Kati ya majengo ya chuo kikuu cha Iringa (Tumaini)
Baadhi ya viongozi na washindi wa mashindano ya Ujasiriamali, mafunzo yaliyoanzishwa na chuo kikuu cha Iringa, lengo likiwa ni kuwaongezea ujuzi, ubunifu na ufanisi wa kazi vijana pindi wanapohitimu masomo yao.
Baadhi ya viongozi na washindi wa mashindano ya
Ujasiriamali, mafunzo yaliyoanzishwa na chuo kikuu cha Iringa, lengo
likiwa ni kuwaongezea ujuzi, ubunifu na ufanisi wa kazi vijana pindi
wanapohitimu masomo yao.
Washindi wa nafasi ya kwanza, wakiwa na mfano wa hundi, kiasi cha shilingi Milioni 3, zilizotolewa na kitengo cha ujasiriamali chuo kikuu cha Iringa, ili kuleta hamasa ya vijana wasomi kupenda kujiajiri kwa kubuni miradi mbalimbali ya Ujasirimali na biashara. Wanafunzi walioibuka na ushindi kwa kushika nafasi ya kwanza, wakiwa na mfano wa hundi ya kiasi cha shilingi Milioni 3, zilizotolewa na kitengo cha ujasiriamali chuo kikuu cha Iringa, ili kuleta hamasa ya vijana wasomi kupenda kujiajiri kwa kubuni miradi mbalimbali ya Ujasirimali na biashara
Washindi wa nafasi ya kwanza, wakiwa na mfano wa hundi, kiasi cha shilingi Milioni 3, zilizotolewa na kitengo cha ujasiriamali chuo kikuu cha Iringa, ili kuleta hamasa ya vijana wasomi kupenda kujiajiri kwa kubuni miradi mbalimbali ya Ujasirimali na biashara
Mkurugenzi wa kitengo cha Ujasiriamali Chuo kikuu Iringa- Dr. Hosea Mpogole, akiwa nje ya jengo la kitengo chake cha Ujasiriamali.
Ni chupa za maji ya kunywa ambazo zimetumika, na wanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa wakabuni kutengeneza Dampo "Dustbin" ikiwa ni moja ya kazi za ujasiriamali,kuonyesha ni kiwango gani wanaweza kutumia fulsa zilizopo.
Winifrida Kyense akionyesha kazi aliyoifanya, kama ni sehemu ya ubunifu wa kutumia fulsa zilizopo katika kukabiliana na hali ngumu ya upatikanaji wa ajira.
Winfrida Kyense mwanafunzi wa mwaka wa tatu, maendeleo ya jamii, akiwa na Neema Yunge mwanafunzi wa mwaka wa tatu ualimu, wote wanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa, wakionyesha ubunifu wao kwa kutumia chupa za maji ya kunywa ambazo zimetuika.
Neema Yunge akionyesha kazi aliyoifanya, kama ni
sehemu ya ubunifu wa kutumia fulsa zilizopo katika kukabiliana na hali
ngumu ya upatikanaji wa ajira.
Joseph Charles mwanafunzi wa chuo kikuu Iringa, maendeleo ya jamii, akionyesha Pazia la Mlango ambalo limetengenezwa kwa ktumia kitako cha chupa za maji ya kunywa.
Joseph Charles mwanafunzi wa chuo kikuu Iringa, maendeleo
ya jamii, akionyesha Pazia la Mlango ambalo limetengenezwa kwa ktumia
kitako cha chupa za maji ya kunywa.
Madam Neema Mwamoto, mwalimu wa Chuo kikuu cha Iringa kitivo cha ualimu, ambaye pia alikuwa msimamizi na mwandazi wa shughuli za maonyesho ya ujasiriamali.
Neema Mwamotto akiwa na Neema Mwakatobe, waandazi na wasimamizi wa shughuli za maonyesho ya wiki ya ujasirimali, chuo kikuu cha Iringa, kabla ya kukabidhi mfano huo wa hundi kwa wanafunzi walioshinda nafasi ya kwanza katika mashindano hayo.
Madam Neema Mwamoto, mwalimu wa Chuo kikuu cha Iringa kitivo cha ualimu, ambaye pia alikuwa msimamizi na mwandazi wa shughuli za maonyesho ya ujasiriamali.
Waandazi wa shughuli za ujasiriamali Neema Mwamotto na Neema Mwakatobe, wakijiandaa kukabdhidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni tatu kwa washindi wa kwanza wa mashindano ya ujasiriamali.
<<<HABARI>>>
CHUO kikuu cha Iringa ambacho
awali Tumaini, kimewataka vijana kuachana na dhana ya kuajiriwa, kwa kupata
ajira za maofisini na badala yake watumia mbinu mbalimbali kubuni shughuli na biashara
ambazo zitawaondoa katika lindi la umasikini.
Hayo yamezungumzwa na Enock
Ugulumo mkuu wa kitivo cha biashara na uchumi, wa chuo kikuu cha Iringa, wakati
wa madhimisho ya wiki ya ujasiliamali chuoni hapo, maadhimisho yenye lengo kuu la
kuwaongezea vijana na wanafunzi maarifa katika kujitegemea.
Ugulumo amesema vijana
wanapaswa kuacha tabia ya kuchagua kazi za kufanya, na badala yake wajitume
katika kubuni shughuli za ujasiriamali zenenye tija, ambazo zinatasaidia
kupunguza…kuondoa changamoto ya upatikanaji wa ajira kwao.
Amesema wameanzisha
mpango huo chuoni hapo ili kuibua vipawa kwa vijana na kuwawezesha wanafunzi
kutumia elimu na ujuzi walionao kuibua ajira mpya, hatua itakayotoa fulsa kwa
jamii kupata nafuu ya upatikanaji wa kazi.
Aidha amesema mfumo huu
wa ujasiriamali ambao unaendana na mafunzo kwa vitendo, unawafundisha wanafunzi
namna ya kutengeneza bidhaa na kutoa huduma, kama sehemu ya kukabiriana na hali
ya maisha, kutokana na ugumu wa upatikanaji wa ajira, ambapo vijana wanatakiwa kuitumia
teknolojia waliyoipata kujitegemea.
“Chuo kikuu Iringa
tumeanzisha elimu ya kuwaandaa vijana wawe wabunifu, lakini pia tumekuwa na changamoto
kubwa, tunatoa elimu kwa vijana lakini vyuo vikuu na taasisi zinazoajiri hakuna
ushirikiano wa kutosha kwani waajiri hawajawajibika kutoa ushirikiano kwa vijana
wetu, kwani mpango huu unahitaji uwepo wa ushirikiano mkubwa baina ya vyuo
vikuu, vijana na taasisi zinazotoa ajira.
Naye Dr. Hosea Mpogole–mkurugenzi wa kitengo
cha Ujasiliamali chuo kikuu Iringa, amesema
kupitia mpango huo wa elimu ya ujasiriamali, kero ya ajira kwa vijana itapungua, ikiwa
pamoja na waajiri kuwawezesha kupata vijana
wasomi wenye ujuzi, kwani mpango huo utawasaidia vijana pia kujua na kutenda,
tofauti na siku za awali ambapo vijana wengi wasomi walikuwa na ufahamu pekee pasipokuwa
na ujuzi katika eneo la vitendo.
Dr. Hosema amesema
elimu Tanzania kwa muda mrefu imekuwa haimsaidia kijana kujua na siyo kutenda,
kwani ufahamu peke yake haumsaidii mtu katika kufanya kazi..
“Kumekuwa na changamoto
ya uelewa hasi wa dhana nzima ya ujasiriamali, wengi wanajua ujasiriamali
wanadhani ni hali ya kufanya biashara ndogondogo, ndiyo maana hata watu wasomi
wamekuwa hawapendi kujikita katika ujasiriamali, lakini ujasiriamali
tunaouzungumzia hapa chuoni ni namna ya kumfanya mtu awe mbunifu kwa kufanya
kazi kwa kujituma bila kusukumwa na kuleta mabadiliko kazini,” Alisema.
Amesema licha ya kutoa
elimu hiyo kwa wanafunzi pia wanatoa elimu ya mafunzo ya ujasiriamali kwa muda
mfupi kwa jamii inayowazunguka ya wafanyabiashara kwani baadhi ya wananchi
katika jamii, kuna tabia ya kufanya biashara kwa mazoea, na mpango huo
utawawezesha wananchi kufanya biashara zenye tija kwao na Taifa.
Hata hivyo washindi wa maonyesho
ya ujasiriamali chuo kikuu cha Iringa (Tumaini)
wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa fedha, ambapo kuanzia nafasi ya
kwanza hadi ya tatu wamepatiwa jumla ya shilingi Milioni tano.
Mshindi wa kwanza amechukua
shilingi Milioni tatu kikundi kilichoongozwa na mwenyekiti wao Fuad Faraj
Abri, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na kikundi cha "SunFlowe Oil Production"
kikiongozwa na mwenyekiti wake Denis Peter Ngaleku ambao wamejinyakulia kitita
cha shilingi Milioni mbili.
Nafasi ya tatu imeichukuliwa
na kikundi cha Tourism Safaris Organization kikiongozwa na mwenyekiti wake
James Gasper ambaye amechukua shilingi milioni moja, huku zawadi hizo zikiamsha
mori kwa wanafunzi hao kushiriki katika mashindano ya ujasiriamali kwa miaka
ijayo.
Neema Mwamoto ambaye ni mwalimu wa kitivo cha Ualimu, na Neema Mwakatobe waandaaji wa shughuri hiyo wamesema zawadi hiyo wameifanya kwa kuwashitukizia wanafunzi hao "Surprise" na itasaidia kuleta hamasa kwa wanafunzi kupenda kushiriki mashindano hayo.
Yaani hawakujua kama tunawapa zawadi, tumewafanyia kama Surprise tu, ndiyo maana wengine pale umeona wamepigwa na butwaa baada ya kupewa zawadi zao, lakini mwakani tutajipanga vizuri ili kuhakikisha mashindano haya yanakuwa na mvuto zaidi," Alisema Neema Mwamoto.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni