Baadi ya misaada ambayo imechangwa na wanaKihesa wakiwa nayo katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa, kabla ya kuanza kukabidhi kwa wagonjwa, misaada ambayo ni Shuka, Juice, Sabuni, Mafuta ya kupaka, maji ya kunywa, Biscuit na Pipi.
Algentina Kipate- Mwanaumoja wa Kihesa.
Mmoja wa wanachama wa Kihesa Algentina Kipate ambaye ni muuguzi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa naye yumo katika jumuiya hiyo
Wanaumoja wa Kihesa wakifanya usafi wa kufagia katika maeneo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
Wanaumoja wa Kihesa wakifanya usafi wa kufagia katika maeneo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
Wanaumoja wa Kihesa wakifanya usafi wa kufagia katika maeneo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
Ni kama wanasema "lazima mazingira haya tuyaache yakiwa safi kabisa".
akinamama wa umoja wa "wanakihesa" wakiendeleza usafi katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa.
Wanaumoja wa Kihesa wakifanya usafi wa kufagia katika maeneo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
Wanaumoja wa Kihesa wakifanya usafi wa kufagia katika maeneo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
Mwenyekiti wa umoja wa "Wanakihesa" Mussa wanguvu ambaye pia ni diwani wa Kata ya Kihesa akitoa misaada kwa wagonjwa katika maadhimisho ya "Kihesa Day" ambapo siku nne zimetengwa na umoja huo kwa ajili ya kuwatembelea watu wenye mahitaji maalumu, kama wagonjwa.
Mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa akipokea misaada mbalimbali kutoka kwa wanaumoja wa Kihesa.
Mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa akipokea misaada mbalimbali kutoka kwa wanaumoja wa Kihesa.
Happy Mbegalo, ambaye amelazwa na mtoto wake mchanga, akipokea misaada kutoa kwa wanaumoja wa Kihesa, Happy Mbegalo ni mwanahabari mkoani Iringa.
Happy Mbegalo akifurahi kutembelewa na wanaumoja wa Kihesa, wa kwanza kushoto ni Patricia Nyomolelo mwanaumoja wa Kihesa.
Happy Mbegalo."Mama kichanga"
Mtoto mchanga wa Happy Mbegalo.
Mtoto mchanga wa Happy Mbegalo ambaye naye amebahatika kutembelewa na wanakihesa na kupatiwa misaada mbalimbali.
Mgonjwa akipokea baadhi ya misaada.
Neema Msafiri Mtangazaji wa Radio Ebony fm naye kama mkazi wa Kihesa hakuwa nyuma katika zoezi hilo.
Neema naye akifurahia kuwaona watoto vichanga ambao walitembelewa na wanachama hao wa wanakihesa naye akiwa mmojawao.
Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Ebony Neema Msafiri ambaye ni mkazi wa Kihesa, naye akijumuika katika shughuli za Umoja huo wa "Wanakihesa".
<<<<<<<<<<<<<<HABARI>>>>>>>>>>>>
HOSPITALI ya
rufaa ya mkoa wa Iringa, inakabiliwa na uhaba mkubwa wa shuka katika vitanda
vya kulalia wagonjwa, jambo ambalo linaweza kuibua magonjwa mengine kwa wagonjwa
wanaolazwa katika Hospitali hiyo.
Hayo yamebainika
wakati kikundi cha “Wanakihesa” cha mjini Iringa kilipotembelea wagonjwa na
kutoa misaada mbalimbali yakiwemo mashuka ya wagonjwa katika Wodi za Hospitali
hiyo ya Rufaa ya Iringa.
Wakizungumza na
mtandao huu, baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika moja za wodi za Hospitali
hiyo wamesema wanalazimika kulala katika magodoro yenye Naironi yasiyo na
shuka jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa afya zao.
Catherine Kilave
amesema wagonjwa wenye uwezo wanalazimika kuchukua mashuka na Blanketi kutoka nyumbani ili kujifunika Hospitalini hapo,
mara tu wanapotakiwa kulazwa.
Catherine
anaongeza kuwa uwezekano mkubwa wa kuibuka kwa magonjwa ya kuambukiza kama
Upele na magonjwa yote ya ngozi kwa kuwa magodoro hayo yanalalilwa na wagonjwa
wa kila aina.
Delila Mtambo
amesema hata mashuka yaliyopo yamekuwa yakichukua muda mrefu kubadilishwa na
idara ya usafi, na hivyo wao kuwa katika hatari ya kupata magonjwa mengine nayale
yaliyowapeleka Hospitalini hapo.
“Tatizo la
mashuka hapa Wodini linatuathiri sana sisi wagonjwa, kwa sababu tunalazimika
kulalalia Naironi hizi ambazo kila mgonjwa amelalia, na kila mgonjwa hapa
amekuja na ugonjwa mbalimbali, lakini hata yaliyopo hayabadilishwi kwa muda,
yanakaa wiki mbili hayajaondolewa kwenda kufuliwa,” Walisema.
Aidha wamesema
uwepo wa tatizo hilo umewafanya baadhi ya wagonjwa kwenda Hospitalini hapo na
mashuka yao kwa lengo la kukwepa maambukizi ya magonjwa yatokanayo na uchafu.
Kutokana na hali
hiyo Umoja wa “Wanakihesa” kikundi cha mjini Iringa kimefika katika Hospitali
hiyo na kutoa misaada mbalimbali, zikiwemo shuka zenye thamani zaidi ya
shilingi laki sita, Maziwa, Sabuni, Mafuta ya kujipaka, Maji ya kunywa, Biscuit
na pipi.
Akizungumzia
msaada huo, mwenyekiti wa Umoja wa “Wanakihesa” Mussa Wanguvu amesema hatua
hiyo ni katika kusherekea sikukuu ya Pasaka, pamoja na kutimiza mwaka mmoja
tangu Umoja huo uundwe.
Wanguvu amesema
misaada hiyo imetolewa na wanachama kwa kuchangia kila mmoja kwa hiari, huku
msaada wa shuka hamsini zikinunuliwa kwa gharama ya shilingi Laki sita, lengo
likiwa ni kupunguza tatizo la uhaba wa shuka katika Hospitali hiyo ya Rufaa
mkoa wa Iringa.
Ernesta
Mgongolwa mmoja wa waanzilishi wa umoja huo amesema wao kama wanachama wanaona msimu
wa sikukuu ya Pasaka ni siku nzuri kutoa misaada kwa wagonjwa, kwani ni moja
kati ya kundi lenye uhitaji mkubwa unaotegemea misaada kutokana na shida
mbalimbali.
Happy Mbegalo mmoja
wa wagonjwa katika wodi ya watoto amekishukuru kikundi hicho cha “Wanakihesa”
kwa umoja wao na hasa kuwakumbuka wahitaji wanaosumbuliwa na maradhi katika
hospitali hiyo.
“Tumefarijika sana
jamani, yaani tunaona mmetujali kuja kututembelea na kuptupa hii misaada,
tunaomba na vikundi vingine navyo viwe vinaona umuhimu wa kuyakumbuka makundi
yenye uhitaji kama wagonjwa,” Alisema Happy.
Juliana
Augustino mgonjwa naye amesema hatua ya kikundi hicho imewafariji wao kama
wagonjwa, kwakuwa imewatia moyo na kuona kama kuna wenzao wanaoumia juu ya wao
kuugua.
Akizungumzia hali
ya uhaba wa mashuka msimamizi mkuu wa shughuli za Hospitali hiyo ya Rufaa mkoa
wa Iringa Elias Kiitu amesema tatizo la uhaba wa mashuka Hospitalini hapo ni
kubwa.
Kiitu amesema
Hospitali ina zaidi ya vitanda 460, huku kila kitanda kikihitaji shuka 8, hali
ambayo kwa sasa kuna shuka 1840 pekee huku hitaji likiwa ni jumla ya shuka
3680.
Aidha amesema msaada
huo wa shuka kutoka umoja wa “Wanakihesa
“ umepunguza
tatizo hilo la uhaba wa shuka katika Hospitali hiyo, huku akiwataka wananchi
kujitolea katika kusaidia Hospitali hiyo katika masuala ya afya.
Kiitu amesema
uwepo wa shuka chache unakwamisha mpango wa usafi jambo ambalo ni hatari, kwa
madai kuwa Hospitali ina wastani wa shuka nne kwa kila kitanda na hivyo kuwa na
nusu ya hitaji halisi.
Hata hivyo
amesema utaratibu wa Hospitali hauruhusu wagonjwa kwenda na Shuka au Blanket
katika Hospitali, na kutokana na hali halisi iliyopo shuka zilizopo hubadishwa
baada ya kufuliwa.
Kikundi hicho cha
Kihesa msimu huu wa sikukuu ya Pasaka, kinayatembelea makundi mbalimbali yenye
uhitaji ikiwa pamoja na kutoa misaada mbalimbali ya kijamii, kama Sabuni,
Maziwa, Juice, Maji ya kunywa, Mafuta ya kupaka, Biscuit na pipi kwa ajili ya watoto.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni