunda akimkabidhi Box la Vitabu mkuu wa shule ya sekondari Tosamaganga damas Mgimwa Meneja wa Airtel mkoa wa Iringa Beda Kinunda akimkabidhi Box la Vitabu mkuu wa shule ya sekondari Tosamaganga damas Mgimwa
Mkuu wa shule ya Sekondari Tosamaganga - Damas Mgimwa akishuhudia wanafunzi wakishangilia msaada huo wa vitabu kutoka kampuni ya Airtel.
<<<HABARI>>>
KAMPUNI ya simu za mkononi ya
Airtel imekabidhi vitabu vya masomo ya Sayansi, kwa wanafunzi wa shule ya
sekondari ya Tosamaganga, kwa lengo la kupungua ukali wa tatizo la vitabu shuleni
hapo.
Akikabidhi
msaada huo meneja wa kampuni ya Airtel mkoa wa Iringa Beda Kinunda amesema
kampuni yake imejiwekea mikakati ya kusaidia sekta ya elimu, kwa kutoa vitabu
ambavyo ni tatizo sugu kwa shule nyingi za sekondari hapa nchini.
Kinunda amesema Airtel imetoa msaada huo kupitia mpango wa “Shule yetu” ambapo kampuni hutoa msaada wa vitabu vya masomo ya
sayansi kwa shule zenye uhitaji - lengo likiwa ni kuinua kiwango cha elimu
nchini.
Hudson Kamenya-
Afisa biashara wa Airtel mkoa wa Iringa
na kuwa shule ya Tosamanganga ni kati ya shule zenye changamoto za
vitabu na Tosamaganga ni shule yenye bahati zilizochaguliwa na kampuni hiyo.
Hiraly Sandagila
mwalimu wa taaluma Tosamaganga amesema kuna upungufu mkubwa wa vitabu vya
masomo ya Sayansi, Somo la Physicia kuna vitabu 23 uhitaji ni 3527 na hisabati 24
ambapo kitabu kimoja uwiano nikwa
wanafunzi 17 huku uhitaji 529.
Sandagila
amesema kwa somo la Chemia kuna afadhari kwani vitabu vilivyopo ni 300 huku mahitaji
yakiwa vitabu 100 na vitabu vya Biologia vipo 38 mahitaji ni zaidi ya vitabu 260,
na kuwa msaada huo utasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa vitabu hususani
vitabu vya Hesabu na Pysicia.
Sandagila ameishukuru
kampuni ya Airtel kwa kuliona tatizo hilo, kwa madai kuwa baadhi ya wanafunzi
wanmwamko wa elimu lakini wamekuwa wakikwamisha na hali ya upungufu wa vitabu,
na hivyo kushindwa kujisomea.
Mkuu wa shule
hiyo ya Sekondari Tosamaganga Damas
Mgimwa amewataka wanafunzi hao kuvitunza vitabu hivyo ili viwasaidie kujisomea
zaidi na kuongeza kiwango cha ufaulu.
Nao wawakirishi wa wanafunzi hao
wa sekondari ya Tosamaganga - Dominic Kamugisha na Frolian Mwebesa wameishukuru kampuni
hiyo ya Airtel kwa msaada huo.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni