Baadhi ya warembo watakaopanda jukwaa kuwania taji la miss Iringa leo tarehe 20-june-2014.
Kati ya warembo 10 watakaopanda jukwaa leo kuwania taji la miss Iringa 20-june-2014. Warembo 4 kati ya 10 watakaopanda jukwaa la St. Dominic leo kuwania taji la miss Iringa 20-june-2014.
Ni warembo wanne kati ya 10 watakaopanda jukwaani leo kuwania taji la miss Iringa 20-june-2014-katika ukumbi wa St. Dominic Mjini Iringa.
Mratibu na mkurugenzi wa Chakudika Entertainments- Victory Chakudika akifafanua jambo husiana na mashindano hayo.
<<<HABARI>>>
HATIMAYE wapenzi
wa mashindano ya Miss Iringa leo kushuhudia mlimbwende atakayevalishwa taji kwa
kuibuka mshindi – baada ya warembo 10 walioingia katika mashindano hayo kupanda
jukwaani.
Akizungumzia
ubora wa mashindano hayo- mratibu wa mashindano Victory Chakudika ambaye ni
mkurugenzi wa Chakudika Entertainments amesema warembo hao 10 wapo vizuri na
wamepikwa kwa vigezo vya Kimataifa.
Chakudika
amesema mashindano hayo niya aina tofauti kwa mwaka huu 2014 kwani yameandaliwa
vyema na wapenzi wa mashindano hayo ubora wa hali ya juu na hiyo ni kutokana na
warembo wenyewe kujitambua.
Aidha Chakudika amesema kambi ya
walimbwende hao 10 imekitwa katika Hotel ya kitaifa ya Gentle Hill iliyopo eneo
la Gangilonga mjini Iringa na hiyo ni kuwawezesha walimu wa warembo hao kufanya
kazi inayotakiwa ili mkoa wa Iringa kutoa mrembo atakayekubalika hadi ngazi za
Kitaifa na kimataifa.
Neema Mariti ni Miss
Iringa mwaka 2013 ambaye anatarajia kukabidhi taji hilo kwa mrembo atakaeibuka
kuwa mshindi leo hii siku ya ijumaa, katika
jukwaa la ukumbi wa St. Dominic mjini Iringa.
Neema ambaye pia
ni mwalimu wa warembo hao 10 amesema anayo imani kubwa kwa warembo hao kwani
amewapika kwa viwango vya kimataifa, lengo likiwa ni kuchukua ushindi wa Miss
Tanzania na ngazi za juu za mashindano hayo.
Neema amesema uhakika
huo ni kutokana na kuwaeleza namna ya kufanya warembo hao- huku akiweka bayana
changamoto chache zilizomkosesha taji la Miss Tanzania.
Miss Iringa
ambayo ipo chini ya udhamini mkubwa wa Redds pia imedhaminiwa na Hotel ya Gentle
Hill, kinywaji cha Coca Cola, Savana Pub, Radio Nuru pamoja na mabasi ya SUTCO
Nna kiingilio kikiwa ni shilingi elfu 20 kwa VIP na elfu 10 kwa viti vya
kawaida.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni