Kibao cha shule ya msingi Ibumila, Iliyopo jimbo la Kalenga, Wilaya ya Iringa.
Kuelekea Ibumila.
Shule ya msingi Ibumila inayotumiwa na wanafunzi 379, ambao sasa wamefunga shule yao kwa utaratibu usio rasmi, walimu wakihofia kuibuka kwa majanga.
Choo mbadala ambacho kinatakiwa kutumiwa na wanafunzi 379
Majengo ya vyoo vya awali ambavyo vilititia
Mashimo ya vyoo hivi si hatari tu kuyatumia, bali nihatari hata kuyasogelea.
Ibumila ikiwa imezizioma baada ya kukosa wanafunzi, kwa kukosa huduma ya vyoo, jambo ambalo linaweza kuibua majanga kwa wanafunzi na Taifa hilo la kesho.
<<<<HABARI>>>>
WANAFUNZI shule
ya msingi Ibumila iliyopo Kata ya Mgama katika Wilaya ya Iringa wamelazimika
kuacha masomo, na hivyo kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi, baada ya shule
kufungwa kwa kuhofia usalama wa maisha yao.
Wanafunzi hao
ambao wamekutwa wakifanya biashara mbalimbali, wengine wakiwa katika mapori
waking’oa Uyoga na baadhi yao wakichunga mifugo zikiwemo Ng’ombe, wamesema wamelazimika
kuwa katika mazingira hayo, baada ya vyoo vya shule kubomoka na uongozi wa
shule kuamua kuifunga shule hiyo.
Rahely
Nyanginywa mwanafunzi wa darasala la kwanza na dada yake Nida Nyanginywa wa
darasa la nne wamesema wanalazimika kufanya biashara ya Uyoga ambao wamekuwa
wakiuuza na kusaidia pato la familia.
Sara Nyanginywa na
Joshua Nyang’inywa mwanafunzi wa shule ya msingi Ibumila wamesema shule yao
baada ya kubomoka walimu waliwataka warudi nyumbani mpaka vyoo
vitakavyokamilika, na muda huo wanautumia kuwasaidia wazazi wao.
Sophina Kihaka mmoja
wa wazazi wa wanafunzi wa shule ya msingi Ibumila ameiomba serikali iwasaidia
ujenzi wa vyoo hivyo ili kuwawezesha watoto wao kuendelea na masomo, kwani hali
iliyopo kwa sasa shuleni hapo ni hatari kwa usalama wa wanafunzi.
Suzan Chilimila
mwalimu wa shule hiyo amesema shida kubwa nikwea wanafunzi wa kike waliobarehe
ambao wanashindwa kumudu haja zao pindi wanapokuwa katika siku zao (Hedhi) na
kuwa kukosekana kwa vyoo ni athari kubwa kwa watoto hao wa kike.
Chilimila
amesema baada ya kubomokam vyoo vya muda ambavyo vilitandikwa magogo juu ya
mashimo, walimu na wanafunzi walijenga uzio wa Nyasi usio na shimo ili
kupatikana kwa huduma ya haja ndogo.
Akizungumzia
tatizo hilo kaimu mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ibumila Wilfred Mheluka
amesema hatua ya kufunga shule imekuja baada ya wanafunzi 379 wa shule hiyo kuwa
hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kama Kipindupindu baada ya kukosekana kwa huduma
hiyo muhimu ya vyoo.
Mheluka amesema
walifiaka hatua hiyo baada ya kuona hatari iliyopo kwa wanafunzi wao, kwani
vyoo vyote vimetitia na hivyo wanafunzi kukosa mahali pa kujistiri kwa haja
ndogo na kubwa.
Aidha amesema awali
waliwataka wanafunzi wa darasa la nne na la saba waendelee na masomo, lakini
idadi ya wanafunzi hao iliwafanya washindwe kumudu uwepo wa vyoo viwili vya
walimu ambavyo walipanga vitumike na wanafunzi hao.
Amesema hali
hiyo ya vyoo vya Nyasi imeonekana ni hatari zaidi kutokana na vyoo vyenyewe
kutokuwa na Mahimo na kipindi hiki cha msimu wa mvua mikojo kutapakaa, jambo
ambalo linaweza kuibua magonjwa ya mlipuko kwa wanafunzi.
Chilimila
alisema tatizo hilo la kukosekana kwa vyoo ni sugu na pia lipo kwa upande wa
walimu, kwani nao hulazimika kurudi nyumbani kujisaidia kutokana na uhaba wa
huduma hiyo ya vyoo, kwa kuwa vilivyopo ni viwili pekee.
“Vyoo hivi kama
unavyoviona, havina staha, mwalimu unaingia wanafunzi wanakuona, havina mlango
juu havijaezekwa, kwahiyo mwalimu ukiingia humo unaonekana, kwa hiyo tatizo
hili la vyoonikwa upande wa walimu na wanafunzi, tunalazimika kurudi nyumbani,
huko nyumbani ukifika unakuta kunamajukumu ndipo hapo unachelewa kurudi shule
na kupoteza vipindi vya wanafunzi,” Alisema Chilimila.
Mwenyekiti wa
serikali ya kijiji cha Ibumila Gidion Kilipamwambu, Mtendaji wa Kata ya Mgama
Willium Msofu na mratibu wa elimu Kata ya Mgama Boazi Ngalutila wamekiri kuwepo
kwa tatizo hilo, na kuwa wanajenga vyoo vya muda vya Nyasi ili kumaliza tatizo
hilo la vyoo.
Msofu na
Ngalutila wamesema kukwama kwa ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo, kunatokana
na migogoro ya mara kwa mara, baina ya wananchi na baadhi ya viongozi wa
serikali ya kijiji, jambo linalokwamisha shughuli nyingi za maendeleo, hususani
jenzi mbalimbali.
Viongozi hao
wamesema suala hilo linahitaji ufumbuzi wa haraka zaidi ili kuwanusuru wanafunzi
ambao kwa sasa ambao wanatangatanga mitaani, huku baadhi yao wakifanya shughuli
hatarishi ambazo zitasababisha kuikosa elimu.
Viongozi hao walikwenda mbali
zaidi na kusema baadhi ya wanafunzi wanaweza wakakumbwa na changamoto
mbalimbali huko mitaani na katika mapori wanapookota Uyoga, na kubwa zaidi ni
wanafunzi wa darasa la nne nala saba kufanya vibaya katika mitihani yao.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni