Ijumaa, 5 Septemba 2014

ASKOFU MTETEMELA AMTAJA RAIS WA AWAMU YA TANO


 Askofu mkuu mstaafu wa kanisa la Anglikan Tanzania Donald Mtetemela akizungumza na wadau wa mfuko wa "Mama Bahati foundation" katika uzinduzi wa tawi la taasisi hiyo ya kifedha mjini Mafinga katika wilaya ya Mufindi mkaoni Iringa.
 Kulia ni Japhet Makau- kurugenzi wa mfuko wa "Mama Bahati Foundation," akiwa na baadhi ya viongozi wa mfuko huo katika uzinduzi wa tawi la Mafinga.
 Japhet Makau- Mkurugenzi wa mfuko wa "Mama Bahati Foundation," akiwa na baadhi ya viongozi wa mfuko huo katika uzinduzi wa tawi la Mafinga.
 Evarista Kalalu- Mkuu wa Wilaya ya Mufindi- Iringa akitoa nasaha kwa wadau wa mfuko huo wa "Mama Bahati Foundation," katika uzinduzi wake.
Mmoja wa viongozi wa Five Tarent kutoka nchini Uingereza shirikja rafiki wa mfuko wa "Mama Bahati Foundation," akiwa katika uzinduzi mjini Mafinga.

 Akinamama wadau wa mfuko wa "Mama Bahati Foundation," Wakiwa katika sherehe ya uzinduzi.

 Pendo Donald Mtetemela akiwa katika uzinduzi wa tawi la Mafinga, tawi lililolenga kusogeza huduma ya mikopo kwa akinamama walio nje ya mji wa Iringa.
 Pendo Donald Mtetemela (Kulia) akiwa na baadhi ya viongozi wa mfuko wa "Mama Bahati Foundation," katika uzinduzi wa tawi la Mafinga.
 Kalistus Lugenge, afisa mikopo wa mfuko wa "Mama Bahati Foundation," akishuhudia uzinduzi huo kama ni sehemu ya kuongeza wigo wa huduma katika kuwafikia akinamama wengi zaidi walio wajasiriamali.
 Elick Makamba mmoja wa maafisa katika mfuko wa "Mama Bahati Foundation," akisikiliza jambo kwa umakini katika uzinduzi wa taasisi hiyo ya kifedha.

 Askofu mkuu mstaafu Donald Mtetemela akiteta jambo na Evarista Kalalu - mkuu wa Wilaya ya Mufindi katika sherehe ya uzinduzi wa mfuko wa "Mama Bahati Foundation,".
 Kulia ni mmoja wa marafiki wa mfuko wa "Mama Bahati Foundation," akizungumza jambo katika siku hiyo ya uzinduzi mjini Mafinga.
 
Japhet Makau- Mkurugenzi wa mfuko wa "Mama Bahati Foundation," akizungumza lengo la kufungua tawi la mfuko huo mjini Mafinga.

<<<HABARI>>>


ASKOFU mkuu mstaafu Donald Mtetemela wa kanisa la Anglikan Tanzania, ambaye pia ni mjumbe wa bunge la katiba mpya, amewataka watanzania kuwa makini katika kujadili suala la nani atakaye kalia kiti cha urais awamu ya tano.

Askofu Mtetemela ameyasema hayo- katika uzinduzi wa taasisi ya kifedha ya Mama Bahati foundation, katika tawi la mafinga- Mufindi mkoani Iringa, tawi lililoanzishwa kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi waishio maeneo ya nje ya mji.

Mtetemela amesema suala la watanzania kutazama umri wa rais ajaye– kama ni Kijana au mzee si jambo la muhimu bali ni kuchagua kiongozi atakayekuwa muadilifu mwenye nia thabiti ya kuwainua wananchi wake na Taifa kwa ujumla na ambaye atakuwa ni mnyoofu wa tabia, mwenye kutambua kuwa amebeba maisha ya watu.

Aidha amesema rais wa awamu ya tano awe ni Yule anayetambua wajibu wake, mwenye dhamira ya kulisogeza mbele Taifa kiuchumi na kuwa suala la umri lisiwe kipaumbele, kwakuwa watanzania wanaweza kuchagua kijana au wazee ambaye atalisababishia hasara Taifa.

Akitolea mfano wa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.. Mtetemela licha ya kuwa kiongozi huyo alianza kazi ya kuliongoza taifa akiwa kijana hadi mtu mzima,  lakini busara zake zinaishi na zinahitajika mpaka sasa katika kuliendeleza Taifa, na kuwa jambo la umri si kipaumbele sahihi cha kumpata kiongozi bora.

Akizungumzia suala la tuhuma dhidi yake.. juu ya kuegemea upande wa siasa, Askofu Mtetemela amesema yeye si mwanachama wa chama chochote cha siasa, bali anamsimamo dhidi ya mambo muhimu ambayo ni dira sahihi kwa Taifa, na kuwa kamwe hawezi kuwa na itikadi za kisiasa kutokana na ukweli kuwa waumini wake waliomtuma wanatokana na vyama mbalimbali.

Mtetemela amesema pia yeye kama kiongozi hawezi kukwepa lawama kwa watu, na kamwe hawezi kukasirika anaposikia anazungumziwa iwe nikwa mazuri au mabaya hatatakasilika, na kuwa kuna umuhimu watanzania kuchagua kiongozi anayefanana kwa tabia na mwenendo kama baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

“Kwanza kiongozi ninaamini kuwa tuhuma hupewa yoyote, na ukituhumiwa huwezi ukakasirika ovyo ovyo tu,!! Kupata hizo tuhuma si jambo geni kwangu, lakini pili ningependa nikanushe kuwa mimi siyo mwanachama wa chama chochote, iwe CCM, CHADEMA wala NCCR -maana kama ni kiongozi wa kidini waumini wangu wanatoka katika vyama mbalimbali- siwezi nikageuka nikawa wa chama kimoja, hiyo ndiyo kanuni yangu mimi,” Alisema Askofu Mtetemela.

Aidha amesema hata kama tuhuma hizo za kuwa anafungamana na vyama vya siasa zinamfikia yeye hatua hiyo inatokana na msimamo wake kwani yeye anaunga mkono  kitu ambacho kipo sahihi, na hajali kimesemwa na nani hata kama mtu asiyependana naye bali nini kimesemwa.

“Kwa mfano mimi nilikemea bungeni nikasema siyo sawa mtu kuita bunge ni Intarahamwe, nilikemea kwa sababu sisi siyo wauaji, sikujali nani amesema, maana Intarahamwe walifanya mauaji kule Rwanda, sasa kama kuna watu wananipa tuhuma kwa sababu wanataka niwe upande fulani mimi siwezi kwani ninatoka kundi la 201katika kikundi cha wajumbe wanaowakirisha mashirika ya dini,”

Hata hivyo Mtetemela alisema kamwe hawezi kutoka katika bunge hilo eti kwa sababu kuna watu Fulani wametoka, kwa madai kuwa yeye anao wajibu ambao amepewa na wale waliomtuma na mheshimiwa rais akamteua na kutoka kwake mpaka bunge linapokwisha kisheria.

MWISHO



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni