Uzinduzi wa mradi wa maji ya kuvutwa kwa nishati ya umeme wa jua- Soral.
Bw. Lion Karim Mitta wa kwanza kushoto akiwa na rais anayemaliza muda wake Bi. Nureen Nathoo katika siku ya uzinduzi wa mradi wa maji yanayovutwa kwa kutumia nishati ya umeme wa jua, katika kijiji cha mawindi.
Bi. Shyrose Mitta, mke wa Lion Karim Mitta wa kwanza kushoto wakiwa katika siku ya uzinduzi wa mradi wa maji yanayovutwa
kwa kutumia nishati ya umeme wa jua, katika kijiji cha mawindi.
Naye waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uratibu wa bunge na
sera Willium Lukuvi- akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mawindi katika uzinduzi wa mradi wa maji yanayovutwa
kwa kutumia nishati ya umeme wa jua, katika kijiji cha mawindi.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza jambo kutoka kwa viongozi wa Lion Club waliofika katika uzinduzi wa mradi wa maji yanayovutwa
kwa kutumia nishati ya umeme wa jua, katika kijiji cha mawindi.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza jambo kutoka kwa viongozi wa Lion Club waliofika katika uzinduzi wa mradi wa maji yanayovutwa
kwa kutumia nishati ya umeme wa jua, katika kijiji cha mawindi.
Mzee wa kabila la wahehe akisikiliza jambo kutoka kwa viongozi wa Lion Club waliofika katika uzinduzi wa mradi wa maji yanayovutwa
kwa kutumia nishati ya umeme wa jua, katika kijiji cha mawindi.
Lion Mathew Alex -rais mtarajiwa anayetaraji kuanza kazi Lion Club, akiwa katika uzinduzi huo.
Bi. Nureen Nathoo wa kwanza kulia akiwa na Lion Karim Mitta wakishuhudia upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa kijiji cha mawindi kilichopo Kata ya Nyang'olo katika Tarafa ya isimani Wilayani Iringa.
<<<HABARI>>>
WANANCHI wa kijiji cha Mawindi tarafa ya Isimani mkoani Iringa wameepukana na adha ya shida ya huduma ya maji iliyowafanya watembee umbali wa zaidi ya km 10 kuifuata na kusababisha hali ya uchumi na maendeleo kudumaa.
Hatua hiyo umeilazimu mradi wa Lion Club host ya jijini Dar
es salaam kuingilia kati, kupitia Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu
sera na uratibu wa bunge Willium Lukuvi, ambaye pia ni mbunge wa jimbo
hilo la Isimani.
Lion Club imejenga kisima cha maji kinachotumia nishati ya
Umeme wa jua "Solar" katika kijiji cha Mawindi kilichopo Kata ya
Nyang'olo tarafa ya Isimani, na hiyo nikutokana na jografia ya eneo hilo kuwa
Kame.
Akizungumzia hali hiyo Waziri Lukuvi amesema imemlazimu
kutumia kiwango kikubwa kubaini uwepo wa maji katika kijiji hicho cha Mawindi.
Lukuvi amesema shida kubwa katika tarafa ya Isimani ni kero
ya upatikanaji mgumu wa huduma ya maji, na kuwa sasa tayari amechimba visima 25
katika tarafa hiyo ili kupunguza adha kwa wananchi.
Aidha amesema hali hiyo inatokana na vijiji vya kata ya
Nyang'olo kutopitiwa na mto wala bwawa-na hivyo ardhi yake kuwa kame na
kushindwa kuwa na asili ya maji.
Lion Karim Mitta mmoja wa viongozi wa Lion Club amesema
kupitia Waziri Lukuvi alibaini changamoto kubwa ya maji kwa wananchi wa
Mawindi.
Karim Mitta amesema kuHayo yamezungumzwa na muhandisi wa
maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Lukas Madaha wakati Waziri wa katiba na
sheria Willium Lukuvi wakati akikabidhi mradi wa maji unaotumia nishati ya jua
(Soral).
Lion Mathew Alex rais anayetaraji kuchukua nafasi ya urais
wa "Lion Club" amewataka watanzania kujiunga katika Club hiyo na
kuondokana na fikra ya kudhani kuwa kikundi hicho nikwa ajili ya jamii ya watu
wa Kihindu "Wahindi".
Naye rais anayemaliza muda wake wa "Lion
Club" bi- Nureen Nathoo amesema msaada huo ni mfano, na wapo Lion ipo
tayari kuwasaidia wananchi wa vijijini ambao wanakabiliwa na changamoto ya
huduma ya maji na huduma ya afya.
"Tunatoa huduma mbalimbali kama ya afya, tumekuwa
tukiwasaidia wagonjwa wa Moyo, lakini hili la maji kwa njia ya nishati ya umeme
wa jua ni huduma ya mfano na tupo tayari kuwasaidia pia wananchi wa vijiji
mbalimbali vya Isimani kupitia rafiki yetu waziri Lukuvi," Alisema
Nureen.
Upendo Tewele na Zamda Issah niwakazi wa kijiji cha Mawindi
wamesema tatizo la uhaba wa maji katika kijiji chao - umesababisha shughuli za
maendeleo kukwama, huku baadhi ya akinamama wakipata adha ya kuachwa na wenza
wao.
Upendo amesema walikuwa na mpango wa ujenzi wa vyumba vya
madarasa na ujenzi wa nyumba za walimu, lakini wamekwama kufikia lengo hilo
kutokana na kero ya upatikanaji wa maji.
Wamesema hulazimika kutembea umbali wa zaidi ya km 10
kufuata maji katika kijiji cha Msosa, ambapo hujidamka usiku wa manane na kurejea
na ndoo za maji nyumbani saa nane mchana jambo ambalo linadumaza hata kufanyika
kwa shughuli nyingine.
Wamesema baadhi ya akinamama
wajawazito wanaojituma kutafuta maji, wamekuwa wakijifungulia njiani, jambo
ambalo lilikuwa hatari zaidi kwa usalama wa maisha yao na watoto wao, na kuwa
ujio wa mradi huo ni ukombozi mkubwa kwao na salama ya kuvunjika kwa ndoa zao.
Muhandisi wa maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Lukas
Madaha amesema wananchi wa kijiji hicho cha Mawindi wanakabiliwa na
changamoto kubwa ya maji na kuwa Mawindi ni kati ya vijiji zaidi ya 100
ambavyo vilikuwa na adha ya upatikanaji mgumu wa huduma hiyo muhimu.
Madaha amesema hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika
Halmashauri ya Wilaya ya iringa ni wastani wa asilimia 68, huku huduma
hiyo ya maji ikipatikana kwa njia ya miradi ya maji ya bomba, Visima virefu,
miradi ya maji ya visima vifupi, miradi ya maji inayotumia Pampu za injini za
mafuta na umeme.
Hata hivyo Madaha ameiomba Lion Club iendelee kutoa ufadhili
kwa vijiji vingine vyenye shida ya maji vilivyopo katika Halmashauri hiyo
kwa kuwa tatizo bado ni kubwa.
Naye waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uratibu wa bunge na
sera Willium Lukuvi amesema mradi huo wa maji unaotumia nishati ya umeme wa jua umefadhiliwa
na Lion Club Host ya jijini Dar es Salaam na lengo ni kupunguza changamoto
zinazowakabiri wananchi wa jimbo lake.
Lukuvi amesema kwa ushawishi wake kama mbunge wa jimbo hilo
la Isimani amewaomba Lion Club kuchimba visima 25 katika tarafa ya Isimani
ambayo ina hali ngumu ya upatikanaji wa huduma ya maji.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni