Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) Wilaya yab Kilolo akisikiliza jambo kutoka kwa walimu, katika mkutano mkuu ambao hufanyika kila baada ya miaka miwili na nusu.
Baadhi ya walimu wilayani Kilolo wakiandika kumbukumbu za kikao hicho kilichofanyika Wilayani humo _Kilolo.
Wakifuatilia jambo kwa umakini mkubwa.
Mmoja kati ya viongozi wa CWT akifafanua jambo katika mkutano mkuu wa CWT Wilayani Kilolo.
<<<<HABARI>>>>
CHAMA cha walimu Tanzania CWT kimetoa siku 15 kwa
Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, kurejesha fedha za walimu zaidi ya shilingi Milioni 80, zilitolewa
na serikali kwa ajili ya kupunguza deni la
walimu wilayani humo.
Wakizungumzia hali hiyo katika mkutano mkuu ambao hufanyika
kila baada ya mika miwili na nusu, CWT imesema baada ya serikali kupunguza
madeni inayodaiwa na walimu Wilayani humo, Halmashauri ya wilaya ya kilolo
imechepusha fedha hizo na hivyo walimu wake kutopata madai yao.
Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Kilolo, Stansilaus
Muhongole amesema fedha hizo ambazo zimepotelea mikononi mwa Halmashauri hiyo,
zinatakiwa kurudishwa haraka ndani ya siku 15, lasivyo CWT itaiburuza Halmashauri hiyo
katika baraza la Mahakama ya kazi.
“Fedha hizo ziliingia kwenye mtandao zikiwa ni malipo ya walimu wa elimu ya msingi
kwa minajiri ya Serikali kupunguza deni lake, lakini baada ya Halmashauri
kupata fedha hizo ikapeleka kulipa deni la Udzungwa badala ya kuwalipa walimu,
huu ni unyanyasaji mkubwa kwa walimu, jambo hili hatutakubari,” Alisema Muhongole.
Aidha Muhongole amesema Halmashauri inatakiwa kurudisha fedha
hizo ndani ya siku 15, la sivyo CWT itaipeleka Halmashauri hiyo ya Kilolo mahakamani
kupitia baraza la usuruhishi la Kazi.
“Mimi kama mwenyekiti wa CWT jambo hili limenihuzunisha na
kuniumiza sana, na ndiyo maana nimeipa kalipio
Halmashauri hii, na siyo kalipio tu pia ninatoa siku 15 kwa Halmashauri ya
Kilolo iwe imerudisha fedha hizo mapema kabla ya siku hizo 15, la sivyo tutaishitaki
mkurugenzi kwa CMA baraza la usuruhishi la wafanyakazi,” alisema Muhongole.
Naye Patrick Mlowe
muweka hazina wa CWT amesema changamoto nyingi zinazowakabiri walimu Wilayani
humo ni kukosekana kwa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSD), jambo lililosababisha
hata fedha hizo za malipo ya walimu kupotelea mikononi mwa watu wajanja na kuwa
fedha hizo zisipolipwa CWT itatangaza mgogolo na Halmashauri hiyo.
Mlowe alisema Halmashauri hiyo inapaswa itimize agizo la kurejesha fedha hizo la sivyo wao kama CWT watatangaza mgogolo, jambo ambalo hawangependa wafikie hapo.
"Hatuweze kukubali fedha za walimu zipotee hivi hivi, kama hawatarudisha fedha hizo tutatangaza mgogolo na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, huu ni uonevu mkubwa kwa walimu," Alisema Mlowe.
Kaimu
mkurugenzi wa halmashauri hiyo ya Wilaya
ya Kilolo ambaye ni afisa elimu sekondari Wilaya Gloria Kang’oma aikitaka CWT kuwa na subira
ili kulifanyia kazi suala hilo kwa lengo la kutafutiwa ufumbuzi.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni