Mwenge wa Uhuru ukiwa mpaka mwa mkoa wa Iringa na Morogoro- katika Kata ya Ruaha mbunyuni Iringa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma akitoa taarifa ya mbio za mwenge mkoani Iringa, muda mfupi mara baada ya kuupokea kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera.
Askari akionyesha utii, heshima, nidhamu kama ni sehemu ya uzalendo wa Mtanzania, kwa kuulinda Mwenge ambao ni alama ya uhuru wa Tanzania.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dk. Christine Ishengoma (Kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerlad Guninita katika eneo la Ruaha Mbuyuni mara tu baada ya kuupokea mwenge huo kutoka mkoani Morogoro.
<<<HABARI>>>
MWENGE wa Uhuru ambao
upo mkoani Iringa ukitokea mkoani Morogoro- unataraji kuzindua miradi 42 ya maendeleo yenye thamani zaidi ya
shilingi Bilioni 3 na Milioni 109.
Hayo
yamezungumzwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Dk. Christine Ishengoma wakati akipokea
Mwenge huo wa Uhuru eneo la Ruaha Mbunyuni- katika wilaya ya Kilolo, kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera.
Dk. Ishengoma
amesema miradi inayozinduliwa na mbio za Mwenge mkoani Iringa- niya sekta ya
maji, sekta ya afya, elimu na miradi ya maendeleo ya jamii - yote ikiwa na
umbali wa km 1159.
Aidha amesema
fedha za miradi ya maendeleo itakayozinduliwa ni michango mbalimbali kutoka serikali kuu,
wadau wa maendeleo, Halmashauri na manispaa, huku mwenge huo akiukabidhi kwa mkuu wa Wilaya ya
Kilolo kama ni sehemu ya kuanza rasmi kwa kazi za kukimbiza Mwenge mkoani Iringa.
Hata hivyo Dk. Ishengoma alimkabidhi Mwenge huo wa Uhuru mkuu wa Wilaya ya kilolo Gerlad Guninita kwa minajiri ya kuwa unaanza kazi ya kuzindua miradi ya maendeleo katika Wilaya hiyo ya Kilolo.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni