Ijumaa, 25 Aprili 2014

VIONGOZI WA CHADEMA WATIMKIA CCM


 Katibu wa chama cha mapinduzi CCM W/ Ya Mufindi Miraj Mtaturu akiwa na mjumbe wa halmashauri kuu CCM - MNEC Wilaya ya Mufindi ambaye pia ni mwenyekiti wa UWT W ya Mufindi Marcellina Mkini, katika hafla ya kuwapokea viongozi hao waliohama CHADEMA.

Baadhi ya viongozi wa CCM Kata ya Itandula na kijiji cha Kimilinzowo na wale wa Wilaya ya mufindi wakishuhudia tukio hilo.
 Baadhi ya viongozi wa kijiji cha Kiliminzowo na kata ya Itandula Wilaya ya Mufindi- Iringa.
 Baadhi ya wananchi na viongozi wa kijiji na kata ya Itandula wakiwa katika hafla hiyo ya viongozi wa CHADEMA kujiunga na CCM.

 Maimuna Mwakaje - Katibu wa UWT Mufindi kusini akiwa na kiongozi mwenzake Matilda Matimbwi- ambaye ni katibu wa Wazazi Wilaya ya Mufindi wakishuhudia wanachama wapya wa CCM kutoka CHADEMA.
 Baadhi ya viongozi, wanachama na viongozi wa kijiji cha Kimilinzowo na Kata ya Itandula.
 Viongozi wa Kata ya Itandula, wakishuhudia tukio hilo.

 Mwenyekiti wa CCM Tawi la Kimilinzowo Andreas Chagavalye akizungumza na wananchi waliojitokeza katika mkutano huo.
 Andreas Chagavalye akisisitiza jambo.

  Zawadi Waziri Shombe aliyekuwa mjumbe wa Oparesheni ya M4C kanda ya kusini,  akizungumzia azma ya yeye kujiunga na CCM.

  Bernado Lugenge aliyekuwa katibu mwenezi CHADEMA, akitoa neno la ushuhuda mara baada ya kujiunga na CCM.

Aliyekuwa Katibu wa Chadema Jimbo la Mufindi Kusini - Emanuel Ngwalanje, akishuhudia jambo, katika hafla hiyo.
 Daud Yasini Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Mufindi, akishuhudia jambo katika hafla hiyo ya kuwapokea wanachama wapya walioamua kujiunga na CCM.
 Maimuna Mwakaje katibu wa UWT Wilaya ya Mufindi, akizungumza na wananchi, wanachama na viongozi katika mkutano huo.
  Wanachama wapya waliojiunga na CCM kutoka CHADEMA wakila kiapo cha utii.

 Katibu wa chama cha mapinduzi CCM W/ Ya Mufindi Miraj Mtaturu akiwa na mjumbe wa halmashauri kuu CCM - MNEC Wilaya ya Mufindi ambaye pia ni mwenyekiti wa UWT W ya Mufindi Marcellina Mkini, katika hafla ya kuwapokea viongozi hao waliohama CHADEMA.

<<<HABARI>>>
VIONGOZI wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA nyanda za juu kusini, wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha mapinduzi CCM kwa madai kuwa wamechoshwa na ubabaishaji.

Viongozi hao waliohama CHADEMA ni pamoja na Katibu wa Chadema) Jimbo la Mufindi Kusini, Emannuel Ngwalanje, alikuwa katibu wa CHADEMA jimbo la Mufindi Kusini, Zawadi Waziri Shombe ambaye alikuwa ni mjumbe wa Oparesheni ya M4C Nyanda za juu kusini, pamoja na Bernado Lugenge aliyekuwa Katibu Chadema.

Wamesema hatua hiyo ya kujitoa Chadema na kujiunga CCM ni kutokana na hali isiyoeleweka juu ya chama hicho na hivyo kuamua kujiunga na CCM ili kuungana na wananchi wenzao katika kuleta maendeleo.


Ngwalanje amesema katika kipindi cha zaidi ya miaka minne alichokuwa Katibu wa Chadema Jimbo la Mufindi Kusini ameweza kushawishi zaidi ya wakazi 600 katika maeneo mbalimbali jimboni humo ambao waliweza kujiunga na chama hicho.

Naye Zawadi Shombe aliyekuwa mjumbe wa oparesheni ya M4C kanda ya kusini amesema demokrasia inayohubiriwa kutafutwa na chadema nchini ina walakini kwa kuzingatia kwamba ndani ya chama hicho zipo nafasi za uongozi ambazo wanachama wengine wamekuwa hawapatiwi fulsa ya kuzimiliki.


 “Nimeamua kurudi nyumbani, nyumbani kwa baba yangu na mama yangu CCM, ili nishirikiane na wana Mufindi wenzangu kuleta maendeleo ya Taifa,”  nimetumika vya kutosha Chadema na hakuna nilichofanya cha muhimu, zaidi ya upotoshaji na vurugu tupu,” Alisema.


Aidha Bernado Lugenge aliyekuwa katibu mwenezi CHADEMA tawi la Kimilinzowo, amesema hatua ya wao kuingia CCM ni pigo kubwa kwa Chadema kwani wao ndiyo walikuwa mstari wa mbele kutete na kushawishi, ili kukifanya chadema kuwa imara Mufindi.

Baadhi ya wanachama wa CCM na wananchi waliohudhuria hafla hiyo wamesema  CHADEMA imepata pigo kufuatia viongozi hao kuondoka kwani walikuwa ni nguzo kuu wilayani Mufindi.

“Hawa watu walikuwa wanaushawishi mkubwa sana CHADEMA, na walikuwa  wanaogopewa na wana CCM, walikuwa na uwezo mkubwa wa kushawishi na kujenga hoja na hali hiyo ndiyo imewavuta wananchi wengi kujiunga na chamdema,” Walisema.


Hatua ya viongozi hao wa chadema kurudi CCM imepokewa kwa furaha na  wana  CCM huku wananchi wa kijiji cha Kimilinzowo wakipata manufaa kupitia tukio hilo kwani furaha ya viongozi waliohudhuria hafla hiyo imewafanya watoe ahadi ya kusaidia mifuko zaidi ya 50 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi mbalimbali  uliokuwa umekwama.

Baada ya kukabidhi kadi na magwanda ya Chadema kwa uongozi wa CCM wilaya ya Mufindi na baadaye kupewa mavazi na kadi ya CCM, Ngwalanje na wenzie wamesema kazi kubwa iliyopo mbele yao ni kuisambaratisha Chadema katika wilaya hiyo ya Mufindi na mkoa mzima wa Iringa.

“Kazi ya kuibomoa Chadema sasa imeanza, na kazi hii haitaishia katika wilaya ya Mufindi tu, tutaiendeleza hadi Jimbo la Iringa Mjini ambalo linaloongozwa na mbunge Mchungaji Peter Msigwa kupitia Chadema.” Walisema.

Marcelina Mkini mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa  "MNEC" na mwenyekiti wa umoja wa wanawake UWT Wilaya ya  Mufindi amesema tukio hilo la kipekee linapaswa liwe Baraka kwa kuwapa ushirikiano vijana hao, pasipo kuwabagua.

“Vijana hawa wanatosha jamani, tumewasikia walivyojieleza hapa na namna walivyokuwa ni nguzo huko nChadema, kwa kweli kwa hili niwapongeze sana ndugu zangu kwa jambo hili tunalolishuhudia leo, kwani ni jambo linaloonyesha kuwa tupo imara, kwani tungewaacha vijana hawa waendelee kuyumbayumba tungeonekana hatutoshi ndani ya chama chetu, tunatakiwa tuwape ushirikiano wa kutosha, kwani hata makanishani wanaorudi kundini hawapaswi kunyoshewa kidole, kwani hali hii ni ishara ya kudumisha amani katika chama chetu, ” Alisema mkini.

Aidha Mkini amesema katika Wilaya ya Mufindi hakuna wanawake waliojiunga na Chadema kwani wanafahamu kuwa kunapotokea machafuko na kukosekana amani wanaopata taabu ni akinamama na watoto, na kuwa suala hilo ambalo ni ishara ya amani linapaswa kuendelezwa zaidi kwani ni jambo la kujivunia.


Katibu wa CCM Wilay ya Mufindi Miraji Mtaturu, amesema ushuhuda huo ni Baraka hata mbele ya Mwenyezi Mungu, kwakuwa aliweka utaratibu wa kuwasamehe watu wanaotubu dhambi zao.

Mtaturu amesema katika siasa watu wanaoamua kumaliza tofauti na kurejea katika chama tawala ni sawa na mwana mpotevu anaporudi nyumbani, anatakiwa kusamehewa dhambi na kufanyiwa sherehe ya kumpongeza kwa ujasiri, huku akiwapongeza vijana hao kwa ujasiri wa kutambua umuhimu wa wao kuwa ndani ya chama chenye kuwaletea wananchi maendeleo.

"Ninawaombeni wanaCCM wenzangu tushirikiane na vijana wetu hawa, kwa hali na mali, kwani wao wenyewe wamepima na kuona CCM ndiyo chama imara, niwaombeni kusiwepo na ubaguzi wa aina yoyote juu yao,  ni vijana wanaofanya kazi za uimarishaji wa cha, nadhani mnawafahamu ni wenzenu, amani, upendo ndiyo msingi wa kila kitu kuyafikia maendeleo," alisema Mtaturu

Amesema CCM ina furaha kubwa kuendelea kuwapokea watanzania waliopotea kwa kujiunga na vyama vya upinzani na baadaye kubaini makosa waliyoyafanya na kuamua kurudi katika chama kinachohimiza amani, utulivu kwa lengo la kuboresha maisha ya raia wake na kuwaletea maendeleo wananchi.
MWISHO


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni