Ramadhani Mrisho almaarufu MAKOSA, mtu maarufu mkoani Iringa, ambaye sasa ametangaza rasmi kuuza Figo yake ili kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi.
JINA Makosa si geni masikioni mwa
wakazi wa mji wa Iringa na mikoa ya nyanda za juu kusini na hata kwingineko,
Makosa ni mkazi wa Manispaa ya Iringa, licha ya kufanya kazi zake mbali mbali
siku za nyuma.
Makosa jina lake halisi ni “Ramadhani
Mrisho” aliwahi kuwa tajiri wa kusifiwa njini Iringa, kwa kumiliki baadhi ya
majumba, magari, kituo cha Luninga IMTV, ukumbi wa IDYDC awali Cat’s iliyo mkabala na maktaba ya mkoa wa Iringa huku
akiwa na Zahanati iliyojibebea umaarufu mkubwa mjini Iringa iliyoitwa kwa jina
lake “MAKOSA DISPENSARY”.
Makosa aliweza kuwa na utajiri huo
baada ya kustaafu kazi yake ya Ubaharia mwanzoni mwa miaka ya tisini, na pia amewahi
kujitolea kupanda miti ya aina mbalimbali ikiwemo ya matunda Manispaa nzima ya
Iringa, miti ambayo kwa sasa ni urembo unaounakshi Mji wa Iringa, kwa kuwa na
ukijani wa kuvutia katika kila nyumba ambazo ziliuendeleza utamaduni wake wa
kupenda mazingira.
Wakati akifika mjini Iringa, MAKOSA
akiwa na itikadi za watu wanaosuka nywele ndefu (rasta), alikuwa si mnywaji wa pombe,
mnyenyekevu na alijikita katika kuisaidia jamii ya watu wa Iringa kuhifadhi
mazingira likiwempo hilo la kupanda miti, ya aina mbalimbali inayoupendezesha
mji.
Licha ya kufanya kazi hizo na hata
kuisaidia serikali juu ya uhifadhi ya mazingira, historia ya MAKOSA kwa baadhi
ya watu sasa ni kama vile imesahaulika kwasababu hakuna anayemuenzi kwa kazi
kubwa hiyo aliyoifanya.
Sijui ndiyo yale yale ya kutaka
kumsifu na kumuenzi baada ya kupoteza uhai wake, lakini ingekuwa vyema watu wa
aina hii wakapewa sifa zao na hata kuendelea kutumia mawazo yao ili kuwavutia
na wengine kufanya hayo ambayo ni mfano bora katika jamii.
Pamoja na harakati hizo MAKOSA ndio
mtu wa kwanza mjini Iringa kuingiza mabasi madogo ya kusafirisha abiria aina ya
Coaster yaliyokuwa yakifanya kazi katika maeneo mbalimbali ya mjini Iringa hasa
Iringa, Ilula na Ruaha mbuyuni.
Licha ya kuwa mtu huyu MAKOSA amefanya mengi na makubwa lakini hakumbukwi, leo hii natumia pia safu hii japo kumpa sifa zake, bila kusubiri desturi ya kumsifia mtu mpaka anapopoteza uhai wake.
"Makosa ni mtu mcheshi, asiye na makuu, mchangamfu, anayejua kumzoea mtu hata asiyemfahamu, hana ubaguzi kwake kila mmoja ni rafiki, awe kijana au mzee, asiye na aibu kueleza shida yake, hahofii kuchekwa anapotaka kujifunza kitu, muwazi na mkweli".
Miezi kadhaa iliyopita Makosa alitangaza
kujinyonga katika uwanja wa hayati samora Masheli uwanja wa mjini Iringa, huku
akitangaza ,kiingilia kuwa watoto ni sh. 500 nawa kubwa sh. 100 fedha ambazo
zingeweza kusaidia kununua Madawati ili mji shule za Iringa ziepukane na uhaba
wa madawati unaosababisha wanafunzi wake kukaa Sakafuni, huku baadhi yao
wakitumia njia mbadala ya kukalia madawati yaliyotengenezwa kwa Udongo na Nyasi.
Leo hii Makosa amekuja na kali mpya
ya mwaka ya kutangaza kuuza moja kati ya FIGO zake.
“Hali yangu kiuchumi sio nzuri
nalazimika kuuza moja kati ya figo zangu ili nipate fedha itakayonisaidia
kuendesha maisha,” alisema wakati akizungumza na mtandao huu.
MAKOSA ambaye hivikaribuni
amejipachika jina lingine akijiita MOBUTU SESESEKO amesema amefanya maamuzi
hayo akiwa na akili timamu na akaomba watakaopata taarifa hii wasimzanie akili
yake imekuwa tofauti.
“Nina akili timamu, nimeamua
kuchukua uamuzi huu kama nilivyosema kwa lengo la kujikwamua kiuchumi,” alisema
bila kufafanua bei ya FIGO yake kama atapata mteja.
Amesema: “Najua wapo watu wenye
matatizo ya FIGO na wamekuwa wakisafiri mbali na nchi kutafuta,kama kuna yoyote
amekosa au yupo nchini na anahitaji basi aje ili tukubaliane bei.
Katika dhana ile ile ya kupata fedha
zitakazosaidia kuendesha familia yake, Julai 2012 MAKOSA alitangaza kujinyonga
katika tukio alilopanga lifanyike ndani ya uwanja wa Samora kwa sharti la
mashuhuda wake kulipa kiingilio ambacho kingekusanywa na familia yake.
MAKOSA alinukuliwa wakati huo
akisema kuliko familia yake kuendelea kutaabika ni bora ajitoe muhanga ili
zikusanywe fedha zitakazosaidia kuinusuru familia yake na kiasi kingine
kusaidia watoto yatima.
“Mpango wangu huo haukuzaa matunda,
nikiwa katika maandalizi watu mbalimbali wakiwemo Polisi walijitokeza na
kunipatia ushauri nasaha jambo lililosababisha nisitishe uamuzi wa kujingonga,”
alisema.
Sasa nimekuja na mpango mpya, mpango
huu si mwingine zaidi ya huu wa kuuza FIGO yangu moja, naamini nikifanikiwa
nitapata fedha”, amesema.
Taarifa kutoka kwake mwenyewe
biashara zote hizo haziko tena mikononi mwake na ugumu wa maisha unazidi
kumuandama, na kuwa sasa anatafuta kujikwamua na njia halali anayoiona mbele
yake ambayo ni kuuza FIGO yake moja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni